Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Hakikisha mawe yako ya mipaka ya kiwanja (beacons) unayafukia kwa zege ili watu wasiweze kufukua kirahisi na kuhamisha
Tafuta beacon ndefu za futi mbili na nusu, chini fukia urefu wa futi 2, juu itokeze urefu wa nusu futi (15cm)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika ujenzi wa kuta za boma, kuta zote za nje ni vizuri zikaumana (zikaflash) kwa nje na kuta za msingi, na kuta za ndani ni vizuri zikawa kati kati ya kuta za msingi ama mkanda

Hii itasaidia kuleta uwepesi katika zoezi la uwekaji wa rough floor ambapo zile nyuso za juu za kuta za msingi ama nyuso za mkanda zinazoonekana kwa ndani zitatumika kama timanzi ya floor

Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane
 
Ukienda hardware kununua tiles, hakikisha unachukua na box zako za akiba uziweke store, zitakusaidia kufanya matengenezo miaka ya mbele.

Kumbuka hiyo design ya tiles unayonunua sasa, pengine usiione tena baada ya miaka kadhaa mbele.

Sasa ikitokea labda unataka kufanya repair ya vipande vilivyopasuka na huku ndani kwako ukiwa huna akiba itabidi uchanganye design ya tiles tofauti kitu ambacho kinaharibu muonekano mzima wa nyumba

Kama umetumia tiles za size ndogo mfano 30x30 au 40x40, weka box chache tu kwa sababu zenyewe zinakaa pc nyingi ktk box..weka store hata box 3 zinatosha

Kama umetumia tiles za size kubwa mfano 50×50 au 60x60, weka box nyingi kwa sababu zenyewe zinakaa pc chache ktk box..weka store hata box 5 mpaka 7 maana tiles za size kubwa ni rahisi zaidi kukatika tofauti na tiles za size ndogo

Kama ulisahau kuweka tiles za akiba na huko hardware zilishatoweka sokoni, tafuta tiles za rangi nyingine zenye size sawa na tiles za mwanzo kisha chagua chumba kimoja ubandue baadhi ya vipande vya tiles kisha ubandike hizi tiles zingine ulizonunua (iwe kama lile draft wanalochezaga watu na kete).

Tiles utakazokuwa umebandua katika hicho chumba, zitumie kama spare katika sehemu zingine zinazohitaji marekebisho


Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
Habari Mkuu,naomba ushauri ya kiwanda kipi cha hapa nyumbani kinatoa tiles nzuri..Au kampuni gani unashauri.
 
Umeshawahi kuona dirisha la aluminium lina vitundu vidogo katika ubao wake wa chini kwa nje?

Vile vitundu watu huwa wanaviweka makusudi ili maji ya mvua yanapoingia kwenye ule mfereji wa dirisha, maji yaweze kutoka nje kupitia hivyo vitundu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Mtaalamu hivi hakuna madirisha mengine tofauti na aluminium..Maana naona kama kwa dar yanabana sana hewa.Ukiachana na mbao kwani ni gharama.pia pvc naonba Ushauri wako.
 
Mtaalamu hivi hakuna madirisha mengine tofauti na aluminium..Maana naona kama kwa dar yanabana sana hewa.Ukiachana na mbao kwani ni gharama.pia pvc naonba Ushauri wako.
Kuna aina nyingine ya madirisha ambayo vioo vyake vipo kama Louver, vioo vyake vinakuwa ni vipande vipande kama slice za mikate vimebanwa na chuma pembeni ya frem za madirisha(nikipata picha nitawawekea)
 
Hapa naomba ufafanuzi mkuu
Tofali za msingi huwa tunazilaza, kwa hivyo uso wa juu wa msingi unakuwa na upana wa 230mm, nyuso za tofali za boma zinakuwa na upana wa 125mm (nchi 5) au 150mm (nchi 6)

Ukisimamisha tofali kati kati, juu ya ukuta wa msingi maana yake nyuso za kuta za msingi bado zitakuwa zinaonekana kushoto na kulia mwa kuta za boma ( itakuwa ni (230mm-150mm)÷2=40mm kama utatumia tofali za nchi 6 katika boma au 52.5mm kama utatumia tofali za nchi 5)

Hizo 40mm au 52.5mm ya kuta za msingi zinazoonekana ndio zinatumika kama level (timanzi) ya floor wakati unamwaga zege la floor katika vyumba
 
Kumekuwa na matukio mbali mbali ya slab za makaro ya vyoo/visima kushuka/kuporomoka baada ya muda flani.
Ukiona slab ya karo/kisima imeshatengeneza kitu kama sahani kati kati, basi ujue hapo slab yako imeundergo deflection na inaweza ikashuka muda wowote.

