Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
- #501
Katika zoezi la kuset jengo, unaweza ukatumia tofali badala ya kutumia mbao ili kupunguza gharama zisizo na ulazima
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari Mkuu,naomba ushauri ya kiwanda kipi cha hapa nyumbani kinatoa tiles nzuri..Au kampuni gani unashauri.Ukienda hardware kununua tiles, hakikisha unachukua na box zako za akiba uziweke store, zitakusaidia kufanya matengenezo miaka ya mbele.
Kumbuka hiyo design ya tiles unayonunua sasa, pengine usiione tena baada ya miaka kadhaa mbele.
Sasa ikitokea labda unataka kufanya repair ya vipande vilivyopasuka na huku ndani kwako ukiwa huna akiba itabidi uchanganye design ya tiles tofauti kitu ambacho kinaharibu muonekano mzima wa nyumba
Kama umetumia tiles za size ndogo mfano 30x30 au 40x40, weka box chache tu kwa sababu zenyewe zinakaa pc nyingi ktk box..weka store hata box 3 zinatosha
Kama umetumia tiles za size kubwa mfano 50×50 au 60x60, weka box nyingi kwa sababu zenyewe zinakaa pc chache ktk box..weka store hata box 5 mpaka 7 maana tiles za size kubwa ni rahisi zaidi kukatika tofauti na tiles za size ndogo
Kama ulisahau kuweka tiles za akiba na huko hardware zilishatoweka sokoni, tafuta tiles za rangi nyingine zenye size sawa na tiles za mwanzo kisha chagua chumba kimoja ubandue baadhi ya vipande vya tiles kisha ubandike hizi tiles zingine ulizonunua (iwe kama lile draft wanalochezaga watu na kete).
Tiles utakazokuwa umebandua katika hicho chumba, zitumie kama spare katika sehemu zingine zinazohitaji marekebisho
Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
Mtaalamu hivi hakuna madirisha mengine tofauti na aluminium..Maana naona kama kwa dar yanabana sana hewa.Ukiachana na mbao kwani ni gharama.pia pvc naonba Ushauri wako.Umeshawahi kuona dirisha la aluminium lina vitundu vidogo katika ubao wake wa chini kwa nje?
Vile vitundu watu huwa wanaviweka makusudi ili maji ya mvua yanapoingia kwenye ule mfereji wa dirisha, maji yaweze kutoka nje kupitia hivyo vitundu
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Hapa naomba ufafanuzi mkuuKatika zoezi la kuset jengo, unaweza ukatumia tofali badala ya kutumia mbao ili kupunguza gharama zisizo na ulazima
Kwa hapa nyumbani, tiles za Twyford zipo vizuri sanaHabari Mkuu,naomba ushauri ya kiwanda kipi cha hapa nyumbani kinatoa tiles nzuri..Au kampuni gani unashauri.
Kuna aina nyingine ya madirisha ambayo vioo vyake vipo kama Louver, vioo vyake vinakuwa ni vipande vipande kama slice za mikate vimebanwa na chuma pembeni ya frem za madirisha(nikipata picha nitawawekea)Mtaalamu hivi hakuna madirisha mengine tofauti na aluminium..Maana naona kama kwa dar yanabana sana hewa.Ukiachana na mbao kwani ni gharama.pia pvc naonba Ushauri wako.
Tofali za msingi huwa tunazilaza, kwa hivyo uso wa juu wa msingi unakuwa na upana wa 230mm, nyuso za tofali za boma zinakuwa na upana wa 125mm (nchi 5) au 150mm (nchi 6)Hapa naomba ufafanuzi mkuu
Asante mkuu kwa elimu, naomba kujua katika maeneo ya baridi kali kuna design naweza kufanya ili kuzua kupotea kwa joto la ndani ya nyumba hasa kipindi cha usiku? Au kuna namna gani nyingine naweza kufanya (any system installation s) ili kuingiza joto ndani ya nyumba??Katika uchanganyaji wa zege, maji hayatakiwi kuwa mengi kuzidi kipimo kinachohitajika. Kiasi cha maji kinachotakiwa ni nusu ya uzito wa kiasi cha saruji kilichotumika(water cement ratio).
Ukiweka maji mengi, kokoto zitazama chini na kufanya sehemu ya juu ya zege kusiwe na kokoto
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Asante sanaKwa hapa nyumbani, tiles za Twyford zipo vizuri sana
NashukuruKuna aina nyingine ya madirisha ambayo vioo vyake vipo kama Louver, vioo vyake vinakuwa ni vipande vipande kama slice za mikate vimebanwa na chuma pembeni ya frem za madirisha(nikipata picha nitawawekea)
Wapi naweza kupata hsti mafisadi ya louver kama kuna sehemu yanapatikana naomba muongozo.AsanteNashukuru
Hapo kwanza kuna mambo kadhaa ya kukushauri, ukiangalia vizuri hayo madirisha katika michoro ya elevation utagundua kwamba urefu kutokea kwenye floor mpaka kwenye mkanda wa juu ni mdogo (urefu wake unataka kulingana na urefu wa kuta kutokea kwenye mkanda wa juu mpaka kwenye kozi ya coping). Ili nyumba ya contemporary ipendeze, inatakiwa urefu wa kuta kutokea mkanda wa chini mpaka mkanda wa juu uwe ni mara mbili au zaidi ya urefu wa kuta kutokea mkanda wa juu mpaka juu ya coping.View attachment 2996506View attachment 2996507View attachment 2996508View attachment 2996509View attachment 2996511
Hii nyumba inaweza ikagharimu kiasi gani cha fedha za kitanzania?
LouverNashukuru