Rais Tshisekedi siku zake zinahesabika

Rais Tshisekedi siku zake zinahesabika

Wakati wa Mobutu, alipeleka Majeshi yake Rwanda kwenda kupambana na RPF. wakachapwa, baada ya Serikali ya Rwanda kuondolewa na Waasi, Jeshi la zamani likakimbilia DRC, na mimi naamini mpaka leo linalindwa na elements kwenye Regime ya Kinshasa.
Fdlr wapo DRC
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Kweli kabisa mkuu. Mambo ya Kijeshi ni ya kukalia kimya tu. Yangekuwa marahisi basi urusi angeshaichakaza Ukraine ndani ya wiki mbili tu. Ila tizama vita inamaliza mwaka sasa.

Ndio maana sipendi kabisa kuongelea haya mambo
urusi anapambana na nchi zaidi ya 30 (NATO)
 
Ukiniuliza mimi kwenye vita kamili isiyo ya kujificha kati ya Rwanda na DRC nani anashinda nasema ni DRC endapo hakuna external influence baina ya pande zote mbili.

Congo ukitaka kuipima kwa kuangalia eneo lake la Mashariki utapotea, itazame nchi nzima hadi kule Magharibi. Mashariki ni kama imepotezewa na ina waasi wengi wanaojificha na kusumbua kila wakijisikia. Wakipigwa wanavaa kiraia wanalima, wakipata support wanaanza mapigano. Ukija kwenye vita ya nchi na nchi hapo hujifichi, madaraja tunajua yalipo, kambi zilipo, airbase ilipo, HQ, defensive lines na mambo mengine.

Congo sio wazembe kuliko nchi nyingi za Kiafrika, tatizo lao wana rasilimali nyingi na bahati mbaya ya kunyonywa na mataifa ya nje, ila nchi nyingi za Afrika hazina unafuu kijeshi kuwazidi. Hakuna nchi ina makundi ya waasi hadi 10 kama Congo ilivyo, logistics za kuipiga Congo kuanzia mpakani kwa Rwanda mpaka katikati ya nchi kule ni gharama kwa Rwanda. Rwanda kuipiga Congo sio rahisi hata kidogo
Uchambuzi wa kisomi huu[emoji106]
japo Kule Ukraine vs Russia tunapingana sana[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswala ya vita yaache tu yaani unaweza dharau Ila ukatembezewa kichapo Cha karne na underdog wa dunia kwenye vita na usiamini.

Hakuna vita nyepesi. Kama wamejiandaa kulea yatima na wajane wa kutosha basi wapigane.

Ni rahisi sana kuingia vitani sekunde tu ila vita haviishi ndani ya sekunde itachukua muda mrefu mambo kurudi kawaida
Sahii kabisa
Vita haitabiriki mkuu[emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ww jamaa unajua ni gharama kiasi gani zina itajika kuendesha vita na nchi yenye eneo kubwa kama kongo?

Hata Tz hana uwezo wa kuhimili gharama za vita dhidi ya nchi kubwa kama kongo sembuse Rwanda?

Kiufupi Rwanda haina ubavu wa kuivamia Congo.
 
Kwa nini mnaanzisha threads kwa stori za vijiweni?
Kofii akikoroma kwenye zile nyimbo zake unaweza ukahisi jamaa ana weledi mkubwa wa kumsambaratisha adui yake muda wowote.

Kumbe jamaa ni mtalaam wa kukata tu mauno kwenye shoo mbali mbali duniani. Wakongo wanasikitisha sana.
 
Ndombolooooo ndombolo ya solo![emoji849][emoji1787][emoji1787] Na niwachawi kweli ila nadhani wana experience kubwa ya mapigano maana kule kumekua na machafuko mara kwa mara
Wazee wa chivunduuuu, ila wakisikia mlio wa risasi wanajificha ndan ya sifuria.
 
Hivi ww jamaa unajua ni gharama kiasi gani zina itajika kuendesha vita na nchi yenye eneo kubwa kama kongo?

Hata Tz hana uwezo wa kuhimili gharama za vita dhidi ya nchi kubwa kama kongo sembuse Rwanda?

Kiufupi Rwanda haina ubavu wa kuivamia Congo.
Haina ubavu kivipi na wakati mapandikizi yake yanaihenyesha Congo mpaka leo? Je ikiingia mzigoni yenyewe Rwanda si ndo Tshisekedi atakamatwa kiulaini kama njiwa yatima.
 
Wa tanzania mbona muna tuzarau sana sisi wa Congo kwanini ? Tuna uwezo kumizidi ata nyinyi wa Tz ki jeshi [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]View attachment 2407994
Screenshot_20221106-013753.jpg
 
Ni ngumu sana, congo ina walinzi royal sana mfano bodyguards wa Rais Mobutu ukitazama mahojiano yao utaelewa,wale jamaa walipewa kiapo cha kufa kwa ajili ya Rais na walikuwa hawaogopi kifo

Kabila mkubwa alijichanganya akaweka vilinzi vitoto visivyo na mafunzo yoyote ndicho kilimuangusha
Mlimpa ulinzi na kuwa royal kwa yule dictator na mwizi aliyewaibia, kuwatia umaskini na kuwaua kwa miaka zaidi ya 30, hata kama hampendi Kagame lakini mumshukuru maana ndio aliwaondolea yule dictator, na akili zenu zilivyo fupi badala ya kujenga nchi yenu mkaenda kujiunga na wale wapumbavu wa FDLR na kuanza kuua banyamulenge ambao ni wacongo wenzenu, jengeni nchi yenu na kaeni chini na M23 na factions zote muelewane, kusingizia Kagame matatizo yenu kila siku haiwasaidii na mnajua kabisa Rwanda interest yao ni wale wauaji waliokimbilia Congo mnaowapa hifadhi, ndege za wazungu zinabeba mamilioni ya madini kila siku kutoka Congo lakini wanasiasa wenu wamewadanganya kuimba Kagame na nyie mnakubali, amkeni wapuuzi nyie
 
Kofii akikoroma kwenye zile nyimbo zake unaweza ukahisi jamaa ana weledi mkubwa wa kumsambaratisha adui yake muda wowote.

Kumbe jamaa ni mtalaam wa kukata tu mauno kwenye shoo mbali mbali duniani. Wakongo wanasikitisha sana.
Ok, sawa
 
Haina ubavu kivipi na wakati mapandikizi yake yanaihenyesha Congo mpaka leo? Je ikiingia mzigoni yenyewe Rwanda si ndo Tshisekedi atakamatwa kiulaini kama njiwa yatima.
Ww jamaa huna unalo lijua wala hauna uwelewa wowote kwenye medani ya kivita ndio maana unachukulia vitu kirahisi tu.

Rwanda kwa sasa anacho kifanya ni anapigana vita na kongo kwa kutumia mawakala ambao ni hao waasi kwa hiyo anatumia gharama ndogo sana, lakini mambo yatabadirika pale itakapo amuwa kuingia kwenye vita kamili kwa kulihusisha na jeshi lake moja kwa moja.

Alafu kingine unacho takiwa kujua ni kwamba ni sehemu ndogo tu ya jeshi la kongo ndo ipo mashariki mwa kongo kupambana na waasi na sio jeshi zima.
 
Back
Top Bottom