Kutokana na ufinyu/udogo wa eneo, watu wengi huwa wanaweka mabanda ya mifugo au parking ya magari juu ya haya makaro kitu ambacho ni hatari kama slab itakuwa ipo katika risk ya kushuka

1. Unene wa zege la slab hautakiwi kuwa mkubwa sana kwa sababu unene unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo uzito wa slab unavyozidi kuongezeka. Unene wa nchi 5 mpaka 6 unatosha, sasa wengine slab wanaweka mpaka nchi 8

2. Nafasi kati ya nondo na nondo (spacing) isiwe kubwa sana. Weka spacing ya 15cm mpaka 20cm tu, mafundi wengine wanaweka spacing mpaka 30cm ili wabaki na pesa nyingine ya nondo wagawane (hivi vitu kama huna ujuzi navyo, mafundi wanaweza wakawa wanavifanya mbele yako huku wewe mwenyewe unaona)

3. Usiweke mfuniko wa karo kati kati ya slab kwa sababu kati kati ya slab ndipo maximum deflection ya slab hutokea, hivyo nondo hazitakiwi kukatwa ili kuacha huo uwazi wa mfuniko, uwazi wa mfuniko wa karo weka pembeni kabisa


Ili kuepuka hiyo hali, ni vizuri ukaweka cross beams ambapo utakuwa salama zaidi

Mfano kama karo lako ni la duara, mkanda mmoja unajenga kutokea kaskazini kwenda kusini na mkanda mwingine unajenga kutokea mashariki kwenda magharibi ambapo zinakuja kukutana kati kati kutengeneza alama ya jumlisha (+). Hizi ndio tunaita cross beams, ambapo slab inakuja kulala juu yake

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Moja ya factors zinazochangia kuongezeka kwa idadi ya bati katika upauaji ni pamoja na mlalo wa paa (roof pitch)

Ramani inaweza ikawa ni moja, lakini kwenye upauaji idadi ya bati zikatofautiana kutokana na roof pitch kuwa tofauti

Mlalo wa paa kwa maeneo ambayo hayana mabarafu (snow) kama Tanźania unatakiwa uwe kati ya 30 mpaka 45 kutegemeana na ukubwa (span) wa jengo

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Huwa tunaanza kumwaga mchanga kabla ya kulaza tofali za msingi ili kutengeneza tabaka (layer) kati ya udongo na tofali lakini pia inaleta urahisi katika zoezi la kuset tofali (kulikandamiza tofali katika mchanga ili likae level ni rahisi kuliko kulikandamiza kwenye udongo)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika uchanganyaji wa zege, maji hayatakiwi kuwa mengi kuzidi kipimo kinachohitajika. Kiasi cha maji kinachotakiwa ni nusu ya uzito wa kiasi cha saruji kilichotumika(water cement ratio).
Ukiweka maji mengi, kokoto zitazama chini na kufanya sehemu ya juu ya zege kusiwe na kokoto

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika uchanganyaji wa zege, maji hayatakiwi kuwa mengi kuzidi kipimo kinachohitajika. Kiasi cha maji kinachotakiwa ni nusu ya uzito wa kiasi cha saruji kilichotumika(water cement ratio).
Ukiweka maji mengi, kokoto zitazama chini na kufanya sehemu ya juu ya zege kusiwe na kokoto

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Asante mkuu kwa elimu, naomba kujua katika maeneo ya baridi kali kuna design naweza kufanya ili kuzua kupotea kwa joto la ndani ya nyumba hasa kipindi cha usiku? Au kuna namna gani nyingine naweza kufanya (any system installation s) ili kuingiza joto ndani ya nyumba??
 
Hapo kwanza kuna mambo kadhaa ya kukushauri, ukiangalia vizuri hayo madirisha katika michoro ya elevation utagundua kwamba urefu kutokea kwenye floor mpaka kwenye mkanda wa juu ni mdogo (urefu wake unataka kulingana na urefu wa kuta kutokea kwenye mkanda wa juu mpaka kwenye kozi ya coping). Ili nyumba ya contemporary ipendeze, inatakiwa urefu wa kuta kutokea mkanda wa chini mpaka mkanda wa juu uwe ni mara mbili au zaidi ya urefu wa kuta kutokea mkanda wa juu mpaka juu ya coping.

Nyumba za contemporary zinatakiwa ziwe na urefu wa kutosha kutokea kwenye floor mpaka kwenye mkanda wa juu (angalau kuwe na kozi 12). Na pia jitahidi kuta za juu ya mkanda zisizidi kozi 6

Kumbuka hizi nyumba bati zake huwa zinakuwa chini sana kwa hivyo itabidi nyumba iinuke juu zaidi ili kupatikane nafasi ya kutosha kati ya dari na bati vinginevyo mchana ndani patakuwa hapakaliki kutokana na joto kali

Tuwasiliane ndg nikuandalie makadirio ya material yote kuanzia msingi mpaka finishing stepwise
 
Nashukuru
Louver
20240522_231319.jpg
 
Mkuu naomba kufahamu yafatayo;
1. Unapoweka Jamvi unakuwa huna haja ya kuweka mkanda?
2. Kipi naweza kuskip katika namna ya kupunguza gharama lakini nikawa nimelinda ubora ktk haya;
a/kuweka Jamvi
b/ kuweka mkanda
c/ kuweka lenta 2, nikaweka moja tu ile ya juu.
 
Back
Top Bottom