DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Ok sawa,Mkuu sibishani na wewe. Rasimu ya Warioba ninayo na imejadiliwa sana wakati wa Bunge la Katiba. Kuchangia hapa ni mawazo tofauti na yalokuwepo huko. Nisome toka mwanzo wa mada hii upate wewe kunielewa.
Rasimu ya Warioba inapendekeza serikali 3 na ndio kisa cha bunge kuvunjika. Hata mimi sikubaliani nayo! Sasa unataka mpaka niiweke rasimu hapa ndio utaweza kuchangia ?
Baraza la wazee kwa mtazamo wangu sio lazima liwe na mwakilishi wa kila wilaya kwa sababu ya ukubwa wake. Wapo wazee wenye sifa, ama kutokana na utumishi wao sehemu mbalimbali, au kutokana na uwezo wao wa kiuongozi katika mahala husika.Hilo Baraza la wazee ambalo umeliita Senate mbona lita ongeza gharama kwa umma hasa kwenye matumizi ya kodi kulipa mishahara, posho nk mbona unataka kumpa mwananchi mzigo wa Kodi na wakati huo huo ukisema uendeshaji wa serikali 3 utakuwa na gharama ?
Yapi yatakuwa manufaa ya Baraza hilo katika taifa ukizingatia tuna Bunge na Baraza la mawaziri ?
Njia yoyote ile itumike muhimu wawe watu wenye misimamo ya katika kusimamia na kuilinda UTAWALA BORA.Baraza la wazee kwa mtazamo wangu sio lazima liwe na mwakilishi wa kila wilaya kwa sababu ya ukubwa wake. Wapo wazee wenye sifa, ama kutokana na utumishi wao sehemu mbalimbali, au kutokana na uwezo wao wa kiuongozi katika mahala husika.
Kuwa na double check sio kitu kibaya. Umuhimu wake uwe kuangalia na gharama za uendeshaji wa hilo baraza pia
Ni kweli kabisa. Kwa sasa hatuna pakuwawajibisha maana kuna loopholes nyingi. Balance and check is critical for good governance.Njia yoyote ile itumike muhimu wawe watu wenye misimamo ya katika kusimamia na kuilinda UTAWALA BORA.
Hatuwezi kuijenga nchi yetu kwa kutegemea viongozi ambao hawawajibiki na hakuna chombo kinacho watazama kwa makini mienendo yao.
Malalamiko mengi ya Wananchi ni tabia na matendo ya baadhi viongozi ambao wakisha pewa dhamana hujiona hakuna mtu wa kuwagusa hata kama wameitia hasara Serikali katika kusaini mikataba mibovu, dhulma za ardhi, mali zao zihakikiwe kama wanavyodai. Kifupi, Miiko na Maadili ya viongozi yawe na chombo kitakacho wawajibisha.
Nakubaliana na wewe kwenye teuzi za rais kwa hawa Wakurugenzi wa taasisi na mashirika ya Umma. Badala ya teuzi wafanyiwe interview na boards aidha kupitia wizara inayohusika.Miradi ya maendeleo katika mkoa kuwepo sio sababu ya wakuu wa mikoa waliochaguliwa na wananchi wasiisimamie simply because hawakuchaguliwa na Rais!! Aferall usimamizi wa miradi ya maendeleo ni kazi ya watendaji, unfortunately our civil servants who are supposed to be apolitical serving any party in power have been politicized by ccm; kiasi kwamba watendaji hao ni wanachama wa vyama vya siasa! Watendaji wote wa civil service wizarani na mikoani WOTE wawe apolitical.
Kwanini Mkurugenzi awe mteule wa Rais badala ya kuwa part of the civil service; yote hii ilikuwa ni kuhodhi madaraka kwa mtu mmoja and in the process tunazalisha CHAWA ambao hawaleti maendeleo bali wizi!! Miradi ya Serikali kuu na miradi ya Halmashsuri yote inatumia fedha za wananchi sioni sababu kwani usimamizi wake uwe tofauti ; hii yote ni kuongeza gharama za usimamizi na kuongeza nafasi za matumizi mabaya ya fedha!
Baraza la Senate linaweza kua na ufanisi tu pale upatikanaji wa hao Senators utakuwa kwa utashi wa wananchi kwa kuwachagua bila mizengwe ya vyama vya siasa.
