Rais Zelensky utawalipa nini NATO?

Rais Zelensky utawalipa nini NATO?

Kwenye hili umepotoka sana ndugu yangu.

Jiulize, hivi nchi za Magharibi walipowaisaidia sana South Korea, hadi leo Korea kusini kufikia kuwa nchi tajiri kuizidi hata Urusi (achilia mbali North Korea ambayo wananchi wake wanaishi kwa kujikimu), South Korea wanalipa nini kwa mataifa ya magharibi? Je, wananchi wa South Korea wameuzwa kwa nchi za Magharibi? Jiulize pia, baada ya vita kuu ya Dunia, US iliisaidia sana Ujerumani Magharibi na Japan. Je, baada ya hapo hizo nchi zinailipa nini Marekani?

Na huko unakosema wananchi watauzwa, ebu fafanua, binadamu anauzwaje kutoka taifa lake kwa Taifa jingine? Maana binadamu siyo kitoweo au mchele.

Sioni namna ambayo Ukraine italazimishwa kumlipa yeyote. Urusi imepewa misaada mingi ya kifedha kutoka nchi za magharibi miaka ya 1900 mpaka 2000, imekuwa ikiyalipa nini hayo mataifa ya magharibi?

Sisi tuliwasaidia waganda, waSouth Afrika, Msumbiji, Komoro, Angola; je, wanatulipa nini?

Fahamu mpaka leo, wananchi wa North Korea wanauawa mpakani na South Korea, wakitorokea South Korea kutafuta unafuu wa maisha. Na kama kusingekuwa na sheria kali za kuwazuia wananchi wa North Korea kwenda South Korea, mamilioni ya wananchi wa North Korea wangehamia South Korea kuliko kubakia kwa yule Rais wao kichaa.
Ndugu hayo mataifa yote uliyoyataja unadhani yanapumua kwa U.S.A? Yanatii maelekezo ya U.S.A, huko pia ni kuuzwa, hayana utashi wowote nje ya matakwa ya USA, ndiyo maana kote huko ulikotaja USA kasimika kambi kubwa za Jeshi lake, Kwa kifupi mataifa yote uliyoyataja yanaiabudu U.S.A
 
Hero ni Putin maana kaongeza ardhi ya Urusi.
Ila kuna watu huwa siwaelew mmoja ni ww , hv huwa unatumia matacle kufikiri ? Kwa ardh yake kashindwa kuboresha maisha ya warusi 140M ndo awe shujaa wa kuiba ardhi ambayo pia haitabili lolote kwa warusi zaid ya kuwajazia mikodi. Ya ajabu ili kufidia gharama za vita
 
Mahaba yanakusumbua.

KIlichofanyika ni trade diversiom kutoka kufanya biashara na Ulaya/ USA na kugeukia Russia kufanya biashara na China/India na ncbi zingine za Asia Latin America nk. Hiyo sio kuwa koloni. Fuatilia volume ya biashara utaona.

Pili Fussia na Chima zinakubaliana kusaidiana kuifanya dunia iwe multi-polar iachane na unipolar world inayofuata matakwa ya Magharibi na hili ndio litakuwa faida kubwa ya vita hii kwa dunia.

Sasa asilimia kubwa ya biashara inafanyika kwa Yuan sio Dolla tena. Na baadhi ya nchi za kiarabu zimeanza kufanya biashara na China kwa Yuan.

Lengo la kuidhoofisha Russia limeshindwa na waliodhoofishwa ni Ulaya. Uchumi wao umeathiriwa , wananunua nishati kwa bei ghali zaidi stock ya baadhi ya aina za silaha imepungua mpaka below minimum level kiasi kwamba baada ya awamu hii ya msaada itakuwa viigumu kuendelea kutoa msaada kwa kiwango kklekile ndio maana wameweka matarajio makubwa sana kwenye hicho kinachoitwa counteroffensive ambayo dalili zinaonyesba imeishakuwa disrupted sana na mapigo ya sasa ya Rissia ambapo maghala ya hizo silaha na vifaa yameteketezwa.

