Rais wa Afghanistan kakimbia nchi!

Kwanini wasiruhusu, kwani uislamu umekataza wasio waislamu kuingia kwenyi nchi zao!!! Usome uislamu upate kuujua mkuu.
Unatetea kitu gani mkuu?

Hivi umeona zile video watu wamerundikana Airport wanataka kukimbia?

Si ni waislamu wale?
 
So shule nia hiyari yako [emoji23][emoji23]
ndiyo maana umeandika mazuli badala ya mazuri!
Mheshimiwa baba askofu Dr. Josephat Gwajima ni msomi wa Phd,.. ebu msikilize akiwa anatamka neno Rais, habari na hilo "vizuri" unalomzodoa nalo mwenzio, halafu uje usome tena comment yako.

'Elimu' ya ujinga ni ile isiyomsaidia mtu hata kujenga hoja tu!
 
Biden alikurupuka kuondoa majeshi sasa imekula kwake. Halafu wamechukua nchi kirahisi sana sehemu nyingi hilo jeshi la Serikali hata kupigana hawakupigana waliishia kukimbia na kwenye makambi mengi hawakuwa na chakula.
Nakumbuka Trump alishafanya kikao ma hawa Wataliban ma kukubaliana nao mambo kadhaa. Isije ikawa ndiyo walishaamua kuwarudisha madarakani
 
Wewe huna ujualo kuhusu "ugaidi"
 
US ilikuwa haifurahishwi na mwenendo wa watawala huko Afghanistan. Rushwa na uovu mwingine ulikithiri,watawala walijisahau na kuanza kula bata badala ya kuimarisha mifumo ya ulinzi.
Wachunguzi wanasema Marekani ilikuwa na mapatano fulani na Taleban ndio maana imefanikiwa zaidi.

Pia kauli za Wataliban zimekuwa more political kuliko radicals na baadhi ya misimamo yao wamelegeza kama watoto wa kike kwenda shule nk
 
Lengo ni kushika utawala na kuonesha Dunia hivyo sasa hawawezi kufanya huo ujinga ila pia wanatafuta uungwaji mkono kwa wananchi.
 
Sasa hii Vita si ilikuwa ya Bush? Kwa hiyo Biden aelezee nini hapo?
Kimsingi Biden amesema asingependa kumrithisha rais ajaye Vita.
Na kutoa wajeda alianza Trump na Hawa wamemalizia tuu ,labda staili ndio imekuwa tofauti na matarajio.
 
Taarifa za ndani zinasema 50% ya jeshi la serikali ya afghanistan ilikuwa upande wa taliban, so hilo hata yeye usa alilijua kabisa, ni kama alivoikimbia somalia miaka ya 90
Hao wanaoitwa wanajeshi wa afghan ni wapuuzi wakati wanatumwa front walikuwa wanapeleka silaha huko kwa wataleban wanasingizia kutekwa mara wakimbie nchi ni wapuuzi tuu.

Huenda walikuwa hawaridhishwi na namna walivyokuwa wananyanyaswa na wanajeshi wa US
 
Safi sana baada ya hapo waseme na wale wasaliti
Nalog off
 
Ila wewe Jamaa Ni mkweli Sana nyeupe husema nyeupe na nyeusi husema nyeusi.
Licha ya kujulikana kuwa wewe Ni "USA baby" lakini hausifii kila kitu Cha USA ambacho huna hakika nacho.
Uko njema poti.
Shukran jazilan!

Ni kweli kabisa kuwa mimi ni pro-USA.

Lakini sishabikii upuuzi hata kidogo.

Kwenye hili Marekani imechemsha.

Wamechukua medali ya dhahabu katika kukimbia.

Na wameonyesha rangi zao halisi: wakishakutumia na kumaliza shida zao, wanakuacha unaning’inia kama hawakujui vile.

Inasikitisha ila ndo ukweli wenyewe huo.
 
We unadhani US wanawapenda sana Waafghanistan mpaka waende kupoteza hela zote hizo bure tu?
Jibu swali .Afghanistan kuna nini ambacho USA alikuwa anachuma? Wabongo mnapendaga kujifanya mnajua mambo kumbe ushuzi mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…