Rais Tshisekedi siku zake zinahesabika

Rais Tshisekedi siku zake zinahesabika

Wakuu inakuaje? sasa twende kazi.

Siku mbili tatu hizi kumekuwa na hali ya sintofahamu kati ya serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na ile ya Rwanda, kila mmoja akimtupia lawama mwenzake na kutishia kuvunjilia mbali uhusiano wao wa kidiplomasia nk.

Kwa upande wa Congo ndio wanaonekana kuwa wamechukia zaidi hadi kupelekea serikali yao kumfukuza nchini kwao balozi wa Rwanda, na pia kumwata balozi wao aliekuwa nchini Rwanda.

Kwa upande wa Rwanda yenyew haioneshi kupanic wala kuchukizwa kivile, inaonekana ime relax ikisubiria kuona kingine kitachojiri kutoka katika serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Sasa basi... Rwanda ina uwezo wa kuichakaza na kuisambaratisha Congo kijeshi kwa njia zote, iwe kwa angani, majini au ardhini tena kwa muda mfupi sana.

Congo inaweza kuishinda Rwanda kwa maneno tu, maana wakongomani ni waimba miziki na wachezaji wakubwa, ila linapokuja swala la mapambano ya kijeshi na weupe sana wanashindwa hata na Burundi.

Kwanza toka Congo ilipopata uhuru jeshi lake halikuwahi kushinda vita yoyote ile. Wakati wa Mobutu jeshi la Congo lilichakazwa vibaya na waasi waliokuwa wanaongozwa na hayati Desire Kabila (father) na baadae jeshi hilo limeendelea kuchakazwa na makundi mbali mbali ya waasi wengi wao ni kutoka nchi jirani.

Sasa jiulize ikiwa nchi yenye raia zaidi ya milioni 1 inachakazwa na waasi wasiozidi elfu 5, huku waasi hao wakiwa na silaha za kuunga unga na mazoezi ya msituni yasiokuwa rasmi. Je watakapoingia kwenye vita na nchi yenyewe si ndo yatakuja kutokea yale ya Mobutu na Idi Amini!!

Hivi kweli Tshisekedi anaamini kuwa nchi yake inaweza kuipiga Rwanda au ndo kifo kinamwita, au wazee wa kazi (Kabila's team) wanamshauri ujinga ili akipigwa akikimbia Kabila arudi kuongoza Congo?

Maana katika hali ya kawaida haiwezekani nchi inayoshindwa vita na waasi elfu 3, ijidanganye kuwa inaweza kupambana na nchi yenye wanajeshi zaidi ya laki, wenye ueledi mkubwa wa kivita, silaha za kisasa na wanajeshi wa kutosha.

Katika EAC nzima, nchi ambazo Rwanda inaweza kuhofia kwa namna fulani kupambana nazo ni Tanzania na Kenya tu ambazo majeshi yao yameshafanya mambo makubwa ndani na nje ya mipaka yao Tanzania ikiwa inaongoza kwa kufanikiwa oparation mbali mbali katika nchi za Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia, Comoros nk. Ila hizo zingine Rwanda inaziona kama vile ni nchi zinazolindwa na makundi ya sungu sungu tu na sio wanajeshi kamili.

So chonde chonde Tshisekedi watu bado wanakuhitaji uendelee kuwa raisi wao. Usije kuingia kwenye mtego ambao utashindwa kujinasua. Kagame alimhofia Kikwete tu mjeshi mwenzake na anajua watu wa kicheka cheka kama JK maamuzi yao yanakuwaga na athari kubwa kwa wengine. Lakini nyinyi wengine anawaona vikaragosi wake.

Tena kwa Congo ndo kabisa hawezi kutuma jeshi lake kupoteza muda wao. Sana sana ataajiri vijana kutoka katika makampuni mbali mbali ya ulinzi waje kumaliza kazi.

Pichani juu ni jeshi la Rwanda na picha ya chini ni jeshi la Congo.

Siku njema kwa wasomaji na wachangiaji wote. Asanteni.
🤔🤔🤔
 
Rwandan Genocide - Facts, Response & Trials - HISTORY Rwandan Genocide | HISTORY
Genocide ilianza baada ya ndege ya rais kudunguliwa,alidungua nani?..1994 palikua na watusi laki 8 rwanda,inadaiwa waliuawa watu zaidi ya 1m watusi wengi na wachache wahutu wenye msimamo wastani,kwa facts hapakutakiwa kuwa na watutsi Leo rwanda zaidi ya rpf
 
Hivi ww jamaa unajua ni gharama kiasi gani zina itajika kuendesha vita na nchi yenye eneo kubwa kama kongo?

Hata Tz hana uwezo wa kuhimili gharama za vita dhidi ya nchi kubwa kama kongo sembuse Rwanda?

Kiufupi Rwanda haina ubavu wa kuivamia Congo.
Kama ni eneo sidhani kuwa ni shida sana, Congo ni miaka sasa amejiimarisha nae kiulinzi, hasa mafunzo ya askar wake, naamini hivyo.

Bado congo ana damu ya kupendwa na jirani zake kama Tz, Kenya n.k hii inampa advantage kubwa ya kupewa msaada ktk mapigano yake.
 
kagame ashazeeka hana mbinu tena za kuitesa congo, watoto wake wale ni masharo tu wamekulia maisha ya kishua hawana mbinu za msituni kama za baba yao, so usitegemee tena rwanda kuibuka mshindi
 
Mlimpa ulinzi na kuwa royal kwa yule dictator na mwizi aliyewaibia, kuwatia umaskini na kuwaua kwa miaka zaidi ya 30, hata kama hampendi Kagame lakini mumshukuru maana ndio aliwaondolea yule dictator, na akili zenu zilivyo fupi badala ya kujenga nchi yenu mkaenda kujiunga na wale wapumbavu wa FDLR na kuanza kuua banyamulenge ambao ni wacongo wenzenu, jengeni nchi yenu na kaeni chini na M23 na factions zote muelewane, kusingizia Kagame matatizo yenu kila siku haiwasaidii na mnajua kabisa Rwanda interest yao ni wale wauaji waliokimbilia Congo mnaowapa hifadhi, ndege za wazungu zinabeba mamilioni ya madini kila siku kutoka Congo lakini wanasiasa wenu wamewadanganya kuimba Kagame na nyie mnakubali, amkeni wapuuzi nyie
Yaaani ukae chini kujadili na jambazi aliekuvamia? Huo ni uxng....
 
Binafsi kwa utashi wangu Rwanda [emoji1206] ni choko sana, anatafuta nini Congo..? Si atulize matako nchini nwake yeye deilee kumsakama Congo ili amwibie madini yake na magogo, aitajirishe Rwanda muda ho Congo hali tete hata hayo makundi ya M23 nina imani ni ya Rwanda [emoji1206] yana leta choko choko ili waendelee kupiga mali za Congo cha msingi hapo ni Congo kujilipua tu kuhakikisha wana wafyekelea mbali hao wasenge wabaki kwao kila mtu awe na maisha yake ili Congo iweze kupiga hatua nayo sio mambo ya kuwa mtumwa wa Ufaransa na mbelgiji bado na Rwanda akutawale khaaa
Rwanda hana huo ubavu wa kumchokoza DRC! bila nguvu za wazungu matajiri! ......kinacho fanyika hapo Paul Kagame anachochewana kutumiwa km mke Malaya tu,

yaani anapewa pesa na siraha kutoka kwa Matajiri na Mabeberu wa Dunia. mfano; La Medis, Standard charter oil! Merovengian Families! nk.... ili asumbue, na kuleta shida kule DRC!

wkt hayo ya vita yakiendelea wao hao Matajiri wa Dunia wana chota Malighafi za DRC Usiku na Mchana, bila kupiga bismilah wala kunawa, wanatumia midege mikubwa, mikubwa mikubwa inatua Goma,

kila iitwapo leo na kushusha siraha wkt huo huo ina kubeba malighafi za bure za DRC!! chini ya ulinzi wa kagame na Museveni!....Viongozi wooote Africa wanajua hilo!...ila ni waoga.

hakuna mwenye ubavu wakulikemea hilo jambo! km yupo ajaribu aone moto!

Hao hao! wabeba madini ndo walimweka Kagame Madarakani, kwa kutumia hela zao ili baadaye Kagame arudishe fadhira za kutoa Mwanya wao MABEBERU wakaibe Madini DRC!

wooote mnajua kagame hakuwa na ubavu/pesa hata ya kugharamia sungusungu!! au uwezo wa kupata madaraka kirahisi hivo! ka nchi kenyewe kale??

Rwanda/ burundi hakuna Malighafi Mama! za kumtajirisha kagame ivo, zaidi ya ndizi chache na kahawa kiduchu!...Rais wa DRC ngoja nikufungue Macho mbaya wako yuko nje ya Africa ! mfuate huko!

Mpigie kelele huyo, huyu ndugu yako wa damu Kagame Msaliti ndugu yako muache asemwe tuuu na AU mpaka achakae kwa kusemwa!!.....Msaliti = Yuda wa DRC, ni paul Kagame na wasaliti hawanaga aibu!

huwa najiuliza sana hivi kagame sijui ataweka wapi mjisura ule??......mie nawashauri tu viongozi wana siasa hawa vibaraka mkiwaua mnawasaidia sanaaa!! waacheni waishi, wajutie ubaya wao! ni adhabu kubwa sana!

Lkn hao wazungu wana kawaida moja watamtumia weee!....aaaa lkn wakimaliza yao au kukuchokaaa heee!!.....utaomba Dunia ipasuke! mifano ya walio tumiwa Africa hii ya weusi

wooote humu mnaijua ni mingi ila kamata hii michache km vile
1.Savimbi, alisumbua sana Angola kwa miaka miingi huyu walimuua wao kwa kutumia MOSAD AL ABELT! mchana kweupee,

2.Mobutu- alimuua Patrick Lumumba kwa mateso sana tena katumiwa tu! Mawee huyu aibu bana kwanza alifukuzwa nyumbani kwa bwana kuba km mbwa tu, wkt akiumwa, alipunguziwa misaada maksudi, akazurumiwa hela waliyo mdanganya aitunzie huko kwao!

3.Samwel Doe!!! hakuna asiye jua alichofanywa huyu jamaa yaani Raisi aliuawa km kibaka kabisaaa,

4. Idd Amini! huyu hata ahkuwahi kufikiria kuwa atawakimbilia wamuelewe! alijikata kivyake
5.Bokasaank!....sisemi sana makanisema mmbeya nia chuki!
 
Kagame ni tatizo ukanda huu wa EA
Siku akifa, Kagame mtaoana amani itakavo kuwa nzuri ! na watakao muua ni hao hao wanao mpa siraha NA PESA ILI WAVUNE KIFO NI ILI kagame ili asije akatoa siri zao!

Na kagame kwa mfano akiwakatalia kuwapa mwanya wa kwenda DRC, wata muua kwa mapinduzi bandia na kumuweka yule wanaye muona anafaaa!

wajeda wa Rwanda walioko DRC wengi walikataa huo ujinga na kujiunga na jeshi la Drc dhidi ya kagame!...So kagame akawawinda mmoja baada ya mwingine akawaua wooote kwa msaada wa MOSAD! CIA!

So LONG AS DRC kuna madini muziki wake ni mkubwa!
 
Back
Top Bottom