Katiba ilenge kupunguza madaraka ya Rais ambae hivi sasa ni omnipotent; moja sapo ni hilo la kuteua Regional na District commissioners!! Msiwe kwenye hiyo kamati kutetea status quo!!! Nchi hii imaeharibiwa sana na current arrangements.
Nakubaliana na wewe kwenye teuzi za rais kwa hawa Wakurugenzi wa taasisi na mashirika ya Umma. Badala ya teuzi wafanyiwe interview na boards aidha kupitia wizara inayohusika.
Lakini tatizo la Tanzania mkuu wangu ni michongo. Ukiwapa watu madaraka wanachonga mzinga! Watapeana ajira wenyewe ili mchongo usimame. Yaani Tanzania ni pasua kichwa, rahisi sana kusema tumpunguzie rais madaraka lkn hayo.madaraka ulompunguzia unampa nani?
Atakaye pewa atafanya mabaya zaidi. Elewa hoja sii kuwa na nguvu kubwa bali Uwajibikaji.
Leo wanao ongoza ufisadi ni Wakurugenzi. Watu wenye elimu na kila sifa ya ufanyaji kazi lakini mzigo! Nani wa kuwasimamia?
Ukisema Mkuu wa Mkoa asiteuliwe na rais tueleze sababu isiwe tu unataka kumpunguzia madaraka lakini hakuna impact katika ufanisi wa kazi.
Isitoshe hawa ni reflection yetu sisi sote. Mtu akiwa bench ni mpole, mtu wa watu, siku anateuliwa sii yule tena utadhani kakabidhiwa rungu.
Mwisho niseme tu, rais anapounda serikali yake, huteua watu ambao wataifanya kazi kwa niaba yake. Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni sehemu ya idara zake.
Kwanza kabisa niombe samahani kama nimekukwaza wewe na wengine wote mnaoipitisha Rasimu ya Warioba bila kuzingatia kuwa ni Rasimu hiyo hiyo ilotukwamisha kuipata Katiba Mpya.Naomba kutoa tu tahadhari kuhusu huu mjadala ulioanzishwa na anayeitwa Mkandara.
Mkandara anaibeza rasimu ya Warioba akidai ilizingatia maoni ya baadhi tu ya wananchi na si wote. (Milioni 60!)
Hivi Mkandara atatumia njia gani kuwafikia hao wananchi wote anaodai hawakupata fursa ya kutoa maoni?
Swali la pili anamwakilisha nani katika hii harakati ya kuiponda rasimu ya Warioba na kupinga baadhi ya maoni yaliyomo?
Swali la tatu anabeza rasimu ya Warioba kwa niaba ya nani? Kama ni kikosi kazi nanusa harufu isiyo na afya hapa!
Hiki kikosi ambacho kinatumbua mabilioni ya kodi zetu, kiliteuliwa na mpiga zumari au kilichaguliwa na wananchi?
Tuwe makini sana na hizi ghilba za CCM, hiki kikosi hakina tofauti na kamati yoyote ile ya CCM. Eti rasimu ya Warioba haifai!
Shida ilikuwa ya maccm. Kimsingi ile rasimu ya Warioba ilikuwa njema sana.. shida ni kwamba ilihatarisha maslahi ya genge la wahalifu eachache liitwalo ccm. Baasi. Leo hii tungekuwa mbali sanaRasimu ya Warioba ipo, wewe kama mwananchi una mawqzo gani tofauti katika mapwndekezo ya sura ibara zike. Kumbuka sisi wote tuna mitazamo tofauti na hatukubaliani kwa mengi na ndio maana rasimu ile ilisukumwa uvunguni. Je, leo hii tutawezaje kupata suluhu katika Mambo yale yale yalokwama mwanzoni pasipo hata kuwafikia Wananchi.
Unapo zungumzia Muundo una maana ya Muungano wenyewe au Serikali ngapi? Maana elewa Tanzania ni nchi ndogo ukilinganisha na nchi zingine kwa maana ya Ukubwa wake na watu wake.Asante ndugu Mkandara..
Mosi: tufahamu kuwa nchi yetu haina maendeleo kutokana na kukosa falsafa sahihi ya uongozi au kukosa uongozi kabisa.
Pili: Hoja yangu iko kwenye MUUNDO WA SERIKALI.
Muundo uliopo una mapungufu makubwa sana. Ni muundo usio tofauti na wa kikoloni ambapo muundo huo ulihakikisha maslahi ya mkoloni yanalindwa na si ya mwananchi. Hali kadhalika, muundo uliopo ni wa kuhakikisha maslahi ya serikali ndiyo yanalindwa. Ukiangalia vema, utakuta ofisi ya raisi inawakilishwa hadi ngazi ya chini kabisa kwenye kitongoji/mtaa.
