Kuna watu kwa kutomuelewa mheshimiwa rais wetu mpendwa, hayati JPM, wameendelea kumpaka matope hata ktk umauti wake!
Naomba niwasihi na kuwaonya, mtuache tumzike mpendwa wetu kwa aman! Bado hatujakubaliana na ukweli mchungu huu wa kifo ambacho pia hatujui kama kimetokea kiasili au kuna mkono wa mtu!
Tafadhari sana, naomba tupeane nafasi ya kumuomboleza kipenzi cha waafrica wote! Mungu tunakushukuru kwa kutupa JPM kutuongoza, tunakuomba uzidi kuiongoza na kuilinda nchi yetu Tanzania, na utupe rais mwingine ambaye ataiongoza kwa kulinda rasilimali zetu kwa wivu mkubwa zaidi hata ya JPM! Amen!