Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #961
Iv kiongozi shimo la choo kikawaida inatakiwa kuwa na urefu gani na je kujenga shimo moja na mawili bora ni ipi hapoMiaka ya nyuma, ilikuwa unakuta nyumba ina choo na bafu lakini miaka ya sasa vyoo vinajengwa 2 in 1 (choo kinatenganishwa sehemu mbili kwa step moja ndogo, ambapo sehemu inapokaa sink la choo inakuwa juu, na sehemu iliyobaki ambayo inakuwa chini inakuwa ni sehemu ya kuogea)
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Kawaida kina huwa ni futi 12, japo kuna muda mtu anaweza akachimba akakutana na maji kabla ya kufikia hicho kina (hapa itabidi uongeze marefu ya karo ili kufidia futi zitakazopelea kufikia hicho kina)Iv kiongozi shimo la choo kikawaida inatakiwa kuwa na urefu gani na je kujenga shimo moja na mawili bora ni ipi hapo
Ok shukran mbona naona watu wengi wanasema mashimo ya round ndo mazuri kuliko pembe nne unaweza ukaniambia lipi zuri kati ya round au pembe nneKawaida kina huwa ni futi 12, japo kuna muda mtu anaweza akachimba akakutana na maji kabla ya kufikia hicho kina (hapa itabidi uongeze marefu ya karo ili kufidia futi zitakazopelea kufikia hicho kina)
Kila shimo lina kazi yake, kama uchumi unaruhusu chimba mashimo yote mawili lakini kama uchumi hauruhusu, chimba shimo moja (shimo la pembe nne)
kila moja lina kazi yake. ila la muhimu ni hilo la pembe nne. hilo hujulikana kama septic tank. Lina kuwa na mfumo ndani unaosaidia kuvunjavunja kinyesi ambapo humo ndani kuna anaerobic bacteria wanao saidia kuchakaa hicho kinyesi na maji hupita kwenye mfumo mwingee na hapo ndo umuhimu wa shimo la pili linapotokea ambalo lenyewe linatakiwa kujengwa kwa staili ya kuruhusu maji kupaculate arthini kidogo kidogo.Ok shukran mbona naona watu wengi wanasema mashimo ya round ndo mazuri kuliko pembe nne unaweza ukaniambia lipi zuri kati ya round au pembe nne
hii ya kupanga mawe ninzuri ili kuepukana na adha ya kutumbukizwa kwenye mashimo na wezikila moja lina kazi yake. ila la muhimu ni hilo la pembe nne. hilo hujulikana kama septic tank. Lina kuwa na mfumo ndani unaosaidia kuvunjavunja kinyesi ambapo humo ndani kuna anaerobic bacteria wanao saidia kuchakaa hicho kinyesi na maji hupita kwenye mfumo mwingee na hapo ndo umuhimu wa shimo la pili linapotokea ambalo lenyewe linatakiwa kujengwa kwa staili ya kuruhusu maji kupaculate arthini kidogo kidogo.
hilo shimo la kwanza ni la muhimu sana kama uchumi hauruhusu jenga hilo la kwanza vizuri. shimo la pili unaweza tengeneza kitu kama fench drain, ambapo ni mtaro mkubwa unao pangwa mawe au maburungutu na kufunikwa na nailoni kisha kufukiwa juu, humo ndani yanaenda maji tu kinyesi chote kinabaki kwenye mfumo wa kwanza.