Ningetamani kwenye katiba mpya, maslahi ya mwananchi yapewe heshima na nafasi inayostahili. Iko hivi:
Mwananchi aongozwe na mtu aliyemchagua. Maana yake, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi hawatakiwi tena kwenye katiba/sheria zitakazotungwa kutokana na katiba mpya.
Uongozi wa mikoa uchaguliwe na wananchi, kuwe na mabunge kila mkoa. Kila mkoa uwe na taasisi kamili zenye uwezo stahiki mfano elimu, mahakama, ardhi, kilimo, afya, maji, nishati, polisi nk.
Wabunge wa wananchi katika mikoa wawe kweli wamechaguliwa kihalali.
Nguvu ya ofisi ya Rais iishie kwenye wizara.. mfano sasa hivi raisi anateua viongozi wapatao elfu tatu au zaidi, hii siyo sahihi hata kidogo, ndo maana machawa wameongezeka.
Bunge la jamhuri lipunguziwe nguvu na ukuwa, pia lijikite katika masuala ya msingi kama kusimamia serikali kuu na masuala ya kimataifa. Yaliyobaki yatashughulikiwa na mabunge madogo ya mikoa.
Nitarudi tena, asante
Baadhi ya Malengo;Nikuulize, Unapotaka kuunda Majimbo nini haswa malengo yake? Tutafadikaje na majimbo hayo na zipi hasara zake!
- Kuwe na mambo ya Kitaifa na mambo ya Kimajimbo. Watumishi watawajibika kwa wasimamizi wao. Ajira zao, Mishahara yao itatoka sehemu waliyo ajiliwa. Mfano mwalimu wa shule ya msingi A katika Jimbo A, atawajibika kwa Mwalimu mkuu wa shule hiyo, na kulipwa na Jimbo A. Mhasibu wa TCRA tawi la Jimbo A, atawajibika kwa Mhasibu-mkuu, makao makuu ya TCRA, na atalipwa mshahara kutoka serikali kuu.Kama ikiwa nia ni Majimbo yajitegemee kiuchumi ina maana watumishi watakuwa answerable kwa kiongozi wao. Share ya mapato ya kodi itafanyikaje?
Lengo liwe kutotegemea misaada, huku tukiwa na nchi Tajiri kabisa. Hata hivyo, misaada huja kwa lengo fulani.Misaada ya maendeleo itafantikaje?
Itengenezwe miongozo ya kifedha itakayo hakikisha ubadhilifu unazuiwa kabla haujatokea, na Ukitokea miongozo irekebishwa kuhakikisha hautatokea tena.Pia kama lengo lake ni kugawana madaraka, fikiria ikiwa leo Serikali za mitaa zinaongoza kwa ubadhilifu wa fedha za miradi, itakuwaje tukiwa na Majimbo ambayo rais hana mamlaka nayo?
Kama zamani miakanya 70 tulishindwa Madaraka mikoani ikawa shida mkulima kusafirisha mazao toka mkoa mmoja kwenda mwingine. Tukavunja mfumo ule, tumeleta Serikali za mitaa, nazo tumeshudia wananchi wakilalamikia tozo na ushuru. kwa nini turudie makosa? Kwa nini tusiandike Katiba inayo wajali Wananchi kuondoa urasimu huo?
Binafsi yangu naamini Majimbo yanaweza tokea Nigeria. Mifano ipo mingi kwa nchi za Kiafrika kugawanyika.kutokana na Majimbo. Kuanzia Ethiopia, Sudan, Somalia kote huko majimbo yameandamana na Ukabila. Kenya ni swala la muda tu.
Sisi tumeweza kufuta Ukabila na Udini kwa nini unataka mfumo ambao unaweza kurudisha hali ya hatari kwa usalama wa raia? Kama ya Zanzibar yanatushinda tunataka serikali 3 ili.kila.mtu na chake tutawezaje Majimbo?
Muungano wa Serikali 3 utawatenganisha WATU wa Tanganyika na Zanzibar. Hilo.nakuhakkkishia hata kabla halijapitishwa.
