TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Njia nzuri ya kumuenzi Hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli ni kuyaenzi mazuri aliyotuachia [emoji1751][emoji1751][emoji1751]
 
Tutajuta kwanini ameondoka... Mungu amrehemu mpendwa wetu.... daima nitakukumbuka Rais JPM. Umefanya mengi kwenye nchi yetu bila woga...

Bwana ametoa, Bwana ametwaa.
Jina la Bwana lihimidiwe
Nyerere alipoondoka ikulu kulikuwa na wasiwasi kweli lkn maisha yalisonga na alipofariki yalisonga vilevile, tutazoea tu.
 
Nimeumia sana kwakweli.
Katika vitu napenda ni msimamo ntaumiss sana msimamo wake. Historia imeandikwa sasa

Amepigana vita vilivyo vigumu, Mwendo ameumaliza,Imani ameilinda.

Apumzike kwa amani Rais wetu John Pombe Joseph Maghufuli.

Hakika tutakukumbuka sana.
 
Tumezidi kuwa imara zaidi kama nchi na mshikamano kama chama kila nafsi itaonja mauti!
 
"Maisha ni Hadithi tu. Maisha ya mwanadamu ni hadithi tu hapa duniani, basi ewe ndugu yangu kuwa hadithi nzuri kwa hao watakaosimuliwa" Rais Mstaafu Alhassan Mwinyi.

Hakuna asiyeitamani kuisikiliza hadithi nzuri ya Jamedari aliyelala kwa sasa Rais Dr John Pombe Magufuli, kama yupo basi huyo ana chuki zake binafsi za kisiasa tu na wivu wake ambao kila mwanadamu huumbwa nao, hadithi ya kiongozi jasiri shupavu mwenye maamuzi, hadithi ya kiongozi aliekabidhiwa keki ya Taifa na kuamua kuitumia vizuri keki hiyo. Katika ile keki ya taifa ambayo ipo mezani na kila kiongozi aliyepewa keki hii hupewa kisu mkononi kisha kuachwa kuamua afanye nini na keki hiyo, keki hiyo hukaa miaka 5 mezani kwake kwa kila kiongozi wa nchi aliyepewa kwa miaka 5 huwa na maamuzi ya kuamua aitumie vipi.

Kwangu mimi kwa moyo wa dhati kabisa Rais Magufuli aliamua kuikata keki ile vipande vidogo na kila mtu apate na afurahie unga ule wa ngano uliolimwa ndani ya taifa lake mwenyewe, aone utamu wa keki hiyo japo sio wote walioona keki hiyo ni tamu kwani keki hiyo ni moja ladha ni moja lakini ndimi ni mbalimbali zinazohisi ladha ya keki hiyo. Kisha ule mvinyo usio na kilevi wa zabibu kutoka Dodoma akauweka kwenye glasi nyingi kila mtu anywe na afurahie utamu wa mvinyo uliotoka katika shamba la taifa lenye zabibu tamu na bora.

Kupitia JPM maisha yaliingia katika usawa na uzalendo wa kuwafanya wengi wajisifu nikiwemo na mimi kuwa ni mtanzania halisi na naipenda nchi yangu kwasababu JPM alisimama mbele ya mabeberu na wasiotakia mema nchi hii na kutaka waiache nchi katika mikono ya wenye nchi wafanye maamuzi zaidi na kutoamuliwa jambo, sababu Mbuzi wa bwana heri akila shamba la bwana heri yote huwa ni heri tu bwana heri ndio hubaki na maamuzi na mbuzi wake.

Nenda ukapumzike sasa Rais wetu mbio zako umezimaliza japo bado tulitamani sana kuona ukiendelea kukimbia ila ndio umeshavuka mstari wa kumaliza mbio na kijiti umekikabidhi tayari.. hatuna budi kusimama na kupiga makofi huku machozi, kwikwi na vigugumizi vikiwa vimetawala zaidi sababu hatutaziona tena mbio zako za wazi bali tutabaki na kumbukumbu za mbio zako na uhodari wako wa kuvikata vilima vigumu wakati wa kukimbia.

Ulionekana kabisa usoni kuwa umechoka na miguu inauma lakini kwako wewe kuipatia nchi medali ya dhahabu kwenye mbio hizo ni bora zaidi kuliko uchovu na maumivu yako. Mbio zako ziliwachanganya wapinzani na kuwachosha na kukata tamaa ya kushindana na wewe na wengine waliamua tu kuungana na wewe kukamilisha ile kauli ya Senator James E. Watson wa Marekani "kama huwezi kupigana nao basi ungana nao"

Yapo mengi sana ya kusema na nikisema niendelee kusema sitayamaliza ngoja nikae kimya wenye kupenda kusema kama mimi wataendelea nilipoishia

PUMZIKA KWA AMANI RAIS Dr. JPM..JEMEDARIView attachment 1728535

 
Habari hiyo ni ya huzuni kabisa, hata kifo cha Mhe. Magufuli kinatuhuzunisha sana wanafunzi Wachina wanaojifunza Kiswahili. Sina la kusema ila pole🙏 Mungu ibariki Tanzania.
 
Huo ni unafiki,hakuna utu wala huruma kwa muuaji. Nadhani ungekuwa Mzazi wa Ben Saanane na Azory sijui kama ungeongea huu upuuzi the so called Utu. Jiwe alikuwa ni shetani.
Pole sana,..... Akili za kushikiwa hizi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…