Rais Samia: Waziri hutakiwi kujitoa kwenye maamuzi ya Serikali

Rais Samia: Waziri hutakiwi kujitoa kwenye maamuzi ya Serikali

Atakuwa bi mkubwa aliyetumbuliwa....
 
Huyu mama akilazimisha kubakia madarakani hiyo 2025, basi mchele utauzwa elfu 6 kwa kilo! Na mafuta ya petrol na dizeli lita itakuwa elfu 6 pia! Vifaa vya ujenzi ndiyo kabisaa!! Vitaendelea kupanda mara dufu.

Nitafurahi kama atakaa pembeni.
Hapana haitatokea kwasababu wakati huo Putin atakuwa ameshakufa zamani na Yukrein kuna aman
 
Waziri halazimiki kutii kila kitu endapo anaona kuna vitu haviko sawa, alipokosea ni kuendelea kubakia madarakani, alipaswa kujiuzulu baada kuona hakuna muafaka. Kusubiri kuondolewa ni kama kuonesha kiburi.
Ila pia kumbuka bongo hapa ukilazimisha kijiuzulu ni kiburi utafatwa na kitengo bora tu ufukuzwe. Kumbuka abduraman alivyotaka kujiuzulu wakamzingira kwake nakutumwa india kutibiwa
 
Moja ya kosa analofanya Raisi nikuamini kuwa kujaza wanawake kwenye NAFASI NYETI kuta-mpromote.

Wanawake wengi hawakai jiko Moja, wataunguzana tu kwa kuzodoana
Kwanza Wanawake hawapendani na wanaoneana wivu sana.

Kwa haraka tu wengi wasiomuelewa ni wanawake,hata hao amewapa ulaji pengine hawamuelewi kabisa.

Ukiacha hili la kututunza kwenye matumbo yao kwa miezi tisa na tukatoka tukiwa watu kamili, wanawake wana maajabu mengine mengi sana.
 
Rais Samia akiwaapisha mawaziri leo, Oktoba 3 amesema waziri hatakiwi kusema hakubaliani na maamuzi ya Serikali au kusema kuwa nimeelekezwa hivi ila sikubaliani. Hatakiwi kujitoa bali kuwa sehemu ya maamuzi.

Sijui ni waziri gani aliyesema haya ni maamuzi ya Serikali sio yangu?
Pia mh. Rais amesema waziri ANATAKIWA ajue mipaka yake
 
Ila pia kumbuka bongo hapa ukilazimisha kijiuzulu ni kiburi utafatwa na kitengo bora tu ufukuzwe. Kumbuka abduraman alivyotaka kujiuzulu wakamzingira kwake nakutumwa india kutibiwa
Tanzania hata mamlaka inayokuteua haiamini kama unaweza kuachilia V8 na maisha mazuri, ukifanya hivyo mamlaka yenyewe inashangaa umewezaje.

Unakumbuka Lazaro Nyalandu alijiuzulu lakini Magufuli na Ndugai wakakomaa mpaka wakahakikisha ubao unasomeka kwamba CCM imemvua ukada?

Usijaribu kabisa kuonesha msimamo Tanzania kwa kujiuzulu, chuki utakayo tengenezewa hutoweza kuibeba.
 
Huyu mama akilazimisha kubakia madarakani hiyo 2025, basi mchele utauzwa elfu 6 kwa kilo! Na mafuta ya petrol na dizeli lita itakuwa elfu 6 pia! Vifaa vya ujenzi ndiyo kabisaa!! Vitaendelea kupanda mara dufu.

Nitafurahi kama atakaa pembeni.
Rais Samia yupo hapa mpaka 2030, Ndio kituo Cha kupumzika, pia hujakatazwa kwenda shambani kulima ili uje uuze kwa Bei unayotaka wewe
 
Tanzania hata mamlaka inayokuteua haiamini kama unaweza kuachilia V8 na maisha mazuri, ukifanya hivyo mamlaka yenyewe inashangaa umewezaje.

Unakumbuka Lazaro Nyalandu alijiuzulu lakini Magufuli na Ndugai wakakomaa mpaka wakahakikisha ubao unasomeka kwamba CCM imemvua ukada?

Usijaribu kabisa kuonesha msimamo Tanzania kwa kujiuzulu, chuki utakayo tengenezewa hutoweza kuibeba.
Hata Chalamila aliomba kujiuzulu wakamkatalia akaanza vituko maksud kulazimisha kutemwa kipindi kile aliamishiwa mwanza hatimaye wakaamua tu aende. Lakini wamemrudisha.
 
Back
Top Bottom