Rais wa Afghanistan kakimbia nchi!

Rais wa Afghanistan kakimbia nchi!

Kwanini wasiruhusu, kwani uislamu umekataza wasio waislamu kuingia kwenyi nchi zao!!! Usome uislamu upate kuujua mkuu.
Unatetea kitu gani mkuu?

Hivi umeona zile video watu wamerundikana Airport wanataka kukimbia?

Si ni waislamu wale?
 
So shule nia hiyari yako [emoji23][emoji23]
ndiyo maana umeandika mazuli badala ya mazuri!
Mheshimiwa baba askofu Dr. Josephat Gwajima ni msomi wa Phd,.. ebu msikilize akiwa anatamka neno Rais, habari na hilo "vizuri" unalomzodoa nalo mwenzio, halafu uje usome tena comment yako.

'Elimu' ya ujinga ni ile isiyomsaidia mtu hata kujenga hoja tu!
 
Biden alikurupuka kuondoa majeshi sasa imekula kwake. Halafu wamechukua nchi kirahisi sana sehemu nyingi hilo jeshi la Serikali hata kupigana hawakupigana waliishia kukimbia na kwenye makambi mengi hawakuwa na chakula.
Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani, amekimbilia Tajikistan, kwa mujibu wa Al Jazeera!

Taliban wameshinda!

Taliban wamechukua nchi!

Mwezi mmoja uliopita, Rais wa Marekani alisema bila kumung’unya maneno kuwa Taliban kuchukua nchi hakuwezekani kwa sababu jeshi la Afghanistan liko imara.

Hahahaa. Well, tayari Taliban wameshachukua nchi na Rais wa Afghanistan kala kona.

===

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ameikimbia nchi yake leo jioni baada ya wanamgambo wa Taliban kuuzingira mji mkuu wa Kabul.

Maafisa wawili wa serikali ambao hawakutaka majina yao kutajwa wameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Ghani ameondoka Afghanistan na inaarifiwa amekimbilia taifa jirani la Tajikistan.

Mkuu wa Baraza la Maridhiano ya Taifa nchini Afghanistan Abdullah Abdullah pia amethibitisha habari hizo kupitia mkanda wa video.

Kuondoka kwa Ghani kunatoa taswira halisi ya uwezekano wa kundi la Taliban kuchukua madaraka nchini Afghanistan wakati wowote kuanzia sasa.

Wapiganaji wa kundi hilo waliingia kwenye viunga vya pembezoni mwa mji mkuu wa Kabul leo Alfajiri baada ya kupata mafanikio makubwa katika siku za karibuni kwa kuikamata miji mingi nchini humo.
Nakumbuka Trump alishafanya kikao ma hawa Wataliban ma kukubaliana nao mambo kadhaa. Isije ikawa ndiyo walishaamua kuwarudisha madarakani
 
Nimeona kwenye video Wananchi na wageni wakiwa desperate kuondoka Kabul.

Hii fall of Afghanistan kipindi cha Biden ni mbaya sana na itamgarimu kwenye uchaguzi ujao unless kuna jambo kubwa watafanya la kimkakati ku turn situation around.

Ili transition iwe smooth kusiwe na madhara kwa Amerika na dunia hususani kuhusu ugaidi na haki za binadamu kutokana na Taliban kushika tena Mamlaka ya kuongoza Afghanistan
Wewe huna ujualo kuhusu "ugaidi"
 
US ilikuwa haifurahishwi na mwenendo wa watawala huko Afghanistan. Rushwa na uovu mwingine ulikithiri,watawala walijisahau na kuanza kula bata badala ya kuimarisha mifumo ya ulinzi.
Wachunguzi wanasema Marekani ilikuwa na mapatano fulani na Taleban ndio maana imefanikiwa zaidi.

Pia kauli za Wataliban zimekuwa more political kuliko radicals na baadhi ya misimamo yao wamelegeza kama watoto wa kike kwenda shule nk
 
Nimeangalia live watelaban wakiingia Kabul nimegundua mambo kadhaa:kwanza hawa jamaa wananidhamu ya juu mno,sikuona wakipora vitu au mali,hawana wenge la ushindi kushangilia au kuimba au kupiga risasi juu kufurahia ushindi.
Wanahabari wapo na wanachukua habari bila bugdha.
Nimegundua pia US wamebariki kila kilichotokea,US wamemsaliti kiaina Rais wa Afghan na serikali yake ili Taleban wachukue mamlaka.
Nimegundua pia US siku za usoni atakuwa mpole kwa Taleban na wataanza upya mahusiano ya kidiplomasia pamoja na misaada,kwa.kifupi US anabadili mbinu za kupambana na Taleban.
Lengo ni kushika utawala na kuonesha Dunia hivyo sasa hawawezi kufanya huo ujinga ila pia wanatafuta uungwaji mkono kwa wananchi.
 
Taarifa za ndani zinasema 50% ya jeshi la serikali ya afghanistan ilikuwa upande wa taliban, so hilo hata yeye usa alilijua kabisa, ni kama alivoikimbia somalia miaka ya 90
Hao wanaoitwa wanajeshi wa afghan ni wapuuzi wakati wanatumwa front walikuwa wanapeleka silaha huko kwa wataleban wanasingizia kutekwa mara wakimbie nchi ni wapuuzi tuu.

Huenda walikuwa hawaridhishwi na namna walivyokuwa wananyanyaswa na wanajeshi wa US
 
Ila wewe Jamaa Ni mkweli Sana nyeupe husema nyeupe na nyeusi husema nyeusi.
Licha ya kujulikana kuwa wewe Ni "USA baby" lakini hausifii kila kitu Cha USA ambacho huna hakika nacho.
Uko njema poti.
Shukran jazilan!

Ni kweli kabisa kuwa mimi ni pro-USA.

Lakini sishabikii upuuzi hata kidogo.

Kwenye hili Marekani imechemsha.

Wamechukua medali ya dhahabu katika kukimbia.

Na wameonyesha rangi zao halisi: wakishakutumia na kumaliza shida zao, wanakuacha unaning’inia kama hawakujui vile.

Inasikitisha ila ndo ukweli wenyewe huo.
 
We unadhani US wanawapenda sana Waafghanistan mpaka waende kupoteza hela zote hizo bure tu?
Jibu swali .Afghanistan kuna nini ambacho USA alikuwa anachuma? Wabongo mnapendaga kujifanya mnajua mambo kumbe ushuzi mtupu.
 
Back
Top Bottom