TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

TANZIA Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli afariki Dunia kwa ugonjwa wa Moyo hospitali ya Mzena jijini Dar

Status
Not open for further replies.
Lakini mbona Lowassa naye hajaonekana hadharani kwa muda mrefu sasa au ni mimi tu ndo sijamuona?
Ni kweli, lakini hatukuulizia hali yake sababu hakuwa na cheo chochote.Rais anagusa maisha ya WATZ wote.
 
Tunamlilia kwa sababu,pamoja na mabaya yake,lakini alikuwa na mema pia aliyotufanyia watanzania. Kwa mara ya kwanza Taifa la Tanzania tunapitia kwenye kipindi cha kufiwa na Rais akiwa madarakani, tuombe MUNGU Atuvushe.
 
Kuna watu kwa kutomuelewa mheshimiwa rais wetu mpendwa, hayati JPM, wameendelea kumpaka matope hata ktk umauti wake!

Naomba niwasihi na kuwaonya, mtuache tumzike mpendwa wetu kwa aman! Bado hatujakubaliana na ukweli mchungu huu wa kifo ambacho pia hatujui kama kimetokea kiasili au kuna mkono wa mtu!

Tafadhari sana, naomba tupeane nafasi ya kumuomboleza kipenzi cha waafrica wote! Mungu tunakushukuru kwa kutupa JPM kutuongoza, tunakuomba uzidi kuiongoza na kuilinda nchi yetu Tanzania, na utupe rais mwingine ambaye ataiongoza kwa kulinda rasilimali zetu kwa wivu mkubwa zaidi hata ya JPM! Amen!
 
Tunajua jamaa alikuwa anapiga yeye na team yake, ila wengine walikuwa wanakipata cha moto wakidokoa....
JPM RIP alikosea sana kwenda kinyume na kanuni.

Ukisema sisafiri unakuwa husafiri.

Ukisema hutaki kuoanana na watu ulowazuia access unashika hapohapo na wakataa hata mikono yao.

Hii dunia ina mengi mabaya kuliko mazuri kwenye vita ya kiuchumi.
 
Private hiyo mkuu! Sijui km alikua nawashauri wazuri wa afya rais lazima afanjiwe annually check up nje au ndani! Angeenda hata south basi dah!
Kweli kabisa. Ukiwa Mkuu wa ngazi hiyo private is very minimal. Mimi ni mtumishi ujue. Najua wajibu wa wasaidizi wa Rais. Katika nchi zingine hawa wanastahili kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa uzembe huo Mkubwa. Huwezi kusema ajiamulie yeye kila kitu ambacho kingine ni hasara na hatari kwa Taifa.

Halafu nikwambie, Mfumo (system) ilichofanya ni kuwapenyezea Chadema taarifa za kilichopo na ndio maana walisema wazi kwamba wanataka serikali iseme nini kinaendelea kwa huyu ndugu. Pressure ilipozidi ndio wameona watangaze tu hakuna namna. Ndio uzuri wa kuwa na upinzani. Kuna mambo mengine system haiwezi lakini inakuwa na jukwaa la kusemea kupitia upinzani. Taifa likiua upinzani hakuna maendeleo.
 
Samia futilia mbali Uchaguzi wa serikali za Mitaa ili kuirudisha nchi kwenye mstari. Futa ubunge wa Covid-19 kupitia Chadema. Ondoa wakurugenzi , Ma-RAS, Ma-DAS wote ambao ni makada wa chama. Vyeo hivyo washike wataalamu ambao ni watumishi wa umma.
Kwani yeye Samia sio CCM?
 
Mliosema mh rais magufuli yupo anapiga kazi. Dhambi hii mtaibeba na aibu haitaondoka kwenye nyuso zenu.Mmewakosea sana watanzania waombaji. Mngesema ukweli mzee anaumwa waombaji wangemuombea sana tena kwa mchozi mengi.

Nani ajuaye labda Mungu angefanya rehema kama kwa mfalme ezikia alieambiwa na nabii isaya utakufa na baada ya maombi Mungu akamrehemu na kumuongezea miaka 15. Rip mh rais magufuli. Umeacha alama nyuma yako. Ipo reli kila atakayepanda treni utakumbukwa.Lipo bwawa la umeme. Nenda ila umeacha ambayo yatanenwa daima.
 
Mzena ni Private?

Si ya makumbusho hiyo? Something like that! Kwy qns why atoke JMKHI aende mzena sijawai hata kuwaza? Why not flying him to SA au hata Kenya apo baada ya kupata nafuu kwa uangalizi zaidi! Anyway yote tumuachie Mungu
 
Kuna watu kwa kutomuelewa mheshimiwa rais wetu mpendwa, hayati JPM, wameendelea kumpaka matope hata ktk umauti wake!...
Na watanzania tujifunze kuwa ukiwa kiongozi wa aina ya JPM RIP watakiwa kuwa umetengeneza JPM wengine kama watano hivi.

Ili hata siku watangulia mbele ya haki, basi JPM wengine wanashika hatamu.

Hakuna vita mbaya kama ya uchumi na kulinda rasilimali zako.

JPM alikataa katakata access kwa jamaa na wakachukia na muda si mrefu utawasikia wakitoa matamko kadha wa kadha.

Nawalaumu sana baadhi ya watanzania wenzetu ambao wamevua uafrika wetu na kujitwika haiba za kigeni na kusahau kuwa wao ni waafrika.
 
Ndugu zangu watanzania mabibi na mabwana awali ya yote hatuna budi kumshukuru mwenyezi mungu kwa pumzi anayotupatia .Kipekee napenda kutoa pole kwa watanzania wote kwa msiba uliotukuta kwani ni wetu sote.

Ningependa kuwasii ndugu zangu watanzania na viongozi wa umma kwa ujumla kuwa mungu hufanya jambo kwa kusudi maalumu na ni vyema kuichukulia changamoto hii kama ni funzo kwetu kwa kufanya yaliyo mema siku zote za uhai wetu kwan hatuijui kesho yetu n pia ni vyema kwa viongozi wa nchi kujenga mahusiano mazur baina yao na watu wanaowaongoz a kwan wanahifaji sana support yao kama viingozi kwa kuwajali na kuwapa maslai yao kama wananchi wao.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU BARIKI SERIKALI YETU
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom