Rais Tshisekedi siku zake zinahesabika

Hii ni fedheha kwa nchi kubwa kwa idadi ya watu, raslimali na eneo kama DRC kudharauliwa na ka nchi kadogo!
Kinachowamaliza wakongomani ni mambo matatu hapo chini:
1) Kwanza hawana umoja kama taifa, mkongo wa kinshasa hajishughulishi na yanayoendelea Goma na wa Goma hana muda na yanayoendelea Lubumbashi. Wanaoongea lingala wanajiona ndio wakongo original huku wakiwaita wenzao wanaoongea kiswahili kuwa ni watanzania au warundi. Wanaoongea kiswahili nao wanawaona wale wa lingala kama washamba fulan japo wamezaliwa capital centre lkn wanashindwa ujanja na maarifa na wale waliozaliwa katika miji mingine kama vile Lubumbashi, Katanga nk. Ndio maana unaona maelfu ya watu wanakufa huko kivu katika mapigano wakati huo huo Fally Pupa yupo zake kinshasa anatumbuiza, hajui, hajali au kuguswa na kile kinachoendelea huko mashariki mwa nchi yao.

2) Pili wakongo wamebezi sana kwenye mambo ya starehe kama vile ulevi, kwenda club kukata rhumba kiliwanzenza nk. So linapokuja swala la kuwataka kupigana wanakuwa hawana option nalo ni ile tu sometimes wanajikuta wanalazimishwa tu kupigana ili kuokoa maisha yao, familia zao nk.

3) Tatu serikali imewekeza sana katika mambo mengine yasiokuwa na maana huku ikiacha yale ya msingi kama vile ya ulinzi kujiendea tu kiholela kwa kuamini kuwa yanayoendelea huko kivu hayawezi kuwafikia wao walio katika serikali kuu huko kinshasa.

Kwahiyo tusitegemee kuona maajabu yoyote kutoka kwenye jeshi la Congo pale watakapoingia vitani na Rwanda, sanasana utakuta askari wa Congo akivua magwanda kutupa silaha na kujichanganya na raia kukimbilia Tanzania au Burundi kuomba hifadhi ya kikimbizi.
 
Nchi zilozo peleka jeshi mashariki mwa Kongo Ni Kenya ,Burundi , South Sudan .kwanin Tanzania na Uganda hawahangaiki na Vita hvyo ?

Nguvu ya jeshi ya kusimuliwa ni kama kilimo Cha tikiti kwenye PDF havijawahi kua na uhalisia kwenye utekelezaji
Tumeshaanza kulichokoza limekaa kimyaaa halijibu dawa yake amwagiwe mvua tu sasa kama achokozeki tu nafanyaje ni mvua tu au awaambie M23 waondoke kwenye nchi ya watu upesi sana na awaambie THE GIANT HAS AWAKE AND NO SHAMBA LA BIBI
 
Inawezekana mkuu, ushindi wanaoendelea kuupata M23 dhidi ya jeshi la Drc unashangaza Sana, huenda kuna mkono mzito nyuma yao.
Mkuu baadhi ya sababu za serikali ya Congo na jeshi lake kuburuzwa na vijana wa M23 wasiozidi hata elfu 5 nimezielezea kwenye post namb #201
 
subirini mambo yachanganye makombora yakishapishana vya kutosha angani suluhu kubwa itakayotoka jumuiya za kimataifa ni kuigawa Congo.

Congo itagawanywa beleave or not,Goma itakua mji mkuu wa Congo mpya itakayo megwa.
wanaotawala Dunia wapo karibu zaidi na mgogoro huu kuliko tunavyofikiria na itakua kile wanataka kiwe pale Congo.
Kagame siku akiachia Urais Rwanda basi jua mission ya kuimega Congo imetimia.
 
