Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Leo tuangalie upande ambao SEBULE na VYOO vinapotakiwa vikae

Katika pande zote nne yaani Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi, upande wa Kaskazini ndio upande ambapo unapokea jua ama joto kwa kiasi kidogo na upande wa Kusini ndio upande ambao unapokea jua ama joto kwa kiasi kikubwa katika masaa yote ya siku (asubuhi mpaka jioni). Upande wa Mashariki hupokea joto jingi kuanzia asubuhi mpaka mida ya mchana, na upande wa Magharibi hupokea joto jingi kuanzia mchana mpaka jioni

Sebule inatakiwa ielekee Kaskazini kwa sababu ni sehemu ambayo muda mwingi watu watakuwa hapo (asubuhi mpaka jioni) hivyo haitakiwi iwe upande ambao utakuwa sio rafiki kukaa katika mazingira hayo

Tukija upande wa Kusini ambao unapokea joto jingi zaidi katika masaa yote ya siku, kitu ambacho unaweza kuweka upande huu (kusini) ni vyoo na mabafu. Hii ni kwa sababu chooni sio mahali ambapo watu hukaa muda mrefu, watu hukaa muda mfupi na pia ni kwa mara chache.

Ramani, Makadirio na Ushauri wa kitaalam tuwasiliane +255(0)624068809
Una Plot Kariakoo hizi mbwembwe utabaki nazo Jamii Forums tu
 
UFUNDI UMEME


(1) Hata kama unampa ela ya vifaa fundi basi ni vizuri kuakikisha alichokiandika ni sahihi maana mafundi uwa tuna tamaa baada ya ela kuwa mikononi.unakuta fundi kakuandikia waya(kampuni ya euro)ila unashangaa analeta site waya usiojulikana.hii ni hatari sana kwa usalama wako na vifaa vyako.

(2) Kabla ya kufanya wiring ni vizuri wewe muhusika kumwambia fundi maitaji yako yote ya vitu ambavyo utakuja kutumia baadae ili isije ikatokea changamoto ya kufanya upanuzi wa maitaji mengine ya umeme.mfano kwenye stage ya kwanza(kuchimbia bomba) ni vizuri kuweka point nyingi ili hata ikitokea unaitaji kuongeza kibu basi kusiwe na changamoto.

(3) hakikisha umeme wowote unaopita chini ya ardhi basi ununue waya maalum kwa ajili ya chini ya ardhi.sio kila waya una uwezo wa kupita chini ya ardhi.hii baadae itakuja kukuletea shida wakati huo utashindwa kufanya kitu kwa sababu gharama ya marekebisho itakuwa kubwa.

(4)Hakikisha unanunua vifaa vya umeme ambayo kwa ndani vimetengenezwa kwa copper na sio chuma kilicholambishwa copper.kampuni yenye vifaa vilivyotengenezwa kwa pure copper kwa hapa nchini ni( Tronic,ABB,Africab,havels)


(5)Hakikisha fundi anatumia bomba kwenye kufanya wiring na pia anafunga na mifuniko kwenye sehemu zenye juction box ili kuzuia wadudu kufika kwenye switch au main switch.

(6) Hakikisha fundi anaorodhesha matumizi yako yote kwenye kuomba mita tanesco ili usije ukapewa mita ndogo ukashangaa umeme unaenda mwingi kumbe mita inazidiwa.hakikisha taarifa za matumizi alizoweka kwenye mchoro ni sahihi.





Kwa ushauri pamoja na kazi piga namba
+255(0)624068809


(Mrs .Hechy Essy)
Bro, we acha tu hiyo content yako ibaki yenyewe, namba yangu na jina uliloweka hapo chini naomba uondoe, mimi nitajitangaza mwenyewe
 
Una Plot Kariakoo hizi mbwembwe utabaki nazo Jamii Forums tu
Sio kkoo tu, hata huku mtaani kuna muda inakulazimu upande wa mbele wa nyumba uelekee sehemu flani kutokana na mpangilio wa barabara za mitaa. Hii pia ni changamoto
 
Kwenye ubandikaji wa tiles, mafundi wengi wanakosea kutumia pima maji (spirit level), ndio maana unakuta fundi alitumia pima maji lakini baadae maji yakijaa sakafuni bado yanatengeneza bwawa/vibwawa upande mmoja (floor inakuwa haipo level)

Sasa leo nitaelekeza namna ya kuitumia pima maji kiusahihi

Unapoiset ile tile ya pili kwa kufuata tile ya kwanza, hakikisha sehemu kubwa ya pima maji (zaidi ya nusu ya urefu wa pima maji) imelala upande wa tile ya kwanza, kwanini iwe hivi?

