Rais Samia: Watu 13 wamefariki kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo. Serikali kugharamia matibabu ya majeruhi na kuhakikisha waliofariki wanasitiriwa

Rais Samia: Watu 13 wamefariki kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo. Serikali kugharamia matibabu ya majeruhi na kuhakikisha waliofariki wanasitiriwa

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Rais Samia ambaye amesafiri kwenda Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil 16 Novemba, 2024 kwa mwaliko wa Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20, amezungumza na Wananchi kufuatia kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.


Rais Samia amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuporomoka kwa ghorofa katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Nimekuwa nikipata taarifa za mara kwa mara kuhusu zoezi la uokoaji kutoka kwa Waziri Mkuu na nimekuwa nikifuatilia zoezi hilo kwa karibu zaidi.”

Pia soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa

Amesema “Hadi saa nne asubuhi leo, jumla ya watu 84 wameokolewa na kufikishwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Kati ya hao majeruhi 26 bado wanaendelea na matibabu. Pamoja na hao kwa huzuni kubwa tumepoteza wenzetu 13 katika tukio hilo.”

Aidha ameongeza kuwa “Serikali itabeba gharama za matibabu kwa wote waliojeruhiwa, na kuhakikisha waliofariki wanastiriwa ipasavyo. Nitoe pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na tukio hili. Niwaombe watanzania wote tuwaweke kwenye maombi wote walioathirika na tukio hili na kuwaweka kwenye maombi waliotangulia mbele za haki.”

Salamu za Pole za Awali za Rais Samia: Rais Samia atoa pole kwa waathirika Kariakoo. Aagiza kufanywa kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi

“Serikali itaendelea kutoa taarifa zaido kuhusu zoezi la uokoaji hadi hapo zoezi hilo litakapokamilika. Hadi sasa sababu za kitaalamu za jengo hilo kuporomoka bado hazijachunguzwa na kubainishwa, kwani kipaumbele chetu kwanza ni kuwaokoa wenzetu waliokuwa ndani ya jengo hilo.”

“Nashukuru mashirika binafsi na wananchi wote waliojitolea na waliotoa ushirikiano katika zoezi hilo. Nashukuru pia Madaktari wanaoendelea kuhudumia majeruhi. Nampongeza Waziri Mkuu, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na timu zao kwa kusimamia kazi kubwa ya uokozi.”

“Baada ya uokozi kukamilia, namtaka Waziri mkuu kuongoza timu ya Wakaguzi majengo, kukagua majengo yote ya eneo la Kariakoo na tupate taarifa kamili ya hali ya majengo ya Kariakoo yalivyo.”

Soma taarifa ya mwaka 2013: Magorofa 64 hatarini kuanguka Kariakoo

Aidha, Rais Samia ameagiza Jeshi la Polisi kupata taarifa kamili kutoka kwa Mmiliki wa Jengo lililoporomoka, kuhusu ujenzi ulivyokuwa unafanyika. Aidha, amesema taarifa zote za uchunguzi zitakapopatikana zitawekwa wazi kwa wananchi wote
 
Rais Samia amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuporomoka kwa ghorofa katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Nimekuwa nikipata taarifa za mara kwa mara kuhusu zoezi la uokoaji kutoka kwa Waziri Mkuu na nimekuwa nikifuatilia zoezi hilo kwa karibu zaidi.”


Je, hakuna hatua za kisheria na kinidhamu? Ni kina nani waliohusika na usimamizi na uthibitishaji wa kazi iliyokuwa ikiendelea?
 
Rais Samia ambaye amesafiri kwenda Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil 16 Novemba, 2024 kwa Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20, amezungumza n
Kuna wale wapumbavu wanadhani Samia akisafiri basi na Urais umesafiri 😂😂
 
Back
Top Bottom