Kenya , Tanzania, Uganda. Mmekuwa wajinga sana Mmeingiza Ma-nchi yenye migogoro kwenye EAC ...hamtaenda mbali kwa style hii
 
Haina ubavu kivipi na wakati mapandikizi yake yanaihenyesha Congo mpaka leo? Je ikiingia mzigoni yenyewe Rwanda si ndo Tshisekedi atakamatwa kiulaini kama njiwa yatima.
Mapambano ya waasi ni tofauti kabisa baina ya jeshi na jeshi.
Waasi wanapiga kwa kushtukiza wakizidiwa wanajichanganya na raia ni ngumu sana kuwamaliza wote.
Jiulize Marekani na ubabe wake wote ilimchukua miaka mingapi kumnasa Osama Bin Laden ?
Marekani aliingia Afghanistan kupambana na kundi la Taliban,pamoja na kuwatoa madarakani lakini mwaka jana jamaa wamerudi tena madarakani.
Tukiongelea vita ya Taifa la Congo dhidi ya Rwanda ni tofauti kabisa na mapambano dhidi ya waasi.
 
Uchawi kwenye Risasi haufanyi kazi Mzee...sisi tulishafunzwa na Kinjekitile Ngwale Wakongo wao mpaka wana Vikundi vinaitwa "Mai Mai" yaani Maji maji[emoji38][emoji23].
Tafuta mtu aliyeenda ile commission ya kupigana na M23 ikiongozwa na Mwakiborwa. Waasi wa M23 ni wachawi. Hafi mpka masasi ipige na kivuli. So unapiga bodi unapiga chini.

Mwakiborwa alitumia zaidi mizinga mtu na kivuli chake wote jehanum.

Nimehadithiwa.
 
Urusi hapambani na Ukraine anapambana na nato na marekani
Nato na Marekani hawapo Ukraine wala hakuna hata askari wao hata mmoja aliyekamatwa wala kuuwawa na warussia nchini Ukraine.

Askari wa Russia hawana morali ya kupigana vita vya dikteta Putin na ndio maana sasa hivi huyo dikteta amepeleka maaskari maalum wa kuua wale watakaojaribu kukimbia vita.

Russia imeshindwa vita tu na wala wasisingizie Nato wala Marekani kwa sababu Ukraine ana haki ya kununua silaha nchi yoyote kwa ajili ya kupigana vita vyake na Russia sawa na Russia anavyopata silaha kutoka nchi zingine hata Tanzania wakati tukipigana na Uganda mwaka 1978/79 silaha tuliagiza kutoka nje.
 
Kenya , Tanzania, Uganda. Mmekuwa wajinga sana Mmeingiza Ma-nchi yenye migogoro kwenye EAC ...hamtaenda mbali kwa style hii
Lengo la kuuingiza Congo kwenye jumuiya yao, ni kupata mwanya kwa nchi zile ambazo zipo mbali na nchi hii kama vile Kenya wapate fursa ya kupeleka jeshi Congo kwa mgongo wa jumuiya ya EAC afu na wao wachote vya kuchota wapeleke kwao kuendeleza uchumi wao.

Dunia nzima ishajua kwamba Congo sasa ivi ni shamba la bibi, kikubwa ujue utaingia vipi tu ndani ya ardhi yao kupitia amri ya mamlaka ili uibe kiulaini.
 
We umeambiwa na nani?

Hizi imani zilishashindikana kwenye Medani tokea enzi ya Vita vya Maji Maji.

Uchawi kwenye Gunpowder haufanyi mzee.
Watu wamekuwa wakihadaika kupitia movie za kinigeria . Uchawi na risasi wapi na wapi. Ndio maana majambazi wengi wamekuwa wakiuwawa baada ya kudanganywa na waganga wa kienyeji kuwa akiiba akipigwa risasi hatokufa.
 
Sasa basi... Rwanda ina uwezo wa kuichakaza na kuisambaratisha Congo kijeshi kwa njia zote, iwe kwa angani, majini au ardhini tena kwa muda mfupi sana.

JF TEENAGERS ingeanzishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
RPF wana jeshi bora Sana, ndani ya wiki tu wanafika hapo Kinshasa. Ukweli usemwe
 
Wanajeshi wa DRC kwanza hawana nidhamu.
Ni kawaida sana kumkuta coplo anamvimbia Kanali au kupigana ngumi kabisa ndani ya jeshi la DRC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…