Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ni vizuri ukasubiri kwanza kuta zote za msingi zikauke vizuri ndipo ujaze kifusi na kukishindilia, ukijaza kifusi kabla ukuta haujakauka vizuri itasababisha ile pressure ya udongo inayosukuma ukuta kutengeneza nyufa hasa upande wa chini ambao huwa unachelewa kukauka. Ukuta ukiwa umekauka vizuri, na pressure ya udongo ikawa kubwa, nyufa zinakimbilia sehemu ambapo fundi aliweka udongo (mortar) mnene zaidi
 
Mafundi wengi huwa wanachemka sana kwenye kuset jengo, wengine huwa wanatumia muda mrefu sana zaidi hata ya masaa sita au siku nzima kwenye kuset jengo tu. Sababu ni nini?

Katika kuset jengo, square huwa tunaitafuta katika kona moja tu, baada ya hapo hizi kamba mbili zilizotengeneza nyuzi 90 ndizo tunazitumia kama reference lines. Sasa mafundi wengi huwa wanaitafuta hiyo square ktk kona zote ambapo inapoteza muda mwingi na pia inaweza ikakupa vipimo ambavyo sio sahihi (baada ya nyumba kuisha, vyumba vinakuwa na umbo la trapeza badala ya kuwa rectangle au square) kwa sababu utakaposet square ktk kona ya pili, au ya tatu au ya nne unaweza ukaihamisha ile square ya kona ya mwanzo ambayo tayari ulishaiset (hapa sasa ndio unakuta fundi anazunguka site yote mara kumi kumi kama anafanya jogging, ujue hapo tayari kichwani kumeshachangamka na unakuta jua ni kali kweli kweli)

Ili ukimbizane na muda, inatakiwa asubuhi na mapema zoezi la kuset jengo (setting out) linaanza na baada ya masaa mawili watu wanaanza kuchimba msingi (kama muda unatosha, mnamwaga blinding siku hiyo hiyo)
 
Acceptable Height ya Opening ya Mlango ama Lintel ni how much meters?
 
No! 2.5m its not a standard height! Height of an opening(s) to lintel/beam depends on the design and function of the structure!
Hebu tupe maelekezo zaidi mtaalam
 
Acceptable Height ya Opening ya Mlango ama Lintel ni how much meters?
Mlango kama mlango kawaida huwa ni futi 7 sawa na mita 2.1 (hii ni kwa sababu average height ya watu wa karne hizi za karibuni inarange kwenye futi 5 mpaka 6 na point japo wapo wanaozidi hiyo futi 7 lakini ni nadra, kwa hivyo mlango wa futi 7 anaweza kupita mtu yoyote bila kuinamisha kichwa chake)

Kama utahitaji kuwe na vent juu ya mlango, maana yake opening/ frem ya mlango itakuwa ni futi 8 mpaka 9 au zaidi ya hapo kutegemeana na size ya vent unayohitaji kuweka.
 
Mlango kama mlango kawaida huwa ni futi 7 sawa na mita 2.1 (hii ni kwa sababu average height ya watu wa karne hizi za karibuni inarange kwenye futi 5 mpaka 6 na point japo wapo wanaozidi hiyo futi 7 lakini ni nadra, kwa hivyo mlango wa futi 7 anaweza kupita mtu yoyote bila kuinamisha kichwa chake)

Kama utahitaji kuwe na vent juu ya mlango, maana yake opening/ frem ya mlango itakuwa ni futi 8 mpaka 9 au zaidi ya hapo kutegemeana na size ya vent unayohitaji kuweka.
Hizo vents ni necessary?
 
Hizo vents ni necessary?
Yes, ukisema lintel beam ifate urefu wa mlango (mita 2.1), nyumba itakuwa fupi ambapo kati ya mkanda wa chini na mkanda wa juu utapata kama kozi 8 tu badala ya 10 (au zaidi). Labda uweke mkanda mwingine kati kati (yani kuwe na beam juu ya mlango ya kushikilia kozi moja halafu ndipo uweke mkanda wa kunzunguka nyumba nzima ambapo haitaleta muonekano mzuri kutokana na hizi heights kutofautiana kwa kiasi kikubwa pia inaongeza gharama zaidi) vinginevyo utalazimika kutengeneza mlango unaozidi hizo futi 7
 
Kabla ya kufunga gympsum board (dari) zako, chunguza kwanza paa lako kama lipo sawa (kama kuna mahali fundi alipigilia msumari nje ya mbao, ziba kwanza matundu yote) ndipo ufunge gympsum.

Uzuri ni kwamba unaweza ukachunguza paa lako katika hali yoyote (jua ama mvua). Kipindi jua linawaka, zima taa zote na pia funika pazia zote kwenye madirisha halafu anza kuangalia chumba kimoja kimoja (kama kuna mahali kuna tundu, utauona mwanga wa jua)
 
Ramani, Makadirio na Ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane +255(0)624068809
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)

Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Mawasilianao vipi, nahitaji hii ramani.
 
Baada ya kupiga plaster kuta za msingi, paka rangi nyeusi ya bituminous paint kufanya ukuta usifyonze maji na pia kuchafuka maji ya mvua yanapogonga ardhi (mawe) na kugusa kuta
 
Nikuibie tu siri mpenzi msomaji, kuna punguzo kubwa la bei za ramani msimu huu wa sikukuu na mwaka mpya, wahi sasa kabla muda wa offer haujaisha ujipatie ramani kwa bei ya punguzo
 
Back
Top Bottom