Uchaguzi 2020 Rajab Abdul "Harmonize" kugombea ubunge Tandahimba

Uchaguzi 2020 Rajab Abdul "Harmonize" kugombea ubunge Tandahimba

Agombee akichukua usishangae na uwaziri akapewa.
Magufuli inaelekea anapenda hawa wabunge mbumbumbu ambao hawawezi kuhoji chochote kinacholetwa Bungeni au kufanywa na serikali zaidi ya kuunga mkono kila kitu.

Sasa kwa kulitambua hilo, hawa mbumbumbu hawateui mawaziri badala yake anatoa mawaziri wake kutoka kwenye taasisi mbalimbali zenye wasomi nguli ndio hao akina Prof. Ndalichako, Prof. Kabudi, Dk.Mpango. Hawa mbumbumbu kugonga meza na kuleta mipasho ni kazi inayowatosha.
 
Kwa hapa wanachama wa Chadema lazima waponde maana wanajua mjeshi anaenda kuomba kupitia CCM
Mjeshi gani huyo? Hamonize kichwani ni mtupu hata ukiangalia enterview zake huongea kijinga jinga
 
Kiukweli from a neutral perspective hao wabunge mnaowataka wenye vitambi na elimu wamefanya mambo gani remarkable mpk mburudishaji huyu apingwe kwenda kugombea.

Tena mimi sina mzuka wa kupiga kura lkn ningekua natoka kule kwao ningeenda kumpigia kura.
Wakati mwingine tunahitaji watu kama hawa burudani kwa sana.

Hamna cha serious bunge linafanya zaidi ya ndio mzee. Hivyo bora tupate burdani tu
 
Hakuna tatizo, maana kwa tulipofikia hii nchi yeyote anaweza kuwa kiongozi.
 
Magufuli inaelekea anapenda hawa wabunge mbumbumbu ambao hawawezi kuhoji chochote kinacholetwa Bungeni au kufanywa na serikali zaidi ya kuunga mkono kila kitu.

Sasa kwa kulitambua hilo, hawa mbumbumbu hawateui mawaziri badala yake anatoa mawaziri wake kutoka kwenye taasisi mbalimbali zenye wasomi nguli ndio hao akina Prof. Ndalichako, Prof. Kabudi, Dk.Mpango. Hawa mbumbumbu kugonga meza na kuleta mipasho ni kazi inayowatosha.
Pata picha Hamonize akaungane na kibajaji, Msukuma na lijuakali hapo lazima waunde bendi ya taarabu Bungeni . aina hii ya wabunge majuha ndiyo wanapendwa na mtukufu ili iwe rahisi kupitisha katiba mpya inayofuta mfumo wa vyama na kuruhusu Tanzania kutawaliwa kifalume kama Oman, china
 
Juha kama Hamonize akiingia Bungeni heshima na thamani ya mbunge itashuka sana hata Dudu baya konk ataweza kuwa mbunge na hapo atapatikana spika atakayeishangaza Dunia
 
Hebu tuweni serious kidogo na uongozi wa nchi yetu. Sidhani kama msanii Harmonize anajua hata majukumu ya mbunge.

Hajawahi hata kuwa na wazo la kugombea ubunge hapo kabla, lakini toka Rais Magufuli "Amtanie" jukwaani kuwa angependa awe mbunge ameichukulia serious hiyo kauli kana kwamba ni agizo au amri.

Mheshimiwa Rais ni mtu wa utani sana; alikuwa akitania tu kunogesha hotuba na siyo vinginevyo.

Bwana mdogo anawaambia watu kuwa kama Rais amesema basi yeye hana budi kukubali na kugombea ubunge? Kwani anayekwenda kuwatumikia wananchi ni Rais?

Hana mikakati yoyote ile wala nia, kampeni yake kubwa itakuwa "Magufuli kasema nigombee".
 
Katiba haibagui lakini si kila mwenye haki kikatiba ana sifa ya kuwa kiongozi!

Kapitie maana na tafsiri ya kiongozi
Kwani hao wabunge wana kipi kipya kumzidi Harmonizer?
Kwanza yeye ni creative kuliko wengi
 
Back
Top Bottom