Kama nilivyosema awali, kila shimo lina kazi yakeIv kiongozi shimo la choo kikawaida inatakiwa kuwa na urefu gani na je kujenga shimo moja na mawili bora ni ipi hapo
Una maoni yoyote kuhusu shimo lenye chamber 3. Kami hili. Maji taka yanapitia chamber 3 kabla ya kwenda soakway.Kama nilivyosema awali, kila shimo lina kazi yake
Kama utaweka shimo moja (la pembe nne), maana yake hilo shimo litachukua muda mfupi kujaa ukilinganisha na mtu aliyeweka mashimo yote mawili kwa sababu maji yake yatakuwa hayana mahali pa kwenda, lakini kama ukijenga mashimo yote mawili, maji yatakayojaa kwenye shimo la pembe nne yatapelekwa kwenye shimo la duara (ambapo hili shimo la duara pembeni huwa linaachwa matundu kwa ajili ya maji kupotelea ardhini)
Haya mashimo ya kisasa ujenzi wake ni kama ilivyo mashimo ya pembe nne (hawaachi matundu pembeni), lakini pia ikumbukwe tofali zake hazijengwi kwa udongo (mortar) kwa hivyo maji yake yanakuwa yanapotelea ardhini kupitia upenyo uliopo kati ya tofali na tofali japo pia huwa wanaweka na shimo lingine pembeni kwa ajili ya kupokea maji yanayotoka kwenye shimo la kwanza
Kwa hapo sijajua kazi ya hiyo chamber ya tatu inayofuata (labda tukiona namna ilivyojengwa huko chini, isije ikawa hiyo chamber ya tatu inatumika kama soak way pit)Una maoni yoyote kuhusu shimo lenye chamber 3. Kami hili. Maji taka yanapitia chamber 3 kabla ya kwenda soakway.
View attachment 3257694
View attachment 3257716
Nilivyoelewa ni kwamba ukiongeza idadi ya chamber kabla ya soakway unaongeza uwezekano wa kupata maji safi mwisho wa mchakato.Kwa hapo sijajua kazi ya hiyo chamber ya tatu inayofuata (labda tukiona namna ilivyojengwa huko chini, isije ikawa hiyo chamber ya tatu inatumika kama soak way pit)
Kawaida shimo la septic linakuwaga na sehemu mbili, ambapo kati kati kunakuwa na ukuta unaozuia taka yabisi (solid waste) zisiende kuingia katika chamber inayofuata na matundu yake katika huo ukuta huwa yanakuwa juu kama ilivyo hapo kwenye picha kwa sababu maji ya chooni huwa yanajitenga katika matabaka matatu (ambapo tabaka la kati ndio maji yenyewe ambayo tunataka yaende katika soak way pit)
Yale mawe yanayojazwa kwenye msingi huwa yana kazi gani, na kuna tatizo kama utaamua kujaza mchanga pekee badala ya udongo au mawe?.Baada ya kupanga mawe (hardcore) katika msingi, inashauriwa umwage mchanga mwingi ndipo uje umwage zege la jamvi (oversite concrete). Hii ni kwa sababu unapopanga mawe, ile nafasi iliyopo kati ya jiwe na jiwe zege inaweza isipite kwenda kuziba hizo nafasi. Kama hiyo sakafu itapata mgandamzo mkubwa (mfano gari ikapita) inaweza kusababisha hiyo sakafu kutitia kutokana na uwepo wa uwazi (matundu) uliopo chini yake
Kama unahitaji ramani za kitaalamu na makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
Hivyo vionjo vya kwenye madirisha huwa mnazingatia athari za kimazingira kweli, maana hapo kuna vumbi, ndege, baibui kuja kujaza uchafu.Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasilianeView attachment 3259760
room ngapi apa na ina mita ngap kwa ngapRamani, Makadirio au Ushauri tuwasilianeView attachment 3259760
Makadirio yake yapoje hii mkuu...?Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasilianeView attachment 3259760
Nami ningependa kujua haya mawe yanaongeza nini maana naona si kila project inatandika mawe kabla ya kumwaga zege. Labda mwenye uzoefu wa miradi ya serikali anaweza kutujuza. Mawe ni lazima au hapana?Yale mawe yanayojazwa kwenye msingi huwa yana kazi gani, na kuna tatizo kama utaamua kujaza mchanga pekee badala ya udongo au mawe?.
Room tatu, vyumba viwili ni self room, kimoja ni single room, sebule, jiko, na dining. Ukubwa ni mita 10 kwa 12 ila vyumba vyake ni vya wastani, nimeitengeneza kulingana na ukubwa wa kiwanja cha mteja pamoja na mahitaji yakeroom ngapi apa na ina mita ngap kwa ngap
Ukipata jibu naomba unijuze pia.Yale mawe yanayojazwa kwenye msingi huwa yana kazi gani, na kuna tatizo kama utaamua kujaza mchanga pekee badala ya udongo au mawe?.