Rais wetu Samia acha hotuba za kujitetea juu ya jinsia yako, wewe ni Rais siyo Rais mwanamke

Ni vigumu kujiamini kwa sababu dhambi ya uchafuzi wa 28/10 bado inamtafuna. "Hata msipotuchagua CCM itaunda serikali tu".
 
Ndo imeshatokea tu lakin kuna changamoto nyingi rais mwanamke., wakati akienda kujifungua nchi itakuwa kwenye likizo mpaka amalize siku 40, akiwa mja mzito nako pia ni changamoto kuna miezi fulani pale hataweza kuwajibika sawa sawa
ni kweli lakini sababu zako ni irrevelant kwa Mh Rais Samia. sidhani kama ana wakati tena huo wa kwenda labour
 
Ni sawa kuongelea ili kutukumbusha, maana siyo siri mfume dume haujatutoka, lazima aendelee kutupa kumbukizi
Hapana! Kishakuwa rais. Akiendelea kusema mwanamke anataka nini? Huruma ya rais mwanamke? Yaani akifanya vizuri iwe ni sifa kwa mwanamke na siyo rais? Ikumbukwe akivurunda pia itakuwa mwanamke.

Tunataka uongozi mzuri uwe ni wa rais Samia na siyo Samia mwanamke. Akivurunda pia iwe ni rais Samia na siyo Samia mwanamke. stigma bila mwisho haina faida, haijengi.
 
Kitu pekee ninachowaamini wanawake si wezi lakini vingine wanaitaji uangalizi mkubwa sana na kwenda nao kwa taadhari kwani tumeambiwa tuishi nao kwa taadhari sasa kama aliewaumba katupa alert
 
Anachukua tahadhari juu ya mfumo dume!
ni kweli bwashee, ila hata mie nadhani inatosha sasa asifanye tena hivyo...ni infiriority complex tu!.
dunia imebadilika sana na sasa tumeshuhudia wanawake wengi wenye uwezo kuliko wanaume ktk kada mbalimbali...hakuna haja kutumia nguvu kubwa kuwathibitia walimwengu tena.

Muhimu kazi iendelee kama moto yake inavyosema kisha baada ya miaka mi4.5 ndo tutapata jibu tulikuwa na Rais au Rais Mwanamke!.
Wengi tunamuombea apate mafanikio tele na hii itasaidia kupunguza ile dhana hasa huku Afrika kwamba mwanamke hawezi bila kuwezeshwa.
 
Wewe umeenda mbali hadi kuwajua wanaomsumbua. Siamini kama sababu ni hiyo. Wewe una mambo yako na maadui zako. Hii ni tabia anayoweza kuwa anaiunda yeye mwenyewe na anatakiwa aishinde yeye mwenyewe.
 
She's desperate! Tatizo hajiamini


Ukishaapishwa kuwa Rais haya mambo siyo ya kuyaongelea tena. mambo haya anatakiwa kuzungumza kama anashawishi watu wampe kura
Siyo bure kuyasema hayo. Lazima kuna jambo ameliona ndani ya system na kuongeza na zake. Kama ni kweli kuna ambao hawakutaka aapishwe, unadhani wanabadilika tu kwasababu kaapishwa?
Binafsi hata mimi nilijiuliza kwanini ametumia nguvu nyingi kuzungumzia hilo? Lakini nimeongeza na zangu. Labda kumekuwepo na ka “struggle” flani na yeye bado ameka “feel” na hivyo ku “attribute” “towards gender issues”
 
Mkuu, kabla ya kukimbilia kuhukumu mtu ebu jipe nafasi ya kudadavua na kujifunza kupitia kwa watu wengine. Sote tunafanya makosa lakini pia bado tuna fursa ya kujifunza kupitia watu wengine.

Ni vema kabisa, endelea kujifunza kwa wengine.

Kwa hoja yako iliyoitwa uharo umefafanua tofauti ya jinsi na jinsia, tofauti hizo zinajibu nini kwenye hii mada?

Samia ni mwanamke, tunamfahamu na anajitambua... ana haja gani kujikumbusha jinsi yake kila wakati?
 
Mkuu, kabla ya kwenda ndani ya mada husika, Je! umeona neno "jinsia" lilivyotumika katika kichwa cha habari? Ni hapo tu ndiyo ilipokuwa sehemu ya wadau kuelimishana kidogo.
 
Mkuu, kabla ya kwenda ndani ya mada husika, Je! umeona neno "jinsia" lilivyotumika katika kichwa cha habari? Ni hapo tu ndiyo ilipokuwa sehemu ya wadau kuelimishana kidogo.

Heshima mbele mkuu, naondoa makwazo yangu ya awali... nisamehewe tuendelee kujifunza.

Jinsia imekuwa ikitumika kimazoea mahali pa jinsi, labda kwa wanagenzi wachache kama wewe hapo ndio mnakuwa makini sana... ikiwapendeza moderators [kama wanaelewa] watahariri.
 
Kazi Iendelee bwashee!
 
Safi Kabisa !
Yeye achape kazi na ataproof wrong at the end of her tenure.
Hii anayoisemasema anajishusha mwenyewe.
SSH, My President ikiwa utapitia hapa leo, Tafadhali usirudie zile kauli za kujishusha na kujilinganisha, Fanya kazi na Kazi itakuinua yenyewe.
Ndaga lelo, Kyala Nnyaafu.
 
Aiseee kweli mama kazidi kila kukicha mi mwanamke,tunajua wote hvy na imeshatokea,afanye vitu kwa vitendo vionekane asiwe mtu wa kujiamini tu ,tunahitaji vitendo zaidi kuliko maneno,tumeshamuamini inatosha afanye kazi vitendo viwe vingi kuliko mipasho
 
Ndo imeshatokea tu lakin kuna changamoto nyingi rais mwanamke., wakati akienda kujifungua nchi itakuwa kwenye likizo mpaka amalize siku 40, akiwa mja mzito nako pia ni changamoto kuna miezi fulani pale hataweza kuwajibika sawa sawa
Kwani SSH anaendeleaa Kuzaa, si kashafikia ukomo, over 45! jamani.
 
Napata wakati mgumu sana kuandika maoni yangu juu ya jambo hili kwa sababu linawezekana likatafsiriwa kivingine na watu wengine.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…