RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Yaani baba lizy atawale vipindi vitatu?! Hadi 2020 hii Katiba italeta machafuko tanganyika!! Lazima tupinge kipengere hicho
 
Hapo umeneno wana assume kama vile hakutakuwa na mgombea binafsi asiyekuwa na chama huyo nani atamrithi, au watatakiwa kuacha wasia wa nani atarithi kiti chake, hili jambo ni la ovyoo, demicrasia lazima iheshimiwe, watu wachague viongozi hii nchi democrasia ndo inakua hata kupiga tu kura watu bado hawajitokezi kuache kuweka vichocheo vya kukuza voter apathy nchini ni kosa kubwa! Akifa/akijihudhuru au kwa namna yoyote nafasi ya kuchaguliwa yoyote ikibaki wazi lazima uchaguzi ufanyike, hii ndo gharama ya democracy!

hawaja assume bwana mbona warioba ametamka wazi kuwa endapo mgomea binafsi amefariki basi uchaguzi utarudiwa
 
Yaani baba lizy atawale vipindi vitatu?! Hadi 2020 hii Katiba italeta machafuko tanganyika!! Lazima tupinge kipengere hicho
urais hawajasena vipindi vingapi ila kwa upande wa ubunge ndo kunaukomo wa vipindi 3
 
''kiwango cha kura mtu kuchaguliwa kuwa rais............kwa sasa ni mtu kuwa na kura nyingi
tume inapendekeza mgombea lazima apate asilimia zaidi ya 50''....Hapa ni PATAMU sana!

Usisahau CCM mara zote inashinda ushindi wa kishindo 60%+ so kwa CCM 50% ni kama kumukuma mlevi
 
Tunaomba watuwekee hiyo rasimu online. Au kama kuna mtu anayo soft copy atumwagie hapa

Tume hii pesa yetu yote walokula .... HAWANA soft copy ya kutuwekea hapa..... SHAME ON THEM.....
 
mwenye hii thread anyang'anywe ianzishwe nyingine... mods please facilitate this... aliyeanzisha thread hajui ku update mambo.... ama mods msaidieni
 
Wadau leo ndio rasimu ya katiba mpya Inazinduliwa Karimjee .Uzinduzi huo unatarajiwa kurushwa na vituo vya TBC1, TBC Taifa, ITV, Star TV, Channel Ten, ZBC TV na ