Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

3d14a369fb0a51066f213cccbf4ec05e.jpg
 
You will know them by their virtues.

Huo ndiyo Uislam, hata wasio Waislam wayaone mema yetu.
Kabisa, unapotea sana kutukumbusha japo kidago, nakumbuka sana katika uzi wako wa faidika na darsa la faizafoxy, maswali yangu yalikuwa nachangamoto sana, ila mashaallah ulijitahidi kuyajibu kadri Allah alivyokuwezesha.


Ramadhan Mubarak
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] muumini wa kweli hufanya ibada bila kumbugudhi mtu wala kujionesha onesha hovyo kama ni mcha Mungu .

Hiyo ndo tabia yangu ukiniona utadhani ni mtu nisiyejua chochote kuhusu dini.
Swadakta
 
*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

*☪ LEO KATIKA FUNGA ☪*
*( 23 )*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{ ﺷَﻬْﺮُ ﺭَﻣَﻀَﺎﻥَ ﺍﻟَّﺬِﻱَ ﺃُﻧﺰِﻝَ ﻓِﻴﻪِ ﺍﻟْﻘُﺮْﺁﻥُ }*
*Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani.*
ﺳﻮﺭﺓ ﺍﻟﺒﻘﺮﺓ، ﺁﻳﺔ : .185
"""""""""""""""""""""""""""""""""""""

*[emoji287] ضيف آذان بالرحيل*
*MGENI AMEKARIBIA KUONDOKA 2⃣.*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُهِينٌ}*
```Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Allah Mtukufu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.```

Sura An-Nisa', Ayah 14

*NIMETANGULIZA AYA HII AMBAYO ALLAH MTUKUFU AMEWAAHIDI NA KUWAPA ONYO KALI LA KUWATIA MOTONI WATU WENYEKUMUASI YEYE, HII INATOKANA NA MSIBA MKUBWA AMBAO HUDHIHIRI KILA BAADA YA RAMADHANI KUMALIZIKA.*

*JE, MSIBA UPI?*

*هذه مصيبة كبيرة أن يعود شراب الخمر إلى خمورهم.*
*[emoji815] HUU NI MSIBA MKUBWA SANA, NI KUREJEA WANYWA POMBE KATIKA POMBE ZAO*

*ومتعاطي المخدرات إلى مخدراتهم.*
*[emoji815] NA WATUMIAJI WA MADAWA YA KUKEVYA KUREJEA KATIKA UTUMIAJI WA MADAWA YAO.*

*◇ وأصحاب الزنا إلى الزنا.*
*[emoji815] NA WAZINIFU KUREJEA KATIKA ZINAA.*

*◇ وأصحاب الربا إلى الربا.*
*[emoji815] PIA WATU WA RIBA KUREJEA KATIKA RIBA.*

*◇ وأصحاب الفسق ومجالس اللغو إلى اللغو.*
*[emoji815] WATU MAFASIQI WAOVU KUREJEA KATIKA UFASIQI, NA WAKAAJI WA SEHEMU ZA LAGHAU KUREJEA KATIKA LAGHAU.*

*[emoji830] هذه مصيبة كبيرة.*
*■ HUU NI MSIBA MKUBWA SANA SANA.*

*◇ دخلوا بالمعاصي وخرجوا بالمعاصي ما استفادوا شيئا أبدا،*
*[emoji815] WATU HAO WAMEINGIA NDANI YA RAMADHANI KWA KUFANYA MAASI NA WAMETOKA KWA KUFANYA MAASI, KAMWE HAWAKUPATA FAIDA KWA CHOCHOTE.*

*[emoji287] MWEZI WA RAMADHANI HAUPOKELEWI KWA MAASI WALA HAUAGWI KWA MAASI KADHALIKA.*

*■ WEWE AMBAE PENGINE UMEWEKA MALENGO HAYO, MUOGOPE ALLAH MTUKUFU, OGOPA ADHABU ZAKE, PIA HUJUI HUENDA SIKU HIYO NDIO IKAWA MWISHO WA UHAI WAKO NA KUA NA KHATMA MBAYA ALLAH ATUNUSURU KWA HILO NA MENGINEYO.*

*Allah ﷻ Anasema:*

*{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا تُوبُوا إِلَى اللَّهِ تَوْبَةً نَصُوحًا عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَنْ يُكَفِّرَ عَنْكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيُدْخِلَكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ يَوْمَ لَا يُخْزِي اللَّهُ النَّبِيَّ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ ۖ نُورُهُمْ يَسْعَىٰ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَبِأَيْمَانِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ}*
```Enyi mlio amini! Tubuni kwa Mwenyezi Mungu toba iliyo ya kweli! Asaa Mola wenu Mlezi akakufutieni maovu yenu na akakuingizeni katika Pepo zipitazo mito kati yake, siku ambayo Mwenyezi Mungu hatamdhalilisha Nabii na walio amini pamoja naye. Nuru yao inakwenda mbele yao na pande zao za kulia, na huku wanasema: Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.```
Sura At-Tahrim, Ayah 8

☪☪☪☪☪☪☪☪

*[emoji257] ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.*


*الدعوة اﻹسلامية.*
 
[emoji287]23[emoji287]
[emoji310]Hekima ya leo[emoji310]

*Imepokelewa kuwa kuna mwanamke mmoja alifiwa na mumewe na akataka kumtolea sadaka kila usiku wa ujumaa..*
*Ikawa kila usiku wa ijumaa anatengeneza chakula na kumpa mwanawe ampelekee faqiri fulani pale mtaani , wakati huwo huwo kwa vile uwezo mdogo akimyima mwanawe.*
*Ijumaa ya kwanza alipewa kijana apeleke huku njaa ikiwa imembana ila chakula alikifikisha.*
*Ijumaa ya pili alipewa apeleke na huku njaa imembana sawasawa ila chakula alikifikisha tena kwa yule faqiri..*
*Ijumaa ya tatu pia kijana alipewa apeleke, ila njaa usiku ule ilikuwa imembana kupita kiyasi ,akamuwa kile chakula akile yeye na akarudi nyumbani na akalala akiwa ameshiba..*

