Ulikuwa Muislamu bogas , mimi mwenyewe nilikuwa Muislamu bogas lakini Alhamdulillah nimefanikiwa kupunguza kiwango changu Cha ujinga At least nimejua vitu basic sana katika dini na misingi ambayo nikishikilia ni ngumu kupote In Shaa Allaah.
Kabla ya kuwa hivi nilishawahi kujiuliza maswali kibao kuhusu Mungu na uwepo wake , Kuna kipindi nipo darasa la sita nilikaa nikafikira hili swala deeply peke yangu mpaka nikahisi kuchanganyikiwa , nikijiuliza mambo kibao kama uwepo wa shida Duniani , maujai , dhiki nk na kuhusu Shetani nikawa siku zinavyoenda narudia rudia ...
Nikaja swala la dini nikaanza kujiuliza Nina uhakika gani kama nipo upande sahihi ? Je , vipi ikiwa Wakristo ninaowaona wamepoteza wapo katika haki ? Je, ningezaliwa katika familia isiyo ya Kiislamu ningekuwa Muislamu?
Nijajiunga Jf nikakuta controversial idea and thoughts nyingi kuhusu Mungu na dini hapo ndipo ikabidi nitenge muda wangu kuchunguza hili swala deeply kielimu na kiakili ndipo nikajiridhisha Uislamu ni dini ya haki kabisa pasipo na shaka yeyote.
Sikumaliza hapo ndani ya Uislamu nikakuta bado kuna makundi na itikadi nyingi sana na kila upande unadai wao wako sahihi zaidi nalo linichanganya sana , napo nikatenga muda wangu kusoma na kufuatilia karibia kote kwa haki mpaka nilipobainikiwa njia sahihi ni ipi katika Uislamu.
Mimi katika maisha yangu sijachangua niwe bogas lazima kila kitu kinachonihusu hata kidogo nakifuatilia deeply kujua uhalali na usahihi kielimu , sasa wewe huenda ulikuwa Muislamu ila Muislamu oya oya wa kupelekeshwa na kufuata mikumbo.