Sehemu kubwa ya pima maji ikilalia upande wa tile ya pili (ambayo haipo level), uzito wa pima maji utaelemea upande wa tile ya pili na kufanya hiyo pima maji yenyewe isiwe level kwa hivyo matokeo yatakayopatikana hapo hayatokuwa sahihi kwa asilimia 100 licha ya ile bubble kuwa kati kati ambapo tiles zote zinaweza zikawa level lakini kila moja ikawa na level yake.
 
Wakati wa kupaua nyumba, jitahidi zile tie beam usiziweke kati kati ya beam za madirisha na milango kwa sababu zinaongeza mzigo zaidi na kufanya beam ipinde ambapo itasababisha nyufa mlalo (horizontal crack) kati ya mkanda (beam) na kozi ya chini yake.

Ikishindikana kabisa kabisa, pitisha tie beam mwanzoni au mwishoni mwa hizo beam (beam ambazo chini kuna uwazi wa madirisha na milango) kwa sababu deflection ktk beam ni maximum katikati, na ni minimum karibia na support
 
Katika upigiliaji wa gympsum board, ni vizuri ule upande mrefu (244mm) spacing ya mbao ukatumia 81mm badala ya 122mm. Hapa namaaminsha ule upande mrefu uwe na mbao mbili kati kati badala ya mbao moja kwa sababu gympsum ni nzito, ukipigilia mbao mbili kati, dari linakuwa imara zaidi
 
Kuna tiles zingine inabidi ziwekwe kwenye maji kabla ya kuanza kuzibandika. Ukianza kuzibandika bila kuziloweka, zinaanza kufyonza yale maji yaliyopo kwenye udongo wa kubandikia na hivyo kufanya zisishikane vizuri na kubanduka baada ya muda. Utakapoziloweka kwenye maji, zitashiba maji vizuri na hivyo hazitoweza kufyonza maji ya kwenye udongo na kufanya hydration reaction isimame au ipungue kasi kutokana na kupungua kwa maji

Tiles ambazo kasi yake ya ufyonzaji maji ni chini ya asilimia 0.5 hazihitaji kulowekwa kwa sababu zinafyonza maji kidogo sana ambapo haiwezi kuathiri hydration reaction, lakini kuna tiles ambazo kasi yake ya ufyonzaji maji ni zaidi ya asilimia 10 (hizi ni lazima uziloweke kwenye maji ili utakapozibandika zishikane vizuri na udongo/sakafu)

Swali : Utajuaje kama tiles zako zinafyonza sana maji au lah?
Chukua kipande cha tile, kigeuze (kule chini kuwe juu), chukua matone ya maji weka juu yake. Kama hayo matone yatapotea haraka, basi tiles zako zinafyonza maji kwa kiasi kikubwa na hivyo zinahitaji kulowekwa kwenye maji kabla ya kuzibandika. Kama hayo matone yatakaa muda mrefu bila kufyonzwa basi tiles zako hazifyonzi maji mengi na haina ulazima wa kuziloweka.
 
Hapa ni baada ya mtu kuuliza kama kisado cha rangi (4ltrs) kitatosha kupaka rangi chumba kimoja
20231127_072046.jpg
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)

Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Nyie ndio mnaoharibu hii fani...Na ukute hauna ujuzi wowote zaidi ya ku google plans na kuedit kidogo.
 
Nyie ndio mnaoharibu hii fani...Na ukute hauna ujuzi wowote zaidi ya ku google plans na kuedit kidogo.
We jamaa wa ajabu sana. Utakua mtu fulan hivi mwenye kinyongo, roho mbaya, wivu au kijicho. Yaani ni mtu ambae ukiona mwenzio anafanya jambo hata kama halikuhusu lakin linakukera tu.

Ungeweka wazi kipi ambacho mleta mada amekosea ungeonekana mwerevu. Lakini kwa hivi ulivyofanya ni wazi wewe una wivu wa kike.
 
