Ukristo una madhehebu mengi tofauti tofauti na ni vigumu kwa sasa kutambua imani sahihi ya Kikristo. Vyovyote ulivyo, katika muktadha wa sasa, hakuna aliye karibu zaidi na mafundisho asilia ya mitume.
Mungu pekee ndiye ajuaye ni lini Wakristo wataweza kutoa nakala sahihi (asilia) ya kitabu chao (Biblia).
Mtu atashangaa, juu ya idadi ya matoleo ya Biblia yaliyopo leo hii. Kila moja linatofautiana na jingine, ndio, kila moja linadai kuwa yeye ndio toleo asilia.
Matoleo yote hayo yameshawahi kutangaza duniani kuwa, yenyewe ni ufunuo mtakatifu.
Rejeo lao lililo tayari lipo katika (2 Timotheo 3:16), isemayo “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho...”
Lakini kile wasichokifahamu Wakristo ni kuwa, “Kwa hakika, yaliyomo katika Biblia zao si Maandiko matakatifu isipokuwa ni hekaya, fikra, matukio na tamaduni tu.”
Tatizo hilo linachanganya zaidi pale tunapojua kuwa baadhi ya matoleo ya Biblia yana vitabu vingi zaidi kuliko mengine.
Toleo la Orthodox (OVC), lina vitabu 86;
Toleo la Charismatic (CV), lina vitabu 76;
Toleo la Roman Catholic (RCV), lina vitabu 73;
na matoleo yote ya Kiprotestanti yana vitabu 66, likiwemo The New World Translation of the Holy Scripture [1984] (NW), linalotumiwa na Mashahidi wa Yehova na matoleo mengine kama vile the King James [1611-1942] (KJ),
American Standard [1901-1944] (AS), Rivised Standard [1971] Second Edition (RS) Jerusalem Bible [1966] (JB), Good News Bible (1954: iliyochapwa 1956), Ronald A, Knox (Kx), New International Version (NIV), na motoleo mengine yasiyo na idadi.
Zaidi ya hayo, vipi kuhusu hoja ya Warejeaji wanosifika wa Biblia ya the Rivised Standard Version (RS), Rivised Edition ya 1952, na kwa Agano Jipya, Second Edition ya 1971, by Wm. Collins Sons & Co. Ltd. Iliyochapwa na Canadian Bible Society, isemayo katika Utangulizi wake:
(1) “Naam, Toleo la King James lina dosari kubwa mno.... dosari hizo ni nyingi sana na hatari sana kiasi cha kupelekea kuitishwa wito wa kurekebishwa kwa tafsiri yake ya Kingereza.”
(2) “Toleo la King James la Agano Jipya liliegemea katika mandiko ya Kigiriki yaliyoharibiwa kimakosa” Vipi kuhusu hoja ya Mashahidi wa Yehova katika chapa ya Mwamko ya Septemba 1951 inayoeleza; “Biblia ina makosa 50,000!”
Na vipi kama nikisema, kinyume na imani yenu, kuwa “Katika Waandishi wanne wa Injili Hakuna hata mmoja aliyekuwa Mwanafunzi wa Yesu ”
Katika (Luka 6:14-16 na Marko 3:17) tunaona yametajwa majina ya wanafunzi kumi na wawili na Yesu (AS).
Huku majina Mathayo na Yohana yamo, na majina Marko, Luka na Paulo hayajatwaja.
Hata hivyo, kutokana na nkuu zifuatazo, utagundua kuwa hizo Injili mbili zinatajwa kuwa ni za Mathayo na Yohana kwa kuwaheshimu tu, kwani ziliandikwa na mtu wa tatu. Soma nakala halisi ya mstari wa (Mathayo 9:9):
"Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani aitwaye Mathayo, akamwambia nifuate. Akaondoka akamfuata."
Na katika (Yohana 21:24):
"Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya; nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli?"
Katika aya ya kwanza, mwandishi anasimulia tu kile kilichotokea kati ya Yesu (AS) na Mathayo, huku katika aya ya pili, ni wazi kuwa kiwakilishi “nasi” kinawakilisha mwandishi.
"Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya; nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli?"
Katika aya ya kwanza, mwandishi anasimulia tu kile kilichotokea kati ya Yesu (AS) na Mathayo, huku katika aya ya pili, ni wazi kuwa kiwakilishi “nasi” kinawakilisha mwandishi.