Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sasa kama mnatumia jeshi dogo tu kwanini raisi wenu analialia kutaka misaada kutoka katika nchi nyingine kama vile Uganda Burundi nk? Kwanini asitumie jeshi lake mwenyewe ili asiibiwe rasilimali na majeshi yanayotoka nje?Ww jamaa huna unalo lijua wala hauna uwelewa wowote kwenye medani ya kivita ndio maana unachukulia vitu kirahisi tu.
Rwanda kwa sasa anacho kifanya ni anapigana vita na kongo kwa kutumia mawakala ambao ni hao waasi kwa hiyo anatumia gharama ndogo sana, lakini mambo yatabadirika pale itakapo amuwa kuingia kwenye vita kamili kwa kulihusisha na jeshi lake moja kwa moja.
Alafu kingine unacho takiwa kujua ni kwamba ni sehemu ndogo tu ya jeshi la kongo ndo ipo mashariki mwa kongo kupambana na waasi na sio jeshi zima.
Mwaka 2012 Tanzania tulipeleka jeshi letu huko likafanya makubwa hadi M23 wakakubali kukaa mezani na serikali.Nchi zilozo peleka jeshi mashariki mwa Kongo Ni Kenya ,Burundi , South Sudan .kwanin Tanzania na Uganda hawahangaiki na Vita hvyo ?
Nijibu Kisha nikupe abcd za tshekedi
Kwani anaepigana ni Kagame au jeshi la Rwanda. Kagame na Biden nani mkubwa?kagame ashazeeka hana mbinu tena za kuitesa congo, watoto wake wale ni masharo tu wamekulia maisha ya kishua hawana mbinu za msituni kama za baba yao, so usitegemee tena rwanda kuibuka mshindi
Mkuu ndio haya tunayoongea hapa. Sio kwamba serikali na jeshi zima la Congo hakuna mwenye mawazo hayo ya kuwafuata waasi hao Rwanda, ila sasa outcome ya Rwanda baada ya Congo kuvuka mpaka wake itakuwa ya namna gani?Sawa kaka, wachakazeni hao wanyaRwanda na M23, mnakerq sana mnavyomuogopa huyo Kagame, wafuateni hao M23 hata wakikimbilia Rwanda
Wakenya wenyewe wamaeanza kuhoji huu mpango wa kumaliza fedha za walipakodi.😆DRC inasaidiwa na jumuiya ya Afrika Mashariki. Ni mwisho wa Kagame.
Watu wehu wanamtukuza sana sifahamu kwa nini? Possibly hata akajawaomba nanilii watampatia 😂😂😂Kagame mnamtukuza mno.
Wakenya wapumbavu ndio watahoji huu mpango kwa sababu hawajui ya kwamba eneo hilo litakapokuwa huru na DRC wakenya watauza bidhaa nyingi sana DRC, ruto has seen this opportunity he want expand market kwani soko la DRC itakapikuwa huru na ya amani Sisi EA, wote hatutaweza kujazwa bidhaa in free DRC.Wakenya wenyewe wamaeanza kuhoji huu mpango wa kumaliza fedha.😆
![]()
Kenya MPs raise questions over KDF troops deployment to DR Congo
MPs question the sequence of events, saying the deployment should first have been approved by parliament.www.theeastafrican.co.ke
Wamegundua hawatauza kitu chochote na wamegundua huo mgogoro hautaisha bila ya solution.wakenya watauza bidhaa nyingi sana DRC
Nijuavyo hata huko Ukraine wapo wanaodonate chakula, fedha au weapon,kwa Sisi to si lazima tupekeke chochote Sisi tutapeleka maji baridi ya kunywa pekee!Nchi zilozo peleka jeshi mashariki mwa Kongo Ni Kenya ,Burundi , South Sudan .kwanin Tanzania na Uganda hawahangaiki na Vita hvyo ?
Nijibu Kisha nikupe abcd za tshekedi
Kufadhili waasi ni kwa mujibu wa sheria zipi za kimataifa?Majeshi ya Kenya na Uganda hayawezi kuvuka mpaka wa Rwanda kwa sababu hayakwenda kule kupigana na nchi ya Rwanda. Bali kuyakimbiza makundi ya waasi yaliopo Congo.
Ndo maana mwaka 2012 Tanzania na nchi nyingine zilipokwenda kupambana na makundi hayo, M23 na makundi mengine yalipokimbilia Rwanda na Uganda hawakuyafata.
Mkuu kwa uzoefu wako hapa JF sikutegemea kama ungeweza kuandika namna hii. Eti nchi hizo ziingine kwenye ardhi ya nchi nyingine kwa ajili ya kuwafuata waasi, hata sheria za kimataifa haziruhusu hili.
Rwanda kila siku inadai kuwa warundi wanawahifadhi waasi wa Rwanda katika ardhi yao, lkn haikuwahi hata siku 1 kutuma jeshi lake kuingia Burundi kuwasaka waasi hao. Halikadhalika na Burundi nayo inadai kuwa wanyarwanda wanawahifadhi watu waliotaka kupindua serikali yao mwaka 2015 lkn hata siku 1 Burundi haujawai kupelekea jeshi lake Rwanda kuwasaka waasi hao.
Sasa kama nchi husika ambazo zinapeana mpaka zinashindwa kuingiliana iweje nchi inayotoka huko mbali kama vile Kenya nk ziingize jeshi katika ardhi ya nchi nyingine bila ruhusa ya nchi husika?
Nadhani gharama unayomaanisha wewe ni kuikalia (occupation) ila kama ni kuipiga ilishafanya hayo kwa mafanikio mwaka 1996 japo ilishirikiana na waasi wa Zaire na nchi nyingine kama Uganda ,Angola kwa kiasi Eritrea na hata Zimbabwe zilisaidia hayo mafanikio.Hakuna nchi ina makundi ya waasi hadi 10 kama Congo ilivyo, logistics za kuipiga Congo kuanzia mpakani kwa Rwanda mpaka katikati ya nchi kule ni gharama kwa Rwanda. Rwanda kuipiga Congo sio rahisi hata kidogo
usifananishe marekani na rwanda boss, rwanda ni nchi ya mtu mmoja, marekani sio nchi ya mtu mmoja, rwanda ina sumu ya kuuana na kupinduana wahutu na watusi, kila upande hapo unataka kua juu ya mwenzake, na hiyo ndo inachangia pia mgogoro huko congo sababu huko wahutu na watusi wote walikimbilia huko miaka mingi iliyopita sababu ya vita za huko nchini kwao, sumu ambayo bado ipo na haitakaa kuisha labda sijui iweje, ngoja nikuulize swali alafu ujibu, je kuanzia kagame ashike urais rwanda je marekani washapita marais wangapi? je kwanini rwanda awe kagame tu miaka yote? kwa nini akitaka kuinuka mwingine zaidi yake anampoteza? ukipata jibu la hilo swali utapata jibu lako la bidenKwani anaepigana ni Kagame au jeshi la Rwanda. Kagame na Biden nani mkubwa?
Je Kenya yenye raisi kijana inaweza kuitwanga Marekani kwa sababu Biden amezeeka? Mawazo ya wapi haya mkuu!!!
Rwanda yenyewe ishakataa kuwa haiwafadhili. Kwahiyo kama Congo ina ushahidi wa kutosha, hapo kinachotakiwa ni kupeleka kesi katika mahakama ya kimataifa ili mahakama ithibitishe madai hayo kisheria na itoe adhabu kwa mtuhumiwa.Kufadhili waasi ni kwa mujibu wa sheria zipi za kimataifa?
Hata Urusi mbona inapewa support na China na Iran pia.... Au hujasikia drones za Iran ndio zinatumika kudungua?Urusi hapambani na Ukraine anapambana na nato na marekani
Eti DRC inaweza kushinda vita? You're not serious.... Hivi 1st and 2nd Congo war mbona Rwanda alifika mpaka Bas Congo? Tena kwa jeshi dogo vile (usiniambie alipewa support na UG maana hata DRC naye alikua na support ya Zimbabwe, Angola etc)Ukiniuliza mimi kwenye vita kamili isiyo ya kujificha kati ya Rwanda na DRC nani anashinda nasema ni DRC endapo hakuna external influence baina ya pande zote mbili.
Congo ukitaka kuipima kwa kuangalia eneo lake la Mashariki utapotea, itazame nchi nzima hadi kule Magharibi. Mashariki ni kama imepotezewa na ina waasi wengi wanaojificha na kusumbua kila wakijisikia. Wakipigwa wanavaa kiraia wanalima, wakipata support wanaanza mapigano. Ukija kwenye vita ya nchi na nchi hapo hujifichi, madaraja tunajua yalipo, kambi zilipo, airbase ilipo, HQ, defensive lines na mambo mengine.
Congo sio wazembe kuliko nchi nyingi za Kiafrika, tatizo lao wana rasilimali nyingi na bahati mbaya ya kunyonywa na mataifa ya nje, ila nchi nyingi za Afrika hazina unafuu kijeshi kuwazidi. Hakuna nchi ina makundi ya waasi hadi 10 kama Congo ilivyo, logistics za kuipiga Congo kuanzia mpakani kwa Rwanda mpaka katikati ya nchi kule ni gharama kwa Rwanda. Rwanda kuipiga Congo sio rahisi hata kidogo