Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki kikao kazi cha Mabalozi na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje leo tarehe 19 Novemba, 2022 katika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar
SEHEMU YA MAZUNGUNZO YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA MABALOZI WANAOWAKILISHA TANZANIA NJE YA NCHI
Kuhusu Kuhudhuria kwao.
Nimefarijika sana kujua wote mmeitika wito wa mkutano huu na kwamba mabalozi wote mnefika salama wasalimini. Nimefurahi kuwaona wote kwa ujumla wenu. Hii ni fursa adhimu ya kukutana na wote.
Kuhusu Sera Za Nchi.
Nchi yetu kama zilivyo nchi zingine ina sera kuu 2, ambazo ni sera za ndani ambayo hujumlisha sera zote za ndani zenye lengo la kuendeleza na kustawisha taifa letu. Sera hizi ama ni za maendeleo ya kiuchumi ama ya kijamii ambazo hutengeneza kile tunachokiita maslahi ya Taifa. Kama walivyofanya watangulizi wangu, hii ndiyo dhima ninayoiendeleza. Naangalia mema yaliyopita na mema yaliyopo ambayo tunayatekeleza na kupanga maboresho kufanya mema tunapokwenda.
Sera ya pili ni ile ya mambo ya nje ambayo hutafsiri sera ya mambo ya ndani katika mawanda mapana ya Sera za kimataifa kwa maslahi ya taifa letu.
Mabalozi aliochagua.
Katika kipindi cha mwaka 1.5 tangu niwepo madarakani nimeteua mabalozi 61. Idadi hii ni pamoja na walioongezewa mikataba, kati yao 16 wakiwa ni watumishi wa kada ya nje, katika hao wanawake ni 13 na vijana chini ya miaka 45 ni wanne.
Mimi nimekwenda chini ya miaka 45, hapo nyuma tumewahi kuwa na balozi mwenye miaka 21. Ni rekodi ambayo bado haijavunjwa bado kwa ndani, sijui nje.
Kuongeza balozi Nje.
Sambamba na kujaza nafasi tumepanua uwakilishi wetu nje kwa kuongeza ubalozi mpya wa Indonesia na consul Lubumbashi DRC na Guangzhou China. Kupanua huko kumeenda sambamba na kuongeza ushiriki wetu katika mikutano ya kimataifa inayoamua mustakabali wa Dunia na kuathiri maslahi yetu pamoja na ziara za kimkakati zenye lengo la kufungua zaidi fursa za kiuchumi na mashirikiano baina ya nchi yetu na nchi jirani au nchi marafiki.
Mabadiliko ya sasa ya Kidunia.
Sera yetu ya mambo ya nje ina miaka 20 sasa, pia mkutano wa mwisho wa mabalozi ulikaa miaka 4 iliyopita, katika kipindi hiki kuna mambo mengi yamebadilika ndani ya dunia hivyo ni muhimu nasi tukikaa ili tuone kuiangalia sera yetu yenye miaka 20 Je, bado ina mashiko kwenye mabadiliko ya dunia ya sasa hivi.
Mojawapo ya mabadiliko mapya ni matishio mapya ya usalama na ustawi wa nchi yetu yakiwemo mabadiliko ya tabia nchi, majanga ya afya, uhalifu wa kimataifa na mapinduzi ya nne ya viwanda ni mambo ya kukaa na kutafakari.
Pia, kurudi kwa siasa za kuvutana baina ya mafahali wa dunia na kutaka kuziburuza nchi za afrika katika migogoro yenye maslahi yao, na athari ya migogoro hiyo kwenye bei ya nishati, vyakula na sarafu duniani kote.
Mengine ni kubadilika kwa mwendendo wa uchumi wa dunia ambapo bara la Asia kwa sasa linazalisha takriban asilimia 40 ya pato la dunia yaani GDP, Kuongezeka kwa kasi ya utangamano kwa nchi za Afrika ikiwemo kuongezeka kwa nchi zinazounda EAC kwa kuongezeka wanachama kutoka 5 hadi 7, kuanza kutekelezwa kwa itifaki ya soko huru la Afrika pamoja na kuibuka kwa mahitaji mapya ya ndani ikiwemo kukua kwa Uchumi wa blu, kutanuka kwa matumizi ya lugha ya kiswahili, Uchangiaji wa Diaspora nyumbani na maslahi yao huko waliko.
Mabadiliko haya ni makubwa na ili kuendana nayo tunapaswa kujipanga upya na ikibidi kujipangua. Tujipange na kujipangua.
Hatuna budi kujipanga kukabiliana na mabadiliko hayo, sera yetu kuu ioanishwe na mabadiliko haya na yale tuliyoboresha kwenye sera zetu za ndani. Swala lingine ni kuongeza uwajibikaji, kuongeza ushirikishwaji wadau wote muhimu wa Serikalinna wasio wa Serikali ili kuhakikisha diplomasia yetu inakwenda na wakati, kwa ubora na ufanisi.
Suala lingine ni kuajiri na kunoa waliopo ili kuhakikisha kada zote zinazoipa uhai diplomasia yetu zina uwakilishi kwenye wizara zetu.