TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Mwenyezi Mungu mmiliki wa nafsi zote,kwake sote tutarudi.
Mheshimiwa Rais Magufuli,pumzika kwa amani baba.
 
Pumzika kwa amani Rais John Joseph Magufuli.

Uliipenda nchi ya Tanzania kwa dhati nasi watanzania wazalendo tutaendelea kukumbuka daima kwa dhati, tukienzi yote mema uliyoyafanya na kutufundisha kwa manufaa ya nchi yetu na vizazi vyetu sasa na hata badae.

Uliweza kuipigania nchi yetu na rasilimali zake katika wakati mgumu sana, wakati ambapo mifumo ya kidunia iliyo ya kishetani ikiwa imekomaa, ila haukuogopa kwa maslahi ya nchi yetu.

Tunashukuru umetuachia watanzania roho na tabia za kijasiri kuweza kupigania nchi yetu na rasilimali zake bila kuogopa,

Umeweza kupanda mbegu ya kijasiri na uthubutu kwa watanzania watoto na watu wazima, mbegu hiyo tutaendelea kuitunza ili iweze kukua vizazi kwa vizazi kwa manufaaa ya Taifa letu zuri sasa na hata badae.

Amani ya Bwana iwe nawe.
Amen
 
ahsante magufuli kwa utumishi wako JMT
nenda shujaa!!!
R.I.P.
 
Hakika nimelia. Machozi yamenitoka. Nahisi bado moyo unalia. Sikutegemea siku hii itaisha hivi. Apumzike kwa amani JPM. Hakika taifa litakukumbuka. Ulikua na vision uliyoisimamia kwa msimamo thabit. Ni ngumu kuamini!
Pole mkuu. Sisi wengine machozi yetu yapo mbali sana na hasa kutokana na namna tulivyoumizwa na matendo ya utawala wake. Hakika sina hata tone la huzuni. Naogopa kuandika kilichopo moyoni mwangu nafikiri unaweza fikiria..
 
Katika watu nitakaowadharau katika maisha yangu yote, ni Majaliwa. Mtu anaumwa, yuko taabani, bila hata aibu unatoka unasema eti hajambo, anachapa kazi.

Katika hali ya kawaida, itokee ndugu yako au jirani yako anaumwa hoi bin taabani, halafu jitu litokee liseme kuwa huyo jirani yenu ni mzima wa afya kabisa, mtu wa namna hiyo mtamwelewaje?

Majaliwa hastahili kupewa nafasi yoypte kubwa. Kwa kuwa ni mwongo, aliliongopea Taifa.
 
Chuki itaondoka katika taifa letu, siasa za kishenzi mwisho wake, serikali kupika data na kuongea uongo wa wazi sasa mwisho. Na huu ni udhibitisho kuwa huku mitandaoni tunaongea mambo ya kweli. Mliokuwa mnamshabikia mtu muovu mjipange kuleta muovu mwingine tupaze laana zetu.
Mambo mengi yatabaki vile vile ndugu. Msiempenda kaondoka lakini ugumu/urahisi wa maisha yako upo mikononi mwako.
Kura mtaendelea kuibiwa maana CCM ni ile ile. Aliyekimbilia ughaibuni ataendelea kusota kwenye bench akiusubiri urais.

Dah maisha haya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom