Mafundi wengi huwa wanachemka sana kwenye kuset jengo, wengine huwa wanatumia muda mrefu sana zaidi hata ya masaa sita au siku nzima kwenye kuset jengo tu. Sababu ni nini?
Katika kuset jengo, square huwa tunaitafuta katika kona moja tu, baada ya hapo hizi kamba mbili zilizotengeneza nyuzi 90 ndizo tunazitumia kama reference lines. Sasa mafundi wengi huwa wanaitafuta hiyo square ktk kona zote ambapo inapoteza muda mwingi na pia inaweza ikakupa vipimo ambavyo sio sahihi (baada ya nyumba kuisha, vyumba vinakuwa na umbo la trapeza badala ya kuwa rectangle au square) kwa sababu utakaposet square ktk kona ya pili, au ya tatu au ya nne unaweza ukaihamisha ile square ya kona ya mwanzo ambayo tayari ulishaiset (hapa sasa ndio unakuta fundi anazunguka site yote mara kumi kumi kama anafanya jogging, ujue hapo tayari kichwani kumeshachangamka na unakuta jua ni kali kweli kweli)
Ili ukimbizane na muda, inatakiwa asubuhi na mapema zoezi la kuset jengo (setting out) linaanza na baada ya masaa mawili watu wanaanza kuchimba msingi (kama muda unatosha, mnamwaga blinding siku hiyo hiyo)