Hiki ndicho alichoitiwa kwenye ofisi ya ZCO Mafwele
===========
Wakili wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Jebra Kambole, ameshangazwa na hatua ya Jeshi la Polisi kumhoji mteja wake, Boniface Mwabukusi, kwa tuhuma za Baraza la Uongozi la TLS kupokea fedha za kufadhili maandamano ya Oktoba 29, 2026 tarehe ambayo bado haijawahi kufika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya Mwabukusi kumaliza kuhojiwa katika Kituo cha Polisi, Wakili Kambole amebainisha kuwa tuhuma hizo hazina msingi wowote wa kisheria wala ukweli, kwani Baraza la Uongozi la TLS halijawahi kukaa au kujadili masuala ya kuratibu maandamano ya aina hiyo
Soma Pia: Mwabukusi atakiwa kufika ofisi ya ZCO Dar es Salaam tarehe 15 October