Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Ndugu zangu hivi haya maswala ya ndoto yana uharisia wowote kweli?samahan sana kwa kutoka nje ya mada
 
Habari ndugu zangu tunakumbushana ukiwa unafunga epuka kumsema mtu yeyote kwa jambo ambalo mwenyew akilisikia litamkera, epuka kusema uongo, kutazama wanawake wanaopita inamisha macho yako baada ya mtazamo wa kwanza, husivae nguo ambayo ulinunua kwa pesa haramu yan pesa hiyo kama ulidhulmu au uliiba au ulipata kwa njia ambayo sio halali utakuwa huna funga, husile vitu ambavyo vimepatikana kwa njia ya haramu yan futari yake isiwe imepatikana kwa njia ambayo sio halali, kama kwa pesa ya kuuza pombe,guest,hotel au hata kupatikana kwa kuuza nguo za kike za uchi kwa wenye maduka......

Ndugu waislam binadamu tunapaswa kuish kwa njia ya haki kila pumz yetu.

Tumia muda wako mwingi kusoma Quran ikiwa ujui waweza mtaja mwenyezi mungu kwa wingi utapata dhawabu pia.......

Tumia ramadan hii kufanya toba na kujutia uloyatenda.....
 
Wasalaam Maleko ndg ktk Uislam...!

Kuna jambo limeibuka ghafla la watu kuita Ramadhan Ramadan hili limekaaje
Ktk Dini je linakubaliwa?
 
YOTE SAWA TU ILI MRADI FUNGA INAKWENDA VEMA

Huyu jamaa bana eti wasalaam maleko ndo nini??!!!
 
We mwenywe umefanya makosa sana kwenye kutoa hiyo salamu ya mwenyezi Mungu.

Wasalaam Maleko ndio nini?
We we ndio uelewi , wasalaam ni kwa uwingi. Salam maleko ni kwa mmoja mmoja.
 
vyote ni sawa. kwenye lugha ya kiarabu kuna baadhi ya herufi ambazo huwezi kuziandika kwa lugha nyingine. ramadan ina herufi ﺽ ambayo huwezi kuiandika kwa kiswahili au kizungu ndo mana wengine wanaandika ramadhan au ramadan wengine ramazan.
 
Aah mbona wale wanaokula mchana mnawapiga?mkiambiwa ukweli muwe mnakubali bana

Ona huyu nae
IMG_20170614_184100.jpg

Mkuu funga analipa Mungu mwenyewe hakuna anayejua malipo yake, umejuaje kama ameshinda njaa? Either ni dhana au shirki. Omba istighifaar
 
Back
Top Bottom