Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Rais Trump amesaini amri ya kuiondoa Marekani kwenye uanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Wamejitoa!?!?sasa ARV itakuwaje?
Ninyi si mlibeza kikombe cha Babu? Mkatunga na uongo kwamba, waliokunya wamekufa... akati kuna watu wengi walokunywa wametoa ushuhuda wamepona...

Hahahaha! Tena wakati mnamkashifu mliona siifa wenyewe... mmesimamisha vichwa juu kama nguchilo... na wazungu wakawapigia makofi mkasema yess.... sasa ndo mkome na mjue bure siku zote ni ghalama
 
Nitoke nje kidogo ya ninachotaka kuelezea. Biden alisaini hii kabla ya kuondoka Ikulu.

IMG_0103.jpeg
 
Hii inatoa ishara kubwa miradi mingi ya afya hapa Tanzania huenda ikadorora, hususani HIV, Malaria, uzazi salama, TB na tafiti za afya.
WHO wana wafadhili, wanao jitoa ni Serikali ya USA ila wafadhili binafisi hata walioko Marekani wataendelea kufadhili WHO
 
Hii inatoa ishara kubwa miradi mingi ya afya hapa Tanzania huenda ikadorora, hususani HIV, Malaria, uzazi salama, TB na tafiti za afya.
Kabisa mkuu. Naiwazia Basket Fund inavyo tusaidia huku Afya.
 
Itasaidia na watu kuwa makini maana saivi mwenye ukimwi na mzima huwezi kumtofautisha
Bradha dunia lazima iendelee maana arv zinachochea ukimwi.Watu wanapata nguvu kisha wanaendelea kuueneza waachwe wafe.
 
kumbuka wakati akiwa rais mara ya kwanza,alizuia fedha za marekani lakini hatukudorora
Tulidorora aisee,ni vigumu huku kada ya Afya kutegemea Makusanyo ya papo pekee na bima ili kuweza kutekeleza activities zote muhimu.
 
ARV siku zote zinauzwa. Wanachokifanya Serikali ya Marekani kupitia PEPFAR, ni kununua haya madawa kutoka kwenye kampuni kubwa za Madawa halafu wanatugaia kama Msaada as part of their "soft policy" bure. Offcourse baadae lazima upanue.

Athari ni ndogo sana. Almost none. Msaada wa ARV's kutoka marekani ni Direct Funding na hazipitii WHO. Nimehakikishiwa PEPFAR itakuwepo, anagalabu kwa sasa.

Kuku wanakufaje?🤣
Nashukuru kwa ufafanuzi kuhusu ARV, kwasisi tunaopenda chini angalau hatukuwa na hofu tukiukwaa dawa nafuu zitapatikana, zikiwa gharama au pungufu hali itakuww tete. Kuku wanakufa hivi👇
FB_IMG_1737436261050.jpg
 
Bradha dunia lazima iendelee maana arv zinachochea ukimwi.Watu wanapata nguvu kisha wanaendelea kuueneza waachwe wafe.
Wanavyosema wataalam ARV hazichochei UKIMWI zinapunguza.

HIV inasambazwa zaidi na watu walioambukizwa miezi kadhaa iliyopita kuliko wanaojua kuwa wana HIV na kutumia hayo madawa.

Mfano, watu woote wenye UKIMWI na HIV wakijulikana wakatumia dawa maambukizi yanaweza kukoma.

NB: Binafasi hili gonjwa naona limekaa kimkakati sana tangu liingie, pengine hata lilikuwepo ila halikuwa na madhara mpaka lilipofanywa biashara.
 
kwani kuna ubaya? trump ni mwendawazimu ambae atafeli vibaya
Utasubiri sana mpaka uzeeke ila Donald Trump ndiye ATAFANIKIWA sana katika marais wote wa kuanzia mwaka 2000. Sababu hizi hapa:-

1. Ni mtu wa kutaka suluhu zaidi katika migogoro kuliko vita. Kumvuka kuwa toka kugawanyika kwa South na North Korea yeye ndiye Rais pekee aliyeweka mguu North Korea

2. Hapepesi macho katika kukemea vutendo vya ushoga, kubadili jinsia na na ndoa za mashoga

3. Siku 2 kabla ya kuapishwa vile vita vya kihayawani kati Hamas na Israel vimesitishwa

4. Vita vya Ukraine na Russia ambavyo vimeathiri bei ya petrol hadi kwenye nchi zetu navyo vitakoma pengine kabla ya tarehe 01/ 02/ 2025
 
Back
Top Bottom