Rais Tshisekedi siku zake zinahesabika

Vijana wa tolu lazima mfumuliwe safari hiii
 
Namshauri DRC aimarishe Kwanza ujasusi WA ndani na nje , akifanikisha hili mbona Rwanda anachapwa asubuh
Pia DRC akiimarisha ujasusi wa nje atasaudiwa na WA Hutu kumtoa kagame madarakani
Ndoto hii naona ilishindikana zaidi ya miaka 20 iliyopita. Sidhani kama itawezekana leo.
 
Nusu ya Jeshi la Congo DRC ni Wanajeshi hewa, na mishahara wale hewa ndio wanaingiziwa haraka kuliko Wanajeshi kamili inachelewa sana au hawapati kabisa.

Ammo wakipewa wanawauzia Mai mai FLDR na Vikundi vingine vya Waasi huko Ituri, sasa tuulizane kuna Jeshi hapo?

Hata ukiwajengea Jeshi Serious wanarudia kule kule Majenerali wako Kinshasha wanakata viuno kwa Fally Ipupa.
 
Kabila mkubwa kilichomuangusha ni kukubali Kagame kumchagaulia Walizni
 
Ni sahihi,Wakati wa Mobutu alijua ana wanajeshi elfu 60, lakini mshauri wake wa usalama anadai idadi kubwa ilikuwa hewa,alitaka kuhesabu askari wote ila majenerali ambao ndio walipiga hiyo mishahara wakawambia wanajeshi wanataka kufukuzwa,then majenerali wakamuonya Rais kuna uhasi unakaribia hivo zoezi lile likafa
 
Bora wewe umeongea ukweli. Ukubwa wa nchi sio ndio uwezo wa kijeshi.
Nchi inaweza kuwa kubwa na ikachakazwa na kanchi kadogo kama wilaya yake, na watu wakashangaa.
 
We ni mmoja ya wale vijana wa slim mlio pandikizwa umu JF
Mimi sio na kamwe siwezi kuwa mmoja wao. Hapa naongelea uhalisia wa kile kitachotokea endapo Congo itathubutu kuingia vitani na Rwanda.
 
Hakuna kikindi cha waasi hapa Duniani kina weza shindana na Serikali yoyote na kikaweza!. Kinachofanyika ni Serikali za Nchi na Nchi zinapigana proxy wars kwa mgongo wa vikindi vya waasi.

Na jinsi siasa & chumi za Dunia zinavyoondesha kwa hadaha basi Wananchi wengi katika mataifa mengi,huamini uongo unaosema na kutangazw na vyombo vya habari kama ndio ukweli.

Ukweli ni kuwa Kagame na Rwanda yake wanatumiwa na western kuivuruga Kongo.
 
Mkuu endelea kumuingiza maboya Tshisekedi, mwisho wa siku yatakayomkuta ni yeye sio wewe mzungumzaji.
Hivi huwa mnaandika nyuzi kuelemisha na kuelemishwa au??,hivi inakuwaje MTU anaelimishwa kwa jambo ambalo watu wengi sana uelewa nalo kuliko wewe afu wewe unaendelea na maeneno ya shombo.unaonekana hauko serious!!
 
Kagame mnamtukuza mno.
 
Kwa namna yoyote ile Rwanda hawezi ipiga Congo, ila Congo ni raisi sana kuipiga Rwanda. Njia pekee Rwanda anaweza shinda vita na Congo ni kwa kumu eliminate Tshekedi, otherwise Rwanda mwenyewe hayupo tayari Kigali ifumuliwe aanze ijenga na upya.
Kama wameshindwa kukifumua kikundi kidogo cha M23, basi wasahau kufanikiwa kuvuka hata mpaka wa Rwanda.
 
Mimi sina uhusiano wowote na wanyarwanda ila ninachofanya hapa ni kuandika uhalisia wa kile ambacho kitatokea endapo Tshisekedi ataingia mkenge kwa Paka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…