Kumbuka lengo halisi la Muungano wa nchi zetu ilikuwa Kuunganisha WATU wake. Kama tutaunda Serikali 3 ina maana tumekubali kila nchi ibebe msalaba wake. Hapo ndio utawasikia Watanganyika nao wakidai Wazanzibar warudi kwao! Hawa Wazazibar wanafuata nini, nao kule Wabara rudini makwenu. Trust me itatokea wala sii swala la kupigia ramli..
Wenzetu Ulaya, wameweza kabisa kuondoa Ukabila na Ukanda. Mwananchi mkazi wa NewYork au Texas regardless ya race au uzawa wote ni WAMAREKANI na kujitambulisha kama Wamarekani. (Am American) muulize unatoka wapi atasema USA.
Angalia UK kinachiwakeka pamoja ni nguvu ya dola tu lakini Wana ubaguzi ndani ya nchi zao na kuna under ground movements kudai kujigawa.
Na Sisi itakuwa hivyo hivyo, mimi Mtanganyika, mimi Mzanzibar maana tayari dalili zipo wazi machoni mwetu lakini hatutaki kuamini. Nakuhakikishia jina la Tanzania litapotea kabisa kama Tanganyika.
Nia na dhumuni la Katiba hii iwe kuutujenga katika UTANZANIA tuwe proud na nchi yetu badala ta kuchukia kuwa kuitwa Mtanzania.
Ni rahisi sana kusema unapounda.majimbo unataka.kuwasogegezea karibu Wananchi huduma lakini kuna huduma zilokaribu na Wananchi kuliko Serikali za Mitaa?Baadhi ya Malengo;
1 - ni kusogeza uwajibikaji wenye maana karibu zaidi kwa Wenye-nchi (Wananchi).
2 - kutenganisha majukumu, mipango ya maendeleo na utekelezaji wake, etc ya Kitaifa (yanayohusi Taifa zima) na ya kijimbo (Yanayohusu au Yaliyo na maana katika Jimbo)
3 - Kusaidia kupunguza mzigo mkubwa wa majukumu aliyonayo Raisi, kutoka majukumu ya sasa yanayohitaji Raisi mwenye uwezo wa "kiMungu" ili kutelekezeka ipasavyo, kwenda majukumu yanayoweza kutekelezeka na Bin-Adamu mwenye uwezo wa wastani na kuendelea.
4 - Kusaidia kupunguza madhala ya makosa yanayofanywa na viongozi wa Kitaifa ( na hata yatakayokua yanafanywa na viiongozi wa Kimajimbo.
5 - Kuipa Serikali ya Kitaifa/Kuu (Kwa kushirikiana na Serikali za Majimbo) wajibu na nafasi ya kutunga, kusimamia na kurekebisha Miongozo mbalimbali, ambayo itatumika kama Mahitaji ya kima cha chini katika upangaji na utekeleza wa shughuli za maendeleo nchi nzima.
6. N.K
- Kuwe na mambo ya Kitaifa na mambo ya Kimajimbo. Watumishi watawajibika kwa wasimamizi wao. Ajira zao, Mishahara yao itatoka sehemu waliyo ajiliwa. Mfano mwalimu wa shule ya msingi A katika Jimbo A, atawajibika kwa Mwalimu mkuu wa shule hiyo, na kulipwa na Jimbo A. Mhasibu wa TCRA tawi la Jimbo A, atawajibika kwa Mhasibu-mkuu, makao makuu ya TCRA, na atalipwa mshahara kutoka serikali kuu.
- Mapato katika Majimbo yagawanywe, ili kiasi kibaki katika Jimbo na Kiasi kiende Serikali kuu.
Leo liwe kutotegemea misaada, huku tukiwa na nchi Tajiri kabisa. Hata hivyo, misaada huja kwa lengo fulani.
Misaada itumike kutegemea malengo ya misaada hiyo.
Itengenezwe miongozo ya kifedha itakayo hakikisha ubadhilifu unazuiwa kabla haujatokea, na Ukitokea miongozo irekebishwa kuhakikisha hautatokea tena.
- Naamini, mfumo wa Majimbo hautakosa changamoto. Lakini faida zake zinahalisha, uthubutu wa kujikita katika kutatua changamoto hizo.
- Tanganyika ina historia yake. Mfumo wetu wa Majimbo, utakone na hali, historia na mahitaji yetu.
