TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
OMG 😭😭😭😭😭😭😭 Why? Kwaheri Baba JPM Daima tutakukumbuka umetuacha jangwani
 
Watu walisema sana kuhusu hali ya Rais wetu Magufuli, hatimaye Leo yametokea haya!!!Duh wapendwa ni mengi kayafanya na bado alikua akiendelea kufanya ili kutetea nchi yake ikiwemo kwa watoto, vijana wanawake kwa wanaume,walemavu na wazee na miundombinu.

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa
Jina la Bwana libarikiwe

Pumzika kwa Amani Rais wetu JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI
Rest in peace (RIP) OUR PRESIDENT JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI
 
kwa hakika mungu amjaalie pepo.Alikuwa ni mtu mwenye msimamo na alikuwa hamuogopi mtu yeyote mkubwa wala nchi yeyote kubwa.
Alikuwa na sifa zote za kiuongoz na alikuwa na mapunguf yake kma binadam.
INNALILLAH WAINAILLAH RAJIUN
 
Pole nyingi kwa Watanzania wote kwa kuondokewa na Rais wetu
 
Anyways, anaejua sheria inasemaje tujuzane, mama Samia ataongoza nchi mpaa 2025 au utaitishwa uchaguzi mpya?
Katiba iko wazi kabisa, Mama Samia anaongoza mpaka miaka hii minne iliyobaki iishe. Watatkiwa kuchagua mtu mmoja kutoka kwenye chama chake awe Makamu wa Rais. Na yeye ataapishwa kuwa Rais! Namwomba amchague January Makamba (sijui Wakristo watapiga kelele) awe Makamu wa Rais! Hakika kufa kufaana!
 
RIP.
Viongozi mliobaki,jifunzeni kuheshimu watu.
 
Katiba inasemaje? Najua makamu atakuwa Rais kwa miezi mitatu then uchaguzi, vipi kuhusu wabunge?
 
Kifo ni nini! naona mnakoment tu, kifo kinatisha jamani tumwombe MUNGU atupe amani na tuienzi kuongoza watu million sio kazi ndogo, Mwenyezi MUNGU akupeni wepesi tunaingia katika wakati mgumu watanzania, pumzikeni kwa amani marais wetu mliotuachia taifa nakutangulia katika umauti, mama janeth MUNGU akupe faraja wewe na watanzania wote
 
Haina haja ya kuwasingizia mabeberu,Muda na siku yake ilifika.Dunia tunapita tu hatuna hata makazi ya kudumu hapa.Tusikae kwa kujisahau.
 
Kalazwa tangu tarehe 6 March lakini hii Serikali iliyojaa waongo ikaendelea kutudanganya Watanzania kwamba yuko busy anapitia mafaili. Na si ajabu alifariki siku chache zilizopita WAKATUFICHA.
Hata misiba yetu tu ya kawaida( kwenye familia uwa ikishatokea pale hospital mostly uwa tunastuck kwa masaa kadhaa kutafuta namna ya kuwapa taarifa waliopo nyumbani.
 
Nchi ndio kwanza inarudi kwenye mstari mnyoofu.
Sio kweli, kiasi alipoingia madarakani unyonyaji ulipungua, niulize mimi tulichofanyiwa kwenye viwanja vyetu, tumenyanyaswa na matajiri tukanyang'anywa ardhi na vigogo kisa kutoa rushwa,
 
Tunaelewa kafanya mambo makubwa sana hapa nchini.
Kumbuka hakuna asiye na ubaya na uzuri wake kwa sababu hakuna malaika duniani.

Wadhani ni nini hatima ya Tanzania????
Subiri tuzike kwanza
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…