Rais wa nchi kuiita pesa ya nchi yake pesa ya madafu, kiongozi kweli huyo?

JK kazaliwa ktk nchi ya mizaha "samahani kwetu nzi ni eneo fulani lenye utamaduni fulani tofauti " ..kwao mizaha ni udugu na bora kuliko lolote.Ndio maana nchi inaenda hivi nae anafanya hivi.Halafu anajichekesha kinaisha.
 

Ila ukae ukijuwa kikwete mwenyewe lugha haipandi..hana uwezo wa kuongea kiingereza kabbisa kabisa anaongea very poor English utadhani form 2 aliyefeli.
Kwa kweli huyu m baba anatia aibu sana.
 

Ndugu yangu kikwete shule hamna na Tanzania hakuna rais ..zaidi tuna picha au li sanamu tuu la rais..
 
Nadhani watanzania tumerogwa kwani mara ya ngap unasikia ela ya tz ikiitwa madaf na watanzania wenzetu? Kwani rahis anaweza akawa ametumia lugha iliyozoeleka simlaum sana maana ujumbe ulifika kirahis
 
Ila ukae ukijuwa kikwete mwenyewe lugha haipandi..hana uwezo wa kuongea kiingereza kabbisa kabisa anaongea very poor English utadhani form 2 aliyefeli.
Kwa kweli huyu m baba anatia aibu sana.

Hmm....mbona anaongea Kiingereza kizuri tu.

Yaani unadiriki kumlinganisha Kiingereza chake na mtu aliyefeli form two?

Wewe utakuwa ni mmoja wa wale wanaodhani kuongea Kiingereza kizuri ndo kuwa na elimu.

Umeshindwa kutambua kuwa unaweza ukaongea Kiingereza fasaha na bado ukafeli form two vile vile.
 
Ila ukae ukijuwa kikwete mwenyewe lugha haipandi..hana uwezo wa kuongea kiingereza kabbisa kabisa anaongea very poor English utadhani form 2 aliyefeli.
Kwa kweli huyu m baba anatia aibu sana.

Kikwete hata Kiswahili tu kujieleza mzigo.
 
Hata kwenye huu ujinga uko na JK, hii ni zaidi ya mahaba niue.
Ulitaka Rais aseme kitu gani zaidi ya hivyo alivyosema? Shilingi ya Ki-Tanzania ni pesa ya Madafu Au Pesa ya Machungwa haina thamani kokote pale duniani. Wewe Fananisha Shilingi ya Ki-Tanzania na Shilingi ya Ki-Kenya ipi Pesa yenye Thamani? Mkuu SoNotorious Amka acha mapenzi ya kupenda kitu kwako hakina thamani ili mradi unakipenda utapenda umasikini eti ukiulizwa mzee wangu pia alikuwa ni masikini changamka kuondo wa umasikini nyumbani kwako .
 
Last edited by a moderator:

Sasa ndio umeongea nini? Pumba tupu
 
Last edited by a moderator:
Nadhani watanzania tumerogwa kwani mara ya ngap unasikia ela ya tz ikiitwa madaf na watanzania wenzetu? Kwani rahis anaweza akawa ametumia lugha iliyozoeleka simlaum sana maana ujumbe ulifika kirahis

Rais ndiye mkuu wa nchi. Nyerere anakwambia "if the fellow sneezes, the world listens".

Ana kila vested interest na wajibu wa kuisema nchi vizuri, maneno yake ni kama dua inayosikilizwa kuanzia WSJ mpaka MSNBC.

Kikwete kasema hela ni ya madafu, wanahistoria wataandika hela ya Tanzania ilikiwa haina thamani mpaka rais kaiita ya mafafu ai sawa na kusema mitaani hela ilikuwa inaitwa ya madafu.
 
Nakumbuka wakati nafuatilia hotuba ya mh.rais wa anachambua viwango vya fedha,alitamka kuwa fedha ya tz ni ya madafu,je usemi huo hauendani kushuka kwa thamani ya fedha yetu,hivi rais anatamka maneno kama haya na anacheka kama mazuri vile,kwakweli sina imani na rais
 

Hivi unaelewa kinachosemwa? Hata kama majina ya utani yapo, jambo ambalo wanalalamika ni kuwa kutumika ndani ya hotuba halikuwa jambo sahihi. Hayo majina uliyotuwekea David Cameron anayatamka wakat anapofanya mambo ya Kitaifa?

Think widely/ broadly!
 
Labda kwa kuweka sawa tu,
Tanzania (Mke) = Masulupwete
JK = Baba
 

Acha kutetea upuuzi mkuu, swala la rais kudharau hela ya nchi anayoiongoza hadharani ni upumbavu wa hali ya juu
 
Last edited by a moderator:
Amani ya bwana iwe nanyi wazalendo, najua hiyo heading hapo juu wengi mmesikia hasa toka kwa mkuu wa kaya,nikiwa ndani ya ukumbi wa Diamondi, hii kauli haikunistua sana ikizingatiwa nilikuwa kibaruani. Sasa nimekaa na kutafakari pale nilipofika kijijini ( kyela vijijini) watu wanahasira na kauli hii, watu wamepandwa jaziba kiasi kwamba hii kauli ingetoka kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa, chama tawala wasingepata huenda hata mtaa

Nachojiuliza, je walioko Kyela vijijini ndo wazalendo zaidi na Taifa lao kuliko walioko Dar es salaam? na kauli ya hela ya madafu ni kero kwa watu wa kyela tu? kwa nini? 306 Billion ni hela ya madafu lakini Huku kwetu watu / bibi zetu na wazee wetu hawajui hata watasherekeaje kesho maana hata hela ya kibama hawana.

HERI YA X MASS NA MWAKA MPYA KWENU NYOTE.
 
Yaaani iyo kauli ya kukera sana hasa kwa mkuu wa kaya kutamka namna iyo billion hizo kuwa pesa za madafu hii ni dharau kwa thamani yapesa yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…