Hembu wewe tuambie inakuaje Kwaresma, Ramadhani, Naw-Ruz na Holi ziangukie mwezi mmoja??
Ramadhani Imeanza Kulingana Siku hizi tu na Mwezi wa Kwa Rezima Ila Zamani haikuwa Hivyo..
Hiyo ni simple tu inatokana Na Tarehe Kufanana na Ikumbukwe Tarehe za Kiislmu Yaani Hijriya Zinaenda Tifauti na Tarehe za Dunia au Za Roma au Miladiya..
kwanza Nikukumbushe Kwamba Ramadhani Ni mwezi wa 9 Wa Calendar ya Hijriya Na Calendar ya hijiriya Ina Siku 30 kwa Kila Mwezi na Siku zake Hutegemea na Mwezi..
Kwa Kuanza Hii ndo miezi ya Kiislamu au Miezi ya Hijriya..
1. Muharram (المحرّم)
2. Safar (صفر)
3. Rabi' al-Awwal (ربيع الأول)
4. Rabi' al-Thani (ربيع الآخر)
5. Jumada al-Awwal (جمادى الأول)
6. Jumada al-Thani (جمادى الآخر)
7. Rajab (رجب)
8. Sha'ban (شعبان)
9. Ramadhan (رمضان)
10. Shawwal (شوّال)
11. Dhul-Qa'dah (ذو القعدة)
12. Dhul-Hijjah (ذو الحجة)
Na Hii ndo Miezi ya Kimiladiya..
1. Januari (January)
2. Februari (February)
3. Machi (March)
4. Aprili (April)
5. Mei (May)
6. Juni (June)
7. Julai (July)
8. Agosti (August)
9. Septemba (September)
10. Oktoba (October)
11. Novemba (November)
12. Desemba (December)
Na Kwakujibu Swali lako Nitarudi Miaka Kumi Nyuma Kuprove Theory Zote mlizotoa Ni just Conspire tu na Haina Uhalisia..
Mwaka 2015, Ramadhani ilianza tarehe 18 Juni, na Kwaresima ilianza tarehe 18 Februari.
Mwaka 2016, Ramadhani ilianza tarehe 6 Juni, na Kwaresima ilianza tarehe 10 Februari.
Mwaka 2017, Ramadhani ilianza tarehe 27 Mei, na Kwaresima ilianza tarehe 1 Machi.
Mwaka 2018, Ramadhani ilianza tarehe 16 Mei, na Kwaresima ilianza tarehe 14 Februari.
Mwaka 2019, Ramadhani ilianza tarehe 6 Mei, na Kwaresima ilianza tarehe 6 Machi.
Mwaka 2020, Ramadhani ilianza tarehe 24 Aprili, na Kwaresima ilianza tarehe 26 Februari.
Mwaka 2021, Ramadhani ilianza tarehe 13 Aprili, na Kwaresima ilianza tarehe 17 Februari.
Mwaka 2022, Ramadhani ilianza tarehe 2 Aprili, na Kwaresima ilianza tarehe 2 Machi.
Mwaka 2023, Ramadhani ilianza tarehe 23 Machi, na Kwaresima ilianza tarehe 22 Februari.
Mwaka 2024, Ramadhani ilianza tarehe 11 Machi, na Kwaresima ilianza tarehe 14 Februari.
Mwaka 2025, inakadiriwa kuwa Ramadhani itaanza tarehe 1 Machi, na Kwaresima ilianza tarehe 5 Machi...
Sasa hiyo Hapo Juu Inaprove nini Inaprove kwamba Calendar Baina ya Miladiya na Hijriya hazina Static Formation na Haziwezi kuwa..
Ramadhani Imewahi Kuwa Mpaka Mwezi wa Kumi na Moja na Mwezi wa Kumi na Mbili ila KWARESMA haijawahi na Itakuja Kuwahi kuwa..
Na Mwaka 2033 Tunategemea Idd El fitri Itaangukia Tarehe 25/12 siku ya Xmass Najua Pia itakuwa Story nyingine kwa Watu wa Kuconspire