Naona umegusia maeneo kadhaa. Sidhani kama nina majibu yote, hata hivyo nijaribu kuelezea kidogo.Hili nalo ni swala zito sana maana leo hii tupo mil 60 utamilikishaje ardhi ambayo tuseme kuna watu wana eka mil moja ya shamba wakati mwingine hana hata nusu eka? Je unahitaji ardhi kwa sababu gani? Kama nyumba unaweza kununua ya ghorofani sio lazima iwe ardhi yako!
Kama kilimo huoni hatari ya wataondoshwa wakulima wadogo wadogo katika maeneo yao na kuzaa Wakulima matajiri ambao watauziwa ardhi hizo kutokana na tamaa ya kutokana na Umaskini wa wakulima mfano wa Kariakoo ilivyouzwa kwa matajiri?
n
Je, wafugaji wenye mifugo utawapa eka ngapi. Transpassing utazizuia vipi mtu akikatiaha shambani kwako? Najaribu kujenga hoja hapa kusikia majibu yako..
Mikoa na Wilaya, kwa maoni yangu ni majimbo yanayofuata mfumo wa utawala wa kati (Central governance) ambayo ndio chanzo cha Tatizo.Ni rahisi sana kusema unapounda.majimbo unataka.kuwasogegezea karibu Wananchi huduma lakini kuna huduma zilokaribu na Wananchi kuliko Serikali za Mitaa?
Kumbuka tu kwamba hakuna kubwa.ambalo Seeikali ya Majimbo.itafanya dhidi ya Serikali Kuu kuliko serikali za mitaa ambazo zina ukubwa mdogo na kata chache zaidi lakini ndiko Ubadhilifu mkubwa unatokea.
Now, imagine unaongeza wigo kuwa na Majimbo mathlan Shinyanga, Mwanza, Geifa, Mara na Bukoba! Halafu uunde serikali yake na Bunge lake! Patakuwa na wabunge wa jimbo hilo pia Wabunge wawakilishi Bunge la JMT. Fedha hizi za matumizi haya makubwa zitatoka wapi?
Ikiwa.mimi napingana na Seeikali 3, halafu unanambia acha 3 tuunde Majimbo ina maana unaunda Seeikaki Isopungua 6 zenye viongozi na Wabunge wake kisha bado wa Kitaifa!
Kwani Mikoa na Wilaya zina kasoro zipi? Bila shaka ni UTUMISHI yaani hakuna UWAJIBIKAJI. Kama haya yanakosekana na WATU ni walle wale tulonao huoni kwamba tatizo ni WATU sio UTAWALA?
Sisi watumishi ndio tatizo hata kama.tutagawa nyumba kwa nyumba shida zitabakia palepale. Tatizo ni TAASISI zeru haziwajibiki. La kufanya ni.kutafuta mbinu ziwajibike. Kila mmoja wetu aogope kuiibia serikali. Na ndivyo wenzetu waliweza kufanikiwa kwa sababu kila mtumishi ana wajibu na nishani ya kazi.
- Sisi ni Kanyaga Twende, tumechelewa mno..
Sio kweli kabisa maneno haya ni ya Wanasiasa, uhasama.baina ya Watu wa Bara na Visiwani umetokana na Siasa za maji taka nitakwambia kwa nini.
- Hata sasa kuna huo mgawanyo, kuna Wanzanzibar na (so-called) Watanzania Bara. Muungano wa serikali 3 utafasema, huyu Mtanzania Bara, ni Mtaganyika (pamoja na mambo mengine) - ni Muungano usio na unafiki.
- Nafikiri, Watu wenye nia ya kuungana, wakiungana ni jambo zuri. Hatahivyo, Sidhani kama ni sahihi kuwalazimisha watu waungane.
- Ni wazi kuwa Wazanzibar hawataki Tanganyika na Zanzibar ziungane kwa nchi moja (niko tayari kukosolewa kwa hili). Muungano tulionao sasa, hauitendei haki Tanganyika, ukiachana na mapungufu mengine, na ndio maana kunapendekezo la serilkali 3.
Mkuu hata hizi serikali za Majimbo zina viongozi wa Serikali Kuu ndani wakishughulika na mambo ya Jamhuri (federal) Ujue unapounda Majimbo kuna mambo mtafanya ya Serikali Kuu na mengine yataendeshwa na Serikali za Majimbo ni sawa kabisa na Muungano Wa Tanganyika na Zanzibar.Mikoa na Wilaya, kwa maoni yangu ni majimbo yanayofuata mfumo wa utawala wa kati (Central governance) ambayo ndio chanzo cha Tatizo.