Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Kama rais utafanikiwa kufuatilia nyendo na maisha ya wateule wako utashangaa !! Awamu hii Haina ufuatiliaji kwa wateule wako ! Haina ukali na usimamizi huru wa rasilimali za nchi ! Wewe unatafuta hela ,unakopa ,unakusanya Kodi lakini pesa inatumiwa vibaya sana na wateule wako !! Wateule wako wanaishi kama wako peponi ! Kiuhalisia ni kwamba wanakumudu ! Ni vyema viongozi wasikalie ofisi kwa muda mrefu ikiwezekana iwe mwaka mmoja mmoja ! Wanaingia wengine ! Serikali yako iruhusu ukaguzi huru na tume ya maadili iwe na meno ya kufuatilia utajiri wa kutupwa wa mawaziri wako !! Kuna waziri wako mmoja anajilipa ml 74 kwa mwezi na Bado amefungua makampuni makubwa yenye usajili unaoanzia na neno z!! Huko ndio kichaka Cha kutakatishia fedha ! Kwa nini wateule wako wanatumia mali za umma kama mali zao binafsi? Mimi nashauri hili Baraza lote lipumzike isipokuwa waziri mkuu na naibu waziri mkuu ifanyike rotation na sura mpya ziingie kazini !!