TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Inauma mno kupoteza Rais akiwa madarakani. Rais Alie kuwa na uthubutu katika kuleta maendeleo.

Hata hivyo, hayati JPM hakua na utu hata chembe.

Kwa miaka saba hakuna ajira, hakuna kuongeza mishahara Wala Uhuru wa kujieleza.

Haya ni Mambo ambayo mhe Samia lazima Aya address mapema.

Nenda baba JPM.
TUPO NYUMA YAKO
 
Rest in Peace Mr President. Umeacha alama katika mda uliojaliwa. You'll always be remembered.
 
Inauma, inauma, inauma, inauma na inauma Sana! Ee Mungu utufariji na kutusimamia watanzania kwenye kipindi hiki kigumu cha misiba. Poleni watanzania wenzangu.

Pole Sana Mama Samia Suluhu Hassan. Usiogope, Watanzania tunakuamini, tunakupenda na tuna Imani na wewe. Nchi yetu bado iko kwenye mikono salama chini Yako.
 
Serikali inaundwa upya.
 
Maskini Tanzania
 
Kifo ni fumbo. Mungu pekee ndiye mteguaji wa hili fumbo. Lowasa 2015 walisema hauwezi urais maana ni mgonjwa àtaenda fia ikulu. Je binadamu alifanikiwa hapa? Lowasa yungalipo. Lissu je! Risasi zote zile na bado anadunda. Lakini kejeli alizopokea utadhani si binadam. Naskia baada ya kupigwa risasi kuna watu walisoma "albadir". Naskiaga huwa wahusika wote waliotenda huo ubaya lazma wafe. Sijui ni kweli.........

Tuwatendee binadam wenzetu wema maana hatujui saa wala wakati wetu.
 
Amekwenda, na hii ni njia yetu wote, lakini template ya makusanyo ya serikali aliyoiacha, na misingi aliyoisimamia ameacha legacy kubwa sana, na kama wanatawala hawatakuwa mafisadi, hakika hii nchi itasonga mbele, pumzika baba, mwendo umeumaliza.
 

Nasema hivi chuki itaondoka tu, hao wa kuiba wana kazi ngumu, maana hata yeye aliiongoza wizi wa kura kwani alikuwa na roho ya wizi, si kila mmoja ana roho chafu hivyo. Maombi yetu yamejibu fullstop.
 
"...Nataka niwaambie ndugu zangu, siku moja mtanikumbuka, na mimi ninajua mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya, kwa sababu nimetoa sadaka maisha yangu kwa ajili ya Watazania maskini, kwa hiyo tusimame pamoja, tusibaguane kwa vyama, tusibaguane kwa ajili ya dini zetu, tusibaguane hata kwa makabila yetu. Sisi tuijenge Tanzania..." John Pombe Magufuli.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…