Ramani ya Maandamano ya CDM; NI Njia ya mauti au Ulemavu M/kiti Kashawapa

Ramani ya Maandamano ya CDM; NI Njia ya mauti au Ulemavu M/kiti Kashawapa

Ukichaa unawapata hata watu usio weza kudhani wana vimelea vyovyote vya ugonjwa huo. Naona maslahi yanapo guswa kila mtu uwehu unampanda kichwani.
Je unaanzia wapi MAANDAMANO? Jukwaa la Siasa kupitia Habari Mchanganyiko na kuishia InternationalNews? Au Jamii Intelligence?
 
Niwaombe wadau wote wenye uzoefu wa gharama za kutibu majeraha yatokanayo na vurugu na vipigo mbalimbali.

1-Kupasuliwa fuvu.....200,000/=
2-Kuvunjwa taya na gongo la kipolisi....100,000(kianzio)
3-Kupasuliwa bandama....200,000/=
4-Kutovugwa ini,kongosho,figo....150,000 halafu dialysis 150,000 kwa wiki
5-Kuvunjwa senta bolt ya kiuno...25000 kianzio
6-Kutobolewa jicho moja....50,000 kianzio
7-Kung'olewa jino....5000
8-Kupasuliwa yai za kende....50,000
9-Kupasuliwa chembe ya moyo...
10-Kuvunjika shingo...
11-Kuteguliwa uti wa mgongo....
12-Kupasuliwa ngoma ya sikio kwa mbata...5000 ya file
13-Kupasuliwa taya na kitako cha bunduki...20,000
14-kutapishwa kisusio...5000
15-Kutoneshwa busha/mshipa...bure
16-Kugeuzwa kisahani cha goti...150,000
17-kutoneshwa /kupasuliwa tezi dume bure
18-Kutobolewa kibofu au puru(rectum) 200,000 kianzio
19-Kuzikwa na manispaa...bure
20-Vipimo vya Xray,CT scan,Ultra sound,MRI, 250,000.

N.B BEI NILIZOWEKA SIO HALISI

hebu tuongeze nyingine na kuweka gharama zake..
Tahadhari hii imezingatiwa
 
Yale siyo maandamano bali kusanyiko la wasio na malengo wakimsindikiza Mbowe
Basi sawa.
Mimi naona kama maandamano yamefana sana na mama toka sasa kwenda mbele anajuwa hana njia ya kuyarudisha nyuma tena.
Haya yamefikia yalipo ishia, tugange yajayo.
 
Basi sawa.
Mimi naona kama maandamano yamefana sana na mama toka sasa kwenda mbele anajuwa hana njia ya kuyarudisha nyuma tena.
Haya yamefikia yalipo ishia, tugange yajayo.
Hakuna kilichofana kwenye maandamano kwa kuwa watu hawajawaunga mkono. Kwani ndugu unaandika tokea wapi? Minjingu au Nangurukulu?
 
Ndugu Mbowe, ambaye anahamasisha maandamano haya, ana watoto lakini hajawahi hata siku moja kuwaweka mbele kwenye harakati hizi.

Kwa nini nyinyi mufanye hivyo? Vijana, kumbukeni kuwa Tanzania yetu ni nchi moja tu, na hatuna nyingine. Maandamano haya hayatatufaidisha, bali yataharibu taswira nzuri ya nchi yetu.
Tuchukue jukumu la kuyapinga kwa nguvu zetu zote, na tuachane na wanasiasa wachache wanaotaka kutuweka bize na maandamano ili wafurahishe mabosi wao huko nje, kama vile Ujerumani, kwa malengo yao binafsi.
Hii nchi qmmke imelaaniwa sio bure, taswira nzuri watu kutekwa na kuuawa?? Tena na Polisi??
Wallah tutawaliwe tena tu!
 
Hakuna kilichofana kwenye maandamano kwa kuwa watu hawajawaunga mkono. Kwani ndugu unaandika tokea wapi? Minjingu au Nangurukulu?
Sasa hili nalo unataka tupoteze muda humu kulijadili; kama watu wameunga mkono maandamano au hapana?
Mkuu 'Stuxnet', nakupa hadhi kuliko wengi humu kwa kujuwa unao ufahamu wa kutosha. Lakini unapokuja na kusema watu hawakuunga mkono maandamano, inanishangaza sana.
Kwako kuunga mkono ni lazima watu wakapambane na polisi siyo?

Kwa hiyo tuseme hapa kwamba kutojitokeza watu kuunga mkono maandamano maana yake ni watu hao kuunga mkono maovu yanayofanywa na uongozi dhidi ya watu hao hao? Hii ni akili ya wapi?
 
Ule ulikuwa usanii tu. Polisi na Mbowe wanajuwa walichofanya. Yaani mtuhumiwa wa Polisi kweli apande kiti cha mbele cha Difenda??
 
Ule ulikuwa usanii tu. Polisi na Mbowe wanajuwa walichofanya. Yaani mtuhumiwa wa Polisi kweli apande kiti cha mbele cha Difenda??
Unayo picha mkuu?

Lakini , pamoja na lawama nyingi wanazo elekezwa polisi, hasa hawa wa vyeo vya chini, kumbuka kuwa mbali ya upolisi wao na wao ni waTanzania, raia wa nchi hii wanaojua uovu unao fanyika. Hawa wengi hawana tatizo lolote na huo uhasama unao elekezwa kwa viongozi wa Chadema.
Kwa hiyo ninakushangaa wewe kutaka kuja hapa na ulaghai hafifu namna hiyo.
 
Back
Top Bottom