Naona exposure inawaponza wasaidizi wa Rais, Rais anataka kila mteule wake afanye vile anavyotaka yeye hata kama hana ujuzi wa jambo husika, hii sio sawa, anakosea.
Mulamula alikuwa na exposure na mambo ya nje toka enzi za JK, na hiyo exposure yake naamini ndio iliyochangia Rais kumpa kile cheo, leo iweje amuondoe yule aliyegoma kuburuzwa kwenye jambo alilo na experience nalo? lililofanya akaaminiwa na kupewa kazi? Rais hajui anachofanya.
Kuwa na wasaidizi maana yake ni kumsaidia Rais, na sio tu kufanya kazi wanazopangiwa, bali hata kwa ushauri pia, hii kauli aliyoitoa Rais itazidi kuzalisha chawa wengi zaidi, wajinga, majeuri, na viburi.
Matokeo yake kina Mwigulu wanazidi kutuburuza na tozo, huku Makamba na Nape na kauli zao za hovyo kila wakati; yeye anataka jambo lolote wakishakaa na kukubaliana serikalini lisipingwe, vyema atambue hata wajinga huwa wana maamuzi yao na yasipoangaliwa mapema yatatuumiza.
Awaache wenye uzoefu wamsaidie, unaweza kuwa na kundi kubwa la wajinga wasiojua chochote kasoro mmoja wao, na kiongozi mzuri anatakiwa kumtambua huyo mmoja.