Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Baada ya kufunga na kumwaga mkanda wa juu, pandisha kozi tatu badala ya mbili kama wengi wanavyofanya. Kumbuka ule mlalo wa bati (overhang) utaificha kozi moja (au na zaidi) na hivyo itabaki kozi moja inayoonekana ambapo nyumba itaonekana kama imemezwa na paa. Ukiweka kozi 3, nyumba itapendeza zaidi na pia itafanya hata taa za nje zikae vizuri bila shida
 
Huu mfumo unahitaji umakini sana, mimi binafsi napembelea mfumo wa contemporary ambao mfereji wake unazungukia nje kama ilivyo pvc gutter. Upauaji unakuwa wa kawaida (angle ndogo) ila bati linakuwa halionekani na mzunguko wa bati wote unadondoshea maji kwenye huo mfereji (hakuna kuchimbia bati kwenye ukuta)

Ningewatumia picha ila sasa shida picha sio ya kwangu na mmiliki wa picha akiona nimetumia picha yake itakuwa shida
Nimekupata, asante.
 
Bei inaanzia 50,000 na kuendelea mkuu, inategemea na ukubwa / aina ya nyumba. Ukishakuwa na makadirio full, utaepukana na zile gharama za kumlipa fundi kuja site kupima pima mfano fundi tiles akija lazima atapima kwanza ili akupe hesabu ya vifaa (atakata umpe nauli) n.k
fundi aje nimpe nauli mkuu! labda nimerogwa....
ila nimependa kazi yako nitakutafuta kwa ramani ya nyumba ya kupanga ya vyumba vilivyogawanyika kwa single na double self
 
Boss vipi kuhusu apparent ya chumba kimoja master, on the side kina laundry room

Na kina sehemu multi purpose (jiko sitting place na dining place)
Bila shaka ulikuwa unamaanisha apartment sivyo? Tuwasiliane mkuu, mimi nadesign nyumba ya aina yoyote kwa kufata maelekezo ya mteja (na kumshauri pia, mana kuna muda mteja anatoa maelekezo ambayo yanakinzana na aspects of designing)
 
Kama unataka kujenga nyumba ya vyumba vitatu, basi ni heri ukawa na master 1, self moja kwa ajili ya watoto wa kike, na single moja kwa ajili ya watoto wa kiume ambapo hawa wa kiume watakuwa wanatumia choo cha public.
Zama zimebadilika, karne hii sio ya kuwaruhusu watoto wa kike na watoto wa kiume wapishane chooni wakiwa wamevaa taulo. Itafanya hata wenyewe kwa wenyewe wasiheshimiane

Ukija kwangu ukanipa maelekezo ya ramani unayoihitaji, nitakupatia ushauri wa kitaalam kama kutakuwa na chochote cha kurekebisha ili upate ramani yenye kufuata misingi yote ya designing
 
wakati huo huo pale hardware uliponunulia hizo tiles kuna box za tiles ambazo baadhi ya vipande vimekatika na muuzaji anauza kwa bei ya hasara hivyo kama ungechanganya box nzima na zile zilizokatika ungeokoa kiasi flani cha pesa
Usijidanganye mkuu ule mpasuko huwa hauko uniform, niliwahi kufuata ushauri huu kutoka kwa fundi wangu nikajikuta narudi kunua tile zingine nzima ili nipate ladha halisi ya floor niliyotake na yale mavipande yapo mpaka leo
 
Malizia kusoma hiyo comment mpaka mwisho utaona kuna sentensi kwenye mabano. Inawezekana pia walikuchanganyia na rejected, tiles ninazosemea ni zile ambazo zinavunjika kwenye ncha kutokana ule upakiaji/ushushaji wa tiles
 
Point noted
 
Rekebisha hizo vent za huko kwenye paa, hazina kazi yoyote zaidi ya kuozesha ceiling board
Nimeona nyumba nyingi ati wanaweka vioo kwenye vent sijui huwa wanajua kazi yake
 
Nimeona nyumba nyingi ati wanaweka vioo kwenye vent sijui huwa wanajua kazi yake
Kama mtu hapendelei kuweka roof vents, basi anatakiwa aweke vile vitofali vyenye matundu matundu au kuna vingine vinakuwa duara. Hapo utakuwa na kazi ya kupambana na mijusi kuingia kwenye hivyo vitundu
 
Maeneo mengine wanaweka wooden louvers na wavu mgumu kwa ndani
 
348811620_785261603237942_7115873423779434829_n.jpg
 
Kabla ya kuanza kupandisha tofali za boma, ni vizuri ukatandika nailoni maalum (Damp proof course ,DPC) juu ya tofali za msingi(au mkanda kama umeweka) ambapo itasaidia kuzuia unyevu nyevu usiweze kupanda juu na kuathiri kuta za boma.
 
Hizo kazi yake ni kuruhusu mzunguko wa hewa ambapo kama usipoweka, lile joto la hewa iliyopo kati ya paa na dari kipindi jua linawaka inasababisha hewa kuwa na pressure ambayo inaenda kusukuma mikanda ya pembeni ya dari na gympsum board na kusababisha mipasuko ktk maungio
Mipasuko katika dari/mikanda ya gympsum kutokana na joto kali la hewa iliyopo kwenye dari baada ya kukosa sehemu ya kutokea nje
FB_IMG_1697019668911.jpg
 
Back
Top Bottom