Hebu tuweni serious kidogo na uongozi wa nchi yetu. Sidhani kama msanii Harmonize anajua hata majukumu ya mbunge.
Hajawahi hata kuwa na wazo la kugombea ubunge hapo kabla, lakini toka Rais Magufuli "Amtanie" jukwaani kuwa angependa awe mbunge ameichukulia serious hiyo kauli kana kwamba ni agizo au amri.
Mheshimiwa Rais ni mtu wa utani sana; alikuwa akitania tu kunogesha hotuba na siyo vinginevyo.
Bwana mdogo anawaambia watu kuwa kama Rais amesema basi yeye hana budi kukubali na kugombea ubunge? Kwani anayekwenda kuwatumikia wananchi ni Rais?
Hana mikakati yoyote ile wala nia, kampeni yake kubwa itakuwa "Magufuli kasema nigombee".