Ndugu zangu,
Kifo ni nia yetu sote na Mauti ni yetu sote.Jemadari ameanguka lieni na kuomboleza.
Kati yetu tupo ambao hatukupendezwa na Mengi ya Zama na nyakati za Magufuli na Pia tupo ambao tulipendezwa.Wapo ambao hawakunufaika na wapo pia ambao walinufaika.Kama ilivyokuwa katika zama za Nyerere,Mwinyi,Mkapa na hata Kikwete kuna wa kupata na wa kupoteza.Hata hivyo lazima tuambieni ukweli hakuna ambaye Msiba huu haumgusi.Namkumbuka Mfalme Daudi alipopewa habari za kifo cha SAULI pamoja na kwamba SAULI alikuwa adui yako,Daudi aliomboleza KIFO chake.Narudia tena DAUDI aliomboleza kifo chake pamoja na kwamba SAULI alitaka kumuua DAUDI.
Mimi sio muumini wa historia ya Wayahudi bali nimeweka kumbukumbu hii hapa ili tujua kwamba Pamoja na tofauti zetu,MAGUFULI ni JEMADARI WETU TUMLILIE
Tumlilie kwa sababu alikuwa na maono na taifa letu ambayo alihitaji kuyakamilisha na ameondoka na kutuachia wenyewe tuamue kama tutayakamilisha ama tutayaacha.Tumlilie kwa sababu alifanya mambo mengi mema na mabaya ktika kuhakikisha kuwa nchi yetu inaenda mbili.Tumlilie kwa sababu tulimpa jukumu zito la kusimamia uendeshaji wa nchi yetu pamoja na udogo wako.MAGUFULI NI JEMADARI WETU TUMLILIE
TUMLILIE kwa sababu hatujui atakayekuja baada yake atakuwaje,tutambue kwamba tulilalamika mbele ya Mungu na kunungunika tukidai Mfalme kama ambavyo wayahudi katika historia yao walipodai mfalme na wakapewa.Mfalme akaja na maumivu yake na Magufuli alikuja kwetu na Maumivu yake.TUMLILIE MAGUFULI NI JEMADARI WETU.
Tuskubali kudanganywa kwamba yeye alikuwa mwovu kuliko sisi.Kama tulishindwa kusimama katika wakti wa dhiki na kusimamia kile ambacho tuliamini ni haki basi sisi ni waovu kuliko yeye.Kuwepo kwetu hai hakumaanishi kwamba sisi ni wema zadi na wala kufa kwake hakumaanishi yeye ni Mwovu.Tumlilie Jemadari wetu Ameanguka.
Tusisubiri kumlilia wakati tutakapotambua kwamba ni heri mti mbichi kuliko mti mkavu.Tumlilie kwa uchungu kwa maombelezo.Yeye ni jemadari wetu,kiongozi wetu.Yeye alikuwa mkuu kati yetu na mdogo kati yetu.Tumlilie Jemadari wetu MAGUFULI
Nenda Magufuli Nenda. Kaungane na Nyerere na Mkapa katika kulienzi taifa letu.Kaungane na Wazalendo wengine waliotangulia katika kuliombea taifa letu.Kasimame pamoja na mashujaa walinzi wa taifa hilii.Nenda Shujaa,nenda shahidi,Nenda Jemadari.