Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

Gavana wa Bank kuu bwana Benno Ndulu wanajuana na JK kama sikosei walisoma pamoja na alimfuata kule ugaibuni kumwomba aje kuwa Gavana wa Bank baada ya kumfukuza kazi gavana Daudi Balali, sasa kutokana na kujuana huko Gavana anashindwa kumshauri rais hkuhusu madhara ya kukopa bank(kuchapisha noti mpya). Hi ndio madhara ya kufanya kazi kwa kujuwana.
 


Kwani nani anajukumu la kupandisha thamani ya pesa ya tanzania kama raisi mwenywe kaiona haifai hayo maendeleo ya nchi si ndoto za alinaja.
 
Rais alikua anazoza na wazee wa Daslam. Ndio maana alikua anatumia maneno ya vijiweni
 
Na kwa mtindo wa kujuana ndicho chanzo cha Ufisadi ndani ya Serikali! Mfano kujuana kusiko na maslahi kwa JK na Lugemalira kumetufikisha kwenye Ufisadi wa Escrow! Pamoja na yote hayo, Bado hata Mdhibiti Mkuu wa Ikulu (State Controller ) Amepata Mgao wa Ufisadi wa Escrow wa 800 million! na kaachwa akila maisha pale pale Ikulu.
 

Wakati mwingine huwa nakumbuka kauli ya Mwl Nyerere kuhusu Kikwete kama mgombea Urais 1995, kwamba "Kijana, bado", hapa Nyerere hakumaanisha umri, alimaanisha Uwezo wake mdogo!
 
Ukweli bila kuuma maneno, Rais wa nchi kuiita fedha ya nchi yake ya madafu ilihali anajua kauli hiyo maana yake nini ni kitu kinachouma sana. Nadhani wazee wa magogoni walishangaa hata wao wenyewe.

Ni dhihaka isiyo na kipimo kwa kweli. So sad.
Nchi kama za Uarabuni au Ulaya ilitosha kabisa nchi kupata misukosuko kutokana na hilo.
 
Kuna mtu aliita Pesa yake Viji senti mkalalamika sana leo kiongozi was nchi anaiita Pesa yake kua ni ya madafu baadhi yetu mnaona sawa je angeiita mgeni kwa jina hilo? naamini mnge hamaki na kusema katudhallisha tuwe wakweli nampenda na kumheshim raisi wangu lakini katika hili naona kaidhalilisha nchi yangu.raisi ni binadam kama Mimi na wewe lazima tukubali katika hili anapaswa kufikiria mara mbiri.
 
Awamu ijayo walio na nafasi ya kuteua mgombea urais wawe makini kutuletea kiongozi makini, mwadilifu, anaechukia rushwa, mkali kidogo na atakaelinda na kutetea katiba ya wananchi ili tuweze kutoka hapa tulipo sasa kwani tunakaribia 'kupigana'
 
Ukiangalia nchi nyingi ambazo hela yao ni ya ''madafu''jua ni vinchi corrupt ,havikusanyi kodi(mumeona kwa singasinga &Co),vimejaa ufisadi na hizo rushwa ni rushwa kubwa kubwa ,kama sio hivyo basi ni viserikali kandamizi kama Zimbabwe,Uganda,Congo DRC,Ethiopia.
Hebu fikiria hawa majirani zetu tu hapa Kenya hawana madini,hawana gesi wala ardhi nzuri hela yao imetuzidi mara 20.
Huyo huyo anayesema fedha ya madafu ndie kaifanya hela yetu iwe ya madafu.Ndio nchi lazima hela yake iwe ya madafu kama ni nchi ya kuomba omba.
 

Ndugu unaboa wewe sasa kila post unaweka habari zako?

Acha njaa za kitoto huo unabii wako kafanye kwenu bana nabii bongo?
 
jk fanya kazi usisumbuke na hawa watumishi wa ndani wa mzee slaa watanzania tupu nyuma yako tutaunga mkono jitihada zako zote utakazozianzisha katika kuleta maendeleo ya kweli kwa watanzania.
 

we kitunguu utaendelea kukopi na kupesti hadi lini? huoni soo mtu mwenye tumbu kubwa kama wewe kutwa unapest kitu hichohicho tu.
 


Mimi Pia nina muunga mkono Rais Jk Kuita Shilingi taTZ ni Pesa ya Madafu kwa sababu Tanzania hakuna Viongozi wa Serikali wanaojali Maslahi ya Wananchi Viongozi karibu wote ni wabinafsi wanaojali Maslahi yao na Familia yao hawajali walala hoi. mimi pia ninaita Shilingi ya Tz ni Pesa ya Machungwa sio Madafu tu.
 
Last edited by a moderator:
Kauli kama hii kutoka kwa Kiongozi wa nchi mwenye dhamana ya kuongoza nchi katika masuala yote muhimu ya Kiuchumi, kisiasa, kijamii n.k, SIO SAWA hata kidogo! Ni kiwango cha juu kabisa cha Uzembe, Udhaifu na kutojali!
HATUFAI!
 
Last edited by a moderator:
Kauli kama hii kutoka kwa Kiongozi wa nchi mwenye dhamana ya kuongoza nchi katika masuala yote muhimu ya Kiuchumi, kisiasa, kijamii n.k, SIO SAWA hata kidogo! Ni kiwango cha juu kabisa cha Uzembe, Udhaifu na kutojali!
HATUFAI!
Hatufai kivipi wakati tumemchaguwa kuwa kiongozi wetu?Na ana tuongoza Mkuu tajirijasiri hukumpigia kura wewe Rais wetu?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…