Poleni Watanzania kwa msiba huu mzito.
Hakika wengi wetu tumesikitika sana na kifo hiki cha Rais wetu.
Mungu ampumzishe mahala pema peponi.
Kwa tunaosoma lugha ya picha ya mtu, tulimuona Mama Samia akiwa katika huzuni kuu, yawezekana anaona ni mzigo mkubwa sasa anao katika mabega yake, ni kweli tunatakiwa tumuombee Rais pumziko la milele lakini vilevile kama watanzania wazalendo tusimsahau Mama yetu Mama Samia.
Ana kazi kubwa sana ya kwanza kuleta umoja ambao ulianza kufifia kwa kasi kubwa, ana kazi kubwa sana ya kurudisha ile imani kubwa ya wananchi kwa serikali yao. Ana kazi kubwa sana kwa kushirikiana na viongozi wa madhehebu mbalimbali kurudisha UPENDO miongoni mwa Watanzania kwa watanzania na serikali yao. Tunaomba kila mtu kwa nafasi yake amuombee Mama Yetu Mama Samia kwa kazi kubwa aliyonayo mbele yake.
Tumpe moyo, na ajue tupo nae bega kwa bega kwa kazi kubwa aliyonayo kuanzia hivi sasa. Hili ndilo la muhimu, itakua kazi bure kuanza kuwalaumu WANASIASA ambao walitudanganya afya ya Rais wetu, pengine wangesema ukweli tungefunga na kuomba kwa ajili yake, lakini yote tunasema asante Mungu. Pia ambaye ulikua ukiombea mabaya, jiulize sasa je una AMANI YA MOYO? Ushauri kwako/kwenu omba TOBA kwa Mola wako kwa dhati, samehe na kusahau. There is no good in celebrating one's death.
Hitimisho, tunashukuru Mungu bado anaendelea kuwaweka wazee wetu ambao taifa bado linawahitaji haswa wakati huu mgumu, wazee wetu Mzee Kikwete na Mzee Mwinyi, Mzee Warioba, na wazee wetu wengine ambao kimsingi bado tunawahitaji sana. Nadhani wakati huu ndio tunatakiwa tushikamane sana watanzania. Sina mengi. Mungu atusaidie.