DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Samahani Kwa Kusema Hili Najua Kama Wewe Ni Mwislamu Na Umefunga Unaamini Kuwa Funga Hulipa Mungu peke yake na Hakuna Kiumbe chochote Kinahusika nayo..Hadithi ni porojo za kubuni
Ila Kwa Jibu lako Hilo Umeharibu Funga Yako na Umeshinda Njaa Tu š¤£š¤£
Nimekuwa Muslimu kwa Muda Mrefu sana Na Tamko kama Hilo Linaweza Kumtoa Mtu katika Uislamu..
Turudi Kuhusu Hadithi Ni Porojo š¤£š¤£
Sikukatalii Wala Sikukubalii Kuhsu hilo ila Since Unafata Imani ya Kiislamu Hadithi ni tool ya Pili baada ya Quran..
Na Hii Inakubaliwa na Maulamaa wa Pande zote Na Wanazuoni wa Shia hata Wa Sunni kwa madhehebu yote..
Kupitia Hadithi Ndo hupatikana Sunna na maagizo ya Mtume..
Kama Quran inavyotaka Kufanyika..
Qur'an 4:59
"Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wale wenye mamlaka miongoni mwenu..."
Qur'an 4:80
"Anayemtii Mtume, basi kwa hakika amemtii Mwenyezi Mungu..."
Qur'an 59:7
"Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho..."
Qur'an 3:31
"Sema: Ikiwa mnapenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakusameheni dhambi zenu..."Qur'an 7:157
"Wale wanaomfuata Mtume, Nabii asiyejua kusoma wala kuandika, ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurati na Injili, anawaamrisha mema na anawakataza maovu, na anawahalalishia vilivyo vizuri na anawaharimishia vilivyo vibaya, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyokuwa juu yao..."
Nawwza Nikaandika Aya Nyingi sana Ila Haisaidii kitu Ila kama Ni muislamu Amini katika Uislamu ukitaka kuwa Kama Mimi Kuwa kama Mimi ila Usichanganye mawili