We jamaa wa ajabu sana. Utakua mtu fulan hivi mwenye kinyongo, roho mbaya, wivu au kijicho. Yaani ni mtu ambae ukiona mwenzio anafanya jambo hata kama halikuhusu lakin linakukera tu.

Ungeweka wazi kipi ambacho mleta mada amekosea ungeonekana mwerevu. Lakini kwa hivi ulivyofanya ni wazi wewe una wivu wa kike.
Hiyo 100,000/= hapo juu ndio imemleta...anataka kila mtu auze ramani kwa bei anayouza yeye, yeye yupo ofisini anasubiri wateja watakaolipia ramani laki 5 sasa kwa kuwa hapati hao wateja, akija kuona mtu anauza ramani kwa bei ya chini kuliko anayouza yeye, hapo ndipo roho inapomfurukuta.

Watu wa aina hii wapo, ni wale ambao ukiwafata ili wakusaidie na uwezo wa kukusaidia wanao, hawakusaidii hata kidogo lakini wanaumia wakiona unasaidiwa na mwingine. Hapo pia anaumia kuona watu humu wanapata elimu ya vitu mbali mbali alivyovisomea yeye darasani bila wao kukaa darasani, kwamba kwa sababu mimi niliteseka basi na wewe inabidi uteseke ili kukipata nilichonacho (binadamu hatuishi hivi)
 
Hiyo 100,000/= hapo juu ndio imemleta...anataka kila mtu auze ramani kwa bei anayouza yeye, yeye yupo ofisini anasubiri wateja watakaolipia ramani laki 5 sasa kwa kuwa hapati hao wateja, akija kuona mtu anauza ramani kwa bei ya chini kuliko anayouza yeye, hapo ndipo roho inapomfurukuta.
Watu wa aina hii wapo, ni wale ambao ukiwafata ili wakusaidie na uwezo wa kukusaidia wanao, hawakusaidii hata kidogo lakini wanaumia wakiona unasaidiwa na mwingine
Jinga sana huyu hajui kua hizi mambo ni soko huru. Hizi platforms zipo kwa ajili ya kujitangaza. Na mambo ya Ujenzi hayana unique formula moja mtu afuate hiyo hiyo.

Ye anaeuza ramani laki 5 ofisini aendelee kusubiri wateja wake. Kwani tutajuaje pengine hata yeye tukimfuata ofisini ana Google pia? Kwani ku Google ili kuangalia wengine wanafanya vipi kwa ajili ya kujifunza ni dhambi??

Soko huru halihitaji kupangiana bei, bali ni vile ambavyo mzalishaji unaona bei fulani itakulipa kulingana na malengo uliyo nayo.
 
Jinga sana huyu hajui kua hizi mambo ni soko huru. Hizi platforms zipo kwa ajili ya kujitangaza. Na mambo ya Ujenzi hayana unique formula moja mtu afuate hiyo hiyo.

Ye anaeuza ramani laki 5 ofisini aendelee kusubiri wateja wake. Kwani tutajuaje pengine hata yeye tukimfuata ofisini ana Google pia? Kwani ku Google ili kuangalia wengine wanafanya vipi kwa ajili ya kujifunza ni dhambi??

Soko huru halihitaji kupangiana bei, bali ni vile ambavyo mzalishaji unaona bei fulani itakulipa kulingana na malengo uliyo nayo.
Huyu bado hajayajua maisha vizuri, kuna muda maisha yatam-shape atabadilika

Humu ndani kuna watu wanauza ramani mpaka elfu 50 (bei ambayo mimi siwezi kuuza, sitaki kujua kama wanachora wenyewe au lah) lakini sikuwahi kumuattack mtu kwa sababu najua wote tunapambana ili maisha yaende na pia sina haki ya kumpangia mtu bei ya kuuza bidhaa yake, yeye mpaka anauza bei hiyo tayari alishafanya mahesabu yake akaona inamlipaje.

Binafsi hata mimi nimemshangaa sana, ni sawa na mtu aridhie kubeba cement mifuko 10 kwa sh 5000 halafu atokee mtu mwingine aseme usikubali kubeba hiyo mifuko kwa sh 5000, hiyo ni ndogo. Anayefanya kazi, ndiye anayejua uzito na ugumu wa hiyo kazi
 
Back
Top Bottom