Ukitoa ugonjwa ni ngumu sana Mkuu wa nchi kuwepo ndani ya nchi nyingine kwa wiki nzima akifanya ziara labda awe anaumwa hivyo anatibiwa. Ila kwa Tanzania naona inaelekea kuwa jambo la kawaida sana kiongozi wao kufanya ziara na kukaa wiki nzima ndani ya nchi nyingine.
Kumbuka na uzinduzi wa Royal Tour Raisi alikaaa Marekani ziaidi ya wiki akifanya uzinduzi wa Filam. Hii ya Korea kusini ni ya pili sasa.
Hakuna mkuu wa nchi hata za Africa tu anaye fanya ziara iwe Ulaya au Asia au Marekani na kukaaa wiki nzima, hii ni Tanzania pekeee inawezekana. Ipo siki atakaa mwezi mzima akifanya ziara.
Levo ya Raisi ni kukutana na Raisi mwenzake basi, sasa wiki nzima anakutana na wakina nani huko Korea Kusini? Raisi anapaswa kujifunza kwa maraisi wenzake wanavyo fanya dhiara zao.
Wiki nzima utachokwa huko