RUssia kuwa na jamii zingine zaidi ya jamii kubwa ya kirusi sio ukoloni hata hiyo china haina jamii moja ya Han kuna watibet nk. Nchi nyingi zina mchanganyiko wa jamii japokuwa kunakuwa na jamii moja dominant .
Ukute na ww eti una bachelor kabisaaaa.
 
Mkuu Habari,

Kwakuwa wewe una information za kutosha, unaweza niambia media unazotazama kuhusu huo mgogoro na mimi nikwambie kitu.
Taja zote tafadhali
Swala sio media swala ni ukwel wa habari yako , usipende ubishi na mahaba ya kitoto , humu kuna watu wana matatizo ya pschology yaan wakipenda kitu wapo radhi kudanganya ili wanachokipenda kizungumziwe kwa uzuri , nahisi ww unaeza kuwa miongon , hv nchi gan yenye akili ndogo kufikia hatua kuisaidia ukraine iivamie urusi ? Hv hz akili zenu ndogo ndo mmahisi kila mtu anazo ? Ingekuwa nyepes ivyo kwann waitumie ukraine kuivamia nchi yenye nyuklia ? Kwamb hawajui kuwa urusi angerusha nyuklia ndan ya ukraine km majibu
 
Kuimaliza Russia ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu sana ya NATO, Zelensky anatumika kama scapegoat..

Russia was a really threat to the entire regime, power influence and economics to the entire NATO group and their allies.

Labda ungeuliza atawalipa nini maelfu ya raia wake waliopoteza uhai kwa vita isiyo na sababu za msingi kwenye mambo yaliyokuwa yanazungumzika.
Unajua kitu kimoja siwaelewi watu na hata huko mbeleni tutadaiwa. Mchokozi ni aliyeanza kurusha risasi au anayejibu? Ukipigwa kofi hutarudisha? Aisee kwa hiyo ungekua raisi wa Tanzania Kagame akija akikwambia Kagera ni mali yangu utampa tu? Ndicho mnataka Ukraine afanye?. Churchill alisema nitapigana mpaka tobe langu la mwisho. Aliongea maneno hayo wakati Ubelgiji imeshaanguka, Ufaransa ipo njiani kuanguka na jeshi la Waingereza wapatao 400,000 na vifaa vyote vya jeshi vikiwa Ufaransa. Hakukata tamaa. Alisimama kiume akawakomboa wanajeshi wake japo alipoteza vifaa vyake vyote. Miaka mitano mbeleni aliingia Berlin kwa ushindi. Aliyerusha risasi ya kwanza sio Ukraine. Na kama Russia inataka kupigana na NATO kwa nini isiwarushie makombora? Kwani wapo mbali nae? Mbona ni majirani wakubwa? Kule Siberia ni karibu mno na Alaska. Si ampige Mmarekani? Acheni kuwa na mawazo ya kiuonevu. Simama kwenye mstari wa haki uamue.
 
Kavamiwa baada ya kuegesha makombora mengi ya Kavita aliyotumiwa na NATO mpakani mwa Urusi.
Ingekua unachosema ni ukweli asingehangaika kutafuta vifaa vya kijeshi kila sehemu. Acheni kufungwa macho. Ushabiki wa upofu ni mbaya mno.
 
Ingekua unachosema ni ukweli asingehangaika kutafuta vifaa vya kijeshi kila sehemu. Acheni kufungwa macho. Ushabiki wa upofu ni mbaya mno.
Pia ushabiki huo huo ni haki ya mtu huwezi kumpokonya hiyo haki
 
Kwa hili mimi nipo na Rusia siwezi kuwa na mawazo mgando kisa msimamo wangu wa Tanzania

Kusimama na haki si kuwa na mawazo mgando bali ni kuwa na msimamo unaoeleweka.

Hakuna mpigania haki anayeweza kujinasibu Kwa kusimama na Russia kwenye hili.

Ndiyo maana si kupigania haki tu kulikopo bali hata u Simba na yanga nao ni sehemu ya maisha.
 
Back
Top Bottom