*Usiku ule yule mama alimuona marehemu mumewe usingizini akimwambia sijapata chakula isipokuwa leo..*

*Palepale mama alizindukana na kumfata mwanawe akamuliza kwa mshangao ..!*

*Chakula nilichokuwa ninakupa kila usiku ijumaa ukimpa nanii?*

*Mbona nimemuota baba yako leo usingizini akiniambia hajapata cahkula isipokuwa leo!?*
*Kijana akasema:nilikipeleka chakula kwa yule faqiri mara mbili pamoja na kuwa njaa ilikuwa imenibana sana ila mara hii sikuweza, kwavile njaa ilikuwa imenibana kupita kiasi, nikaamuwa nikile mimi na nikarudi na kulala.*

*Hapo mama ndipo alipokugunduwa kuwa mwanawe ndio aliekuwa anastahiki zaidi kile chakula kuliko mtu mwengine.*

*Jamani wale wanaotowa visadaka na zakka katika mwezi huu wa ramdhani na idi ndio hiyoo yapiga hodi ..*

*Watafuteni jamaa zenu huwenda wakawa wao wanahaja zaidi kuliko hao mnaowapa.*

*Amesema Mtume (s,a,w):*

*«الصدقة على المسكين صدقة، وهي على ذي الرحم اثنتان؛ صدقة وصلة»*
*(Sadaka kwa masikini ni sadaka (tu) nayo unapompa jamaa yako ni( mambo mema) mawili:sadaka na kumuunga (jamaa)).*

Ktk:Faidika na mawaidha.
Na:Muhamed Hilal Al abriy.

As/alaykum.
Mchana mwema.
Siku njema.
Mfungo mwema.
 
☆Alama za laylatul-qadri☆

Lailatul-qadri ni usiku mzima....

Unaanzia magharibi mpaka alfajiri...

Sivyo kama waitaqidiyo watu kuwa ni nyota utaiona....
Ukitoiona bahati yako ni mbaya...

Ile zionekaniwazo ni أنوار....
Malaika wanaoteremka, hali ibadilikao...
Basi wanakuwa wengi sana malaika...
Wewe unafikiria ni nyota.

Watu wanaiona (laylatul-qadr) kwa njia ya karama(kutukuzwa na mwenyezimngu)....

Kama alvotaja Al-imam nawawy...

Kama alvoeleza Ibnu-Taymiyyah ya Kuwa:
"Watu wanauona (usiku wa Laylatul-Qadr) kama mfano wa ndoto za watu wema"

Ukiona mambo kama yale....
Uombalo utapata, utakalo utalipata....
Na inakuwa usiku mmoja tu...
Katika masiku ya ramadhani....

Mtume (saw) ilimjia akawa atuambie...
Ni usiku gani (ndiyo inapatikana laylatul-qadr)...

Lakini kwa twabia zetu za kibinadamu mtume (saw) akatoka...
Alipowaona maswahaba wawili wagombana...

Au kwa mujibu wa hadithi yasema:

كان يتلاحيان
Walkuwa wakipapurana

Kila mmoja akimtoa nguvu mwenzake...
Wakiambiana maneno

Mtume (saw) akawaambia:
"Nimetoka niwaambie laylatul-qadri...

Lakini kwahali yenu hiyo, mtagombana...

Mpaka kwajili ya siku moja (laylatul-qadri ipitayo)...
Mtajaza miskiti, ikisha kupita (laylatul-qadri)... Hamtopita tena msikitini."

Kwasababu hiyo Laylatul-Qadri imeondolewa kujulikana siku yake:
فالتمسوها في العشر الأواخر
Itafuteni Laylatul-Qadri katika kumi la mwisho

Na mtume (saw) akaeka alama za Laylatul-Qadri:

Alama ya kwanza...
Usiku wake hauwi na baridi wala joto....
Hauwi na upepo utaona umetulia.

Alama ya pili....
Karibu na alfajiri....
Inanyesha mvua ya kupita...
Si mvua kubwa.

Alama ya tatu...
Jua linatoka na maskitiko...
Utaliona kama jua ni nyonge.

Alama ya nne...
Maji ya bahari yanakuwa kidogo tamu, kuliko siku zote.

Hizo ndo baadhi...
Na ziko nyingi alama zilotajwa na Ibnu-Hajar Al-Asqalani.
 
Kuna jingle(wimbo umekaa kama tangazo hivi) unatangazwa sana na kituo kimoja maarufu cha redio cha hapa jijini Dar es salaam....wenyewe wanajiita redio ya watu.. Lile tangazo kwa upande wangu nadhani linapotosha maudhui na dhumuni kubwa la mfungo wetu mtakatifu wa Ramadhan.. Tangazo linasema hivi kwa kifupi "........waislamu fungeni mpate afya njema...." kwa upande wangu dhumuni kubwa la mfungo sio kupata afya njema ya mwili, nadhani bora ingekua "kupata afya njema ya Roho".. Na kama kuna mwislamu anafunga ili kupata afya njema ya mwili atakua kakose japo hilo laweza kua ni lengo moja wapo lakini dhumuni kubwa ni Afya ya Roho, kwa kutenda mema, kusali sana na kuomba toba kwa Allah..

In short tangazo hilo lina boa na kubadili dhumuni kwa watu wanao lisikia hasa wale wa madhehebu mengine na waislamu kwa ujumla... Wadau mnasemaje..
 
Back
Top Bottom