Uchumi wa Russia hata haufikii California State, wala Texas, wala New York, yaani ukichukua Russia GDP iko nyuma ya California kwa mbali sana, to make you understand kidogo tu, California alone GDP is twice that of Russia, Dec 2018 GDP.. au Texas au New York zimeipita Russia sana tu kiuchumi..!!
Naona umenishambulia sana mimi binafsi hadi ukapoteza mwelekeo mzima wa huu mjadala. Tafadhali usifanye hivyo tena, maana kama na mimi nikikujibu kwa kukushambulia wewe binafsi tunaweza kujikuta tumepoteza maana nzima ya huu mjadala mzuri. Tujibu hoja hata kama hatupendi kuzisikia. Naomba nikutaarifu kabisa kwamba leo sintatumia RT, BBC, CNN wala FOX News katika kukujibu, bali nitakupa tafiti za kitaalamu ambazo zimefanywa na wanazuoni wakubwa tena wale wa nchi za Magharibi. Hebu sasa tuanze kuchambua hoja zako ulizoziwasilisha hapo juu:
So US is the Super Power if compared to Russia, na hakuna nchi duniani itakuwa na nguvu ya kijeshi kali huku uchumi wake ni dhaifu.. So Russia military is weaker compared to US military due to economy..!! US military budget 2018 was $ 700 bil, while Russia military budget was $ 40 bil.. So just using the common sense, kama ww muelewa utajua kabisa Russia can not ever ever be able to engage in war with US.. Hana military muscles to sustain in the war for months..!! US GDP Dec 2018 $ 22 trillions.. Russian GDP 2018 $ 1.3 trillions
Naomba nikubali kwamba nchi ya Marekani ndiyo nchi kubwa sana duniani na yenye uchumi mkubwa kuliko zote ukitumia kiwango cha GDP. Pia Marekani ndiyo nchi yenye bajeti kubwa ya kijeshi kuliko zote ambapo ukichukua bajeti za nchi zote duniani ukaziunganisha hawawezi kufika kwa Marekani.
Lakini sasa hoja yako uliyoileta hapa inaonyesha huna ufahamu mkubwa sana na mambo ya Uchumi, kama ungekuwa nao basi ungekuwa na mtizamo tofauti kabisa: Upande wa pili wa hoja yako ni kwamba unaangalia upande moja wa shilingi bila kujifunza kupitia historia ya mataifa makubwa yaliyowahi kutokea hapa duniani kabla ya Marekani.
Hoja ya kuwa na Uchumi mkubwa ni kuwa na jeshi kubwa ni nzito sana lakini siyo timilifu (Not decisive). Mara nyingi Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF) huwa zinapima uchumi wa nchi kwa kutumia mbinu kuu mbili: Gross Domestic Product (GDP) au Purchasing Power Parity (PPP).
GDP inaonyesha jinsi gani Uchumi wa nchi ulivyo imara kwa kuangalia kiasi cha bidhaa na huduma ambazo zinazalishwa na kutumiwa ndani ya nchi husika mara nyingi ndani ya kipindi cha mwaka. Upande wa pili PPP inatumika kulinganisha nguvu ya fedha ya nchi mbili katika manunuzi ya bidhaa.
Kwenye GDP marekani hakamatwi lakini kwenye PPP wa kwanza ni Uchina. Katika hili tunakuja na kanuni ya kiuchumi iitwayo The BIG MAC INDEX iliyoandaliwa na jarida la The Economist. Ambapo wanasema unachukua dola ya kimarekani halafu ukaweka nchi ya Marekani na Uchina halafu unapima nguvu ya manunuzi.
Leo hii ukichukua dola 10 halafu dola tano ukawa nazo kule Beijing na dola tano nyingine ukawa nazo kule Washington: Itakuwa hivi, Washington utanunua Beef Burger mbili, wakati Beijing utanunua Beef Burger tatu kwasababu maisha yako chini.
Hii ndiyo PPP na mwaka 2014 IMF iliitangaza Uchina kuwa ndiyo nchi ya kwanza katika PPP hivyo basi GDP ya California kuwa kubwa kuliko Urusi isikudanganye na kusema Urusi ni nchi dhaifu. Hili linatujengea msingi mzuri katika kujibu hoja yako ifuatayo:
Vita vinahitaji uchumi imara kabisa..!!
Ndiyo vita vinahitaji Uchumi imara, lakini Uchumi mzuri ni ule ambao unazalisha kwa bei ya chini bidhaa ambazo wenzake wanazalisha kwa gharama kubwa. Tukija kwenye PPP na GDP sasa: Marekani ana bajeti kubwa kwasababu Uchumi wake ujo juu na gharama za maisha ziko juu sana. Hivyo rasilimali ni gharama, kodi kubwa, wafanyakazi kuwalipa ni gharama sana ndiyo maana unakuta ana bajeti ya Bilioni 700.
Lakini upande wa pili nchi kama Uchina na Urusi wananufaika na PPP, ambapo kama ukimpa Urusi na Marekani bilioni 10, ambapo Marekani atanunua vifaru 300 kutoka viwanda vya nchini kwake basi Urusi kwa bilioni 10 atanunua vifaru 350 vyenye kiwango kilekile nchini kwake. Unajua ni kwanini ?? Gharama za uzalishaji ni ndogo nchini Urusi.
Ndiyo maana Uchina na Urusi wanatengeneza hypersonic missiles ambazo ni Mach 10, unadhani hela wanazitoa wapi ??
Ushahidi wa hili amelisema mtu anaitwa
Dr Peter Navarro kwenye vitabu vyake
Death by China na
The Crouching Tiger. Nadhani utakuwa unamjua vizuri huyu jamaa, yeye ndiye mshauri wa Raisi Donald Trump kwenye mambo ya Biashara na Sera za Viwanda: Kiufupi huyu ndiye mwanzilishi wa trade war baina Trump na Xi. Amekiri kabisa kwamba gharama ndogo za uzalishaji zinawabeba wachina na mataifa mengine.
NB: PPP ndiyo ilimpa Marekani uwezo wa kuwa na nguvu na taifa kubwa ambalo liliweza kuwafanya washinde vita zote za dunia dhidi ya Ujerumani. Kama ulikuwa haufahamu hadi mwaka 1900 Ujerumani ndilo lilikuwa taifa lenye nguvu kubwa ya viwanda kuliko hata Uingereza na Marekani. Marekani alikuwa hashindani na Uingereza kwa lolote lile kuanzia nguvu ya sarafu na GDP, lakini Marekani alikuwa ndiyo taifa lenye PPP kubwa duniani tokea mwaka 1872. Huyu anayesema haya ni
Proffesor Joseph Nye wa Harvard University.
Mfano mzuri: Ulikuwa ukiwapa Marekani na Uingereza kiasi sawa cha pesa, basi Marekani alikuwa ana uwezo wa kufanya nayo kazi nyingi kuliko Uingereza kwasababu ya maisha yake kuwa chini. Kwenye vita za dunia yeye ndiyo alikuwa anawauzia silaha na aliajiri wanajeshi wengi sana. Sasa ukikimbilia kuangalia GDP, Uingereza alikuwa kamwacha Marekani mbali sanaa, lakini kwa PPP Marekani alikuwa kamuacha Uingereza mbali sana.
Hivyo bwana Jay One, Uchumi ni kitu kipana sana na ningezungumzia hapa mambo ya vita kuonesha udhaifu wa hoja yako lakini sina muda kwasasa.......