Katika kile unachoweza kutafsiri kama ni Kenya kuguswa na siasa mpya za Tanzania, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesistiza ustahimilivu wa kisiasa hasa kwa nchi zilizoizunguka. Amesema uchaguzi unafaa kuleta utangamano wa nchi na siyo kinyume chake.
Amedai kuwa siyo siri nchi zinazoizunguka Kenya hazina utulivu mzuri wa kisiasa kama ilivyozoeleka. Amedai kuwa kukosekana kwa utulivu kwa jirani ni hatari kwa Kenya.
Huku akipigiwa makofi na wabunge Rais Kenyatta, amesisitiza kuwa wanasiasa wazee wasiwachokoze wanasiasa vijana badala yake wawalee kwa upendo.
=======
Katika hotuba yake Bungeni, Rais Kenyatta amesema:
Nchi nyingi jirani zetu leo zinahitaji kupeana mikono. Wanahitaji siasa ambazo ushindani haugeuki uadui na vita. Wanahitaji viongozi wa kisiasa waliolenga kujumuisha vijana na waliokata tamaa, bila kuwachochea kuasi dhidi ya nchi zao na wazee wao.
Tumejifunza kama Wakenya kwamba uchaguzi pekee hauwezi kuleta amani na umoja kwa watu waliogawanyika. Kwa hilo, viongozi lazima waafikiane na kuwa madaraja ya kuwavusha watu keuelekea kwenye usalama na ustawi.
------------
Many neighboring countries today need a handshake. They need politics in which competition is not turned into enmity and war. They need political leaders focused on including the young and desperate, not inciting them to revolt against their countries and their elders.
We have learned as Kenyans that elections alone cannot bring peace and unity to a divided people. For that, leaders must reach out to each other and build bridges over turbulent waters to allow the people to cross into safety and prosperity.
Demokrasia Kenya? Ulikwishafika Kenya wewe?
Hivi mtanzania kweli kweli uliyezoea maisha ya Amani, utulivu na ustaarabu wa Tz unaweza ishi Kenya ukazoea kabisa wewe? Wale wanaitwa "Nyang'au". Unajua maana ya Nyang'au Wewe? Acheni masihara. Afadhali maisha ya Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, unaweza kuzoea. Wananchi wastaarabu. Wakarimu. Kenya!? Hovyo kabisa.
Hao akina Uhuru, Odinga, Ruto; unawajua wewe?
Tanzania nenda sehemu yoyote utapata ardhi ya kulima, kufugia, kujenga, biashara na maisha yanaendelea. Nenda Kenya ukaone! Maskini ni maskini kweli mpaka kiama; na tajiri hali Kadhalika. Ulikwishafika Kibera wewe. Wapi ktk miji ya Tanzania kuna slums kama zilizopo Kenya. Acheni bwana. Kenya kuna watu wa hovyo usipime, wengine wako huku Wakikuyu na Wajaruo, wanatusimulia pia. Wapo wengi tu, na kwa siasa nzuri za Tanzania wengi wana hali nzuri ya maisha. Ni matajiri wala hawabughudhiwi. Ukiwaambia warudi Kenya wanasema afadhali uwaue kuliko kurudi kule "motoni". Acheni bwana.
Nenda Kenya uone kama utapata ardhi ya kulima au kufugia. Ardhi yote imehodhiwa na akina Uhuru. Ni "miungu watu" wa Kenya ... The untouchables. Ati loyal families!
Maendeleo ya TZ yanakwenda sawia ktk maeneo yote mijini hadi vijijini. Nenda Kenya Kaskazini ukaone. Aibu!
Acheni kutulinganisha TZ na Nchi ya unyonge kama Kenya bwana. Ni jamaa wana publicity hao usipime! Nawafananisha na waingereza wanaoshinda kombe la dunia magazetini!
Ni suala la muda tu; Kwa mwendo tunaokwenda TZ, Kenya watakuja kutupigia magoti miaka si mingi. Hata hivyo, mbona tunawalisha mahindi na maharage mara nyingi tu. Hawana uwezo wa kujitosheleza kwa chakula.
Tanzania ni Nchi pekee Duniani iliyo na Serikali zinazojitegemea kuanzia ngazi ya kitongoji/mtaa.
Ardhi ni mali ya Serikali. Hakuna ubaguzi wa aina yoyote, hata Wakenya waliopo TZ wanapewa nafasi za uongozi almradi wanafaa, nk. Je, Kenya mambo haya yapo? Tunapendana hatubaguani. TZ imekwishakuwa fashion ya zamani kuoa au kuolewa na kabila lako! Kenya ipo hiyo?
Kenya wakitaka kupiga hatua sasa ya maendeleo wakubali kuja kujifunza Tanzania kwani kwa sasa hatuna la kujifunza kutoka Kenya.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU MBARIKI JPM
MUNGU IBARIKI AFRIKA