Pole kwetu sote. Anayepaswa kuabudiwa na kuogopwa na kusujudiwa ni Mungu peke yake. Pia viongozi wetu wajifunze kuwa wakweli. Huyu mtangazaji na Kassim wametukosea sana watanzania. Tulishindwa hata kumwombea kwa sababu ya uongo wao kwamba huyu ndugu yetu yupo kazini. Hivi walikuwa na maana gani? Uongozi wa nchi haupo hivyo. Tungeweza kumweka hata katika maombi japo mwamuzi wa mwisho ni Mungu. Binafsi nafikiri walijua kabisa huyu ndugu anaonekanaje mbele ya jamii ya ndani na nje ya nchi wakakosa ujasiri wa kuliweka wazi kama ilivyokuwa imewekwa wazi kwa Nyerere, Kikwete na Mkapa.
Hatupaswi kufurahi kufa kwa mtu lakini tuomboleze huku tukitafakari somo tulilolipata kutokana na maisha ya uongozi wa huyu ndugu. Nadharia ya Utu iwekwe mbele zaidi ya vitu. Human Relations Approach ilikuja kwa sababu ya ubabe wa Scientific Approach.
Siyo vema kiongozi kuwa Simba katikati ya anaowaongoza.
Namwomba mama yetu Mpendwa Samia Suluhu Hassan afungue ukurasa mpya. Na kwa kuanza Awaombe wote waliokimbia nchi warudi na wahakikishiwe usalama, ili kwa pamoja tuijenge nchi yetu. Nchi irudi katika mstari wake ule wa utu, kujaliana, kupendana, na kuheshimiana bila kujali itikadi za kidini, kisiasa n.k. Turudi kwenye Utanzania wetu ule wa kumpenda mwenzako kama nafsi yako. Tusishuhudie tena watu wakiwa kwenye viroba, wakipotezwa, wakitekwa na kupigwa Risasi. Nakumbuka kuna watu walizuiwa hata kwenda kutoa heshima za mwisho kwa Mzee Mkapa, kisa tu tofauti za Kisiasa. Jamani! Tunawakemea hadi wapakwa mafuta wa Bwana!
Ee mwenyezi Mungu utusaidie tusamehe na kusahau na kisha kusonga mbele. Mungu anaipenda sana nchi yetu. Alimtumia Nyerere kuifanya Tanzania kuwa mfano kwa mataifa mengine kwa kujali utu wa mtu. Tulizisaidia nchi nyingi ziwe huru!
Mojawapo ya somo tulilolipata ni umuhimu wa kumwangalia mara mbilimbili na kumchunguza kwa kina mtu anataka kuwa Kiongozi Mkuu wa nchi yetu. Tusirudie makosa na kusababisha hadi watu kumwombea mabaya Kiongozi huyo. Tuache mifumo ifanye kazi, mojawapo ya mifumo hiyo ni mfumo wa siasa za ushindani na siyo ubabe. Eti, ukimtangaza mpinzani kashindwa unafutwa kazi! Kweli! Eti kutangaza hadharani kwamba Zitto au Mbowe auawe inakuwa tiketi ya kupata cheo!