Rais Samia yuko tayari kufanya kazi pamoja na wapinzani

Rais Samia yuko tayari kufanya kazi pamoja na wapinzani

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Mwenyekiti wa CHADEMA Freemen Mbowe katika mkutano wa CHADEMA alisema kuwa aliandika barua kumuomba Rais Samia Suluhu kufanya maridhiano ya kitaifa wakiamini ni njia sahihi ya kufanya kazi na kujenga nchi na Rais Samia alijibu barua hiyo ndani ya siku 3 alilidhia ombi hilo.

Pamoja na kuwa na majukumu mengi ya kitaifa Rais Dkt. Samia Suluhu aliijibu barua ya Mwenyekiti wa CHADEMA ndani ya muda mfupi na kukubali kufanya maridhiano ya kitaifa. Hii inaonyesha ni jinsi gani Rais Samia Suluhu amerejesha Democrasia iliyopotea.

Lakini pia Menyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa amethibitisha kuwa sasa Tanzania kuna Uhuru wa kutoa maoni, kwaiyo kila Mtanzania anauhuru wa kusema chochote anachokifikilia kwasababu Rais Samia Suluhu anaendelea kudumisha uhuru Tanzania.
 
Namna CCM wanavyohangaika CHADEMA ilishinda chaguzi zote from 1992
 
Mh. RAIS Samia ni Mcha MUNGU wa Kweli tena kwa Vitendo kwani Hata Walioonewa na Mtangulizi wake anajitahidi kuwafuta Machozi kuthibitisha kuwa HAKUHUSIKA na MUNGU atambariki sana ktk KAZI yake ya URAIS
 
Namna CCM wanavyohangaika CHADEMA ilishinda chaguzi zote from 1992
Hii nchi ni huru na ni nchi ya kidemocrasia kwaiyo ni sawa wakishinda na Rais Samia Suluhu kwenye 4R anazozitumia katika uongozi wake kuna maridhiano na ndio maana unaona amekubali maridhiano na Chadema
 
kuna tofauti ya maridhiano na mazungumzo
 
Mh.RAIS Samia ni Mcha MUNGU wa Kweli tena kwa Vitendo kwani Hata Walioonewa na Mtangulizi wake anajitahidi kuwafuta Machozi kuthibitisha kuwa HAKUHUSIKA na MUNGU atambariki sana ktk KAZI yake ya URAIS
Rais Samia Suluhu ni kiongozi ambae anaependa kusimamia haki za wananchi wake lakini pia anapenda democrasia ndio maana tunaona anawapa uhuru vyama vya upinzani
 
Rais Samia Suluhu ni kiongozi ambae anaependa kusimamia haki za wananchi wake lakini pia anapenda democrasia ndio maana tunaona anawapa uhuru vyama vya upinzani
Uhuru gani ambao anavunja katiba aliyoapa kuilinda nchi hii ni vyama vingi mbona anakataza CHADEMA kufanya mikutano ya hadhara!!!
 
Uhuru gani ambao anavunja katiba aliyoapa kuilinda nchi hii ni vyama vingi mbona anakataza CHADEMA kufanya mikutano ya hadhara!!!
Na ndio maana unaambiwa viongozi wapo kwenye maridhiano kwaiyo kila kitu kitakuwa sawa uhuru upo kwasababu watu wanaongea watakavyo na haujasikia kunamtu amekamatwa
 
Ndio lakini Chadema wanafanya maridhiano na Serikali ya Rais Samia Suluhu

..wanafanya mazungumzo.

..maridhiano ni suala jingine.

..huenda Raisi haelewi maana ya maridhiano.

..maridhiano huhitaji TUME YA HAKI NA UKWELI kama ile iliyoundwa Afrika Kusini miaka ya 90.
 
Na ndio maana unaambiwa viongozi wapo kwenye maridhiano kwaiyo kila kitu kitakuwa sawa uhuru upo kwasababu watu wanaongea watakavyo na haujasikia kunamtu amekamatwa

..mikutano ya hadhara bado imezuiliwa kinyume na katiba na sheria.

..mwambieni Raisi ailinde katiba kwa kutengua zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
 
Kwa vyovyote, kuna utofauti mkubwa kati ya Rais Samia na mtangulizi wake. Mtangulizi waje alivuka hata ule mstari wa kiongozi mbaya, akahamia kwenye ukatili.

Lakini Rais Samia anatakuwa kufanya zaidi na kwa spidi zaidi ili aweke alama itakayokumbukwa vizazi vingi vijavyo. Akitaka, Tanzania inaweza kutaka Taifa lisiloeleweka mpaka kuwa Taifa imara katika haki, uhuru, demokrasia na uchumi. Na akitaka kulifanya hilo ni lazima awe na moyo mgumu kwa sababu wapinzani wa haki, wale waliozoea dhuluma, hasa ndani ya CCM, ni wengi sana.
 
..mikutano ya hadhara bado imezuiliwa kinyume na katiba na sheria.

..mwambieni Raisi ailinde katiba kwa kutengua zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
Labda anaenda hatua kwa hatua. Amewaachia wale ambao dikteta Magufuli aliwafunga kwa kuwaonea. Baada ya kukamilisha hilo, sijui atakuja na lipi, la mikutano ya vyama vya siasa, au katiba au Tume Huru ya Uchaguzi. Katika kila jema, Rais ajue yupo pamoja na watu wote wapenda haki na wenye dhamira njema na Taifa hili.
 
..anakwenda taratibu mno ili hapo baadae aseme hakuna muda wa kuunda Tume huru na kuandika katiba mpya.

..hatua alizochukua ilikuwa ni kwa ajili ya kuzilaghai nchi wahisani kuwa utawala wake ni tofauti na ule wa Magufuli.

..lakini jinsi muda unavyokwenda matendo yake yanadhihirisha kwamba hana nia ya kufanya mabadiliko ya kweli, na ya kimsingi, kuondosha dhuluma za Ccm dhidi ya vyama vya upinzani.

NB:

..kwenye kikosi kazi watu wa Ccm na serikali wamekwamisha mapendekezo ya kuundwa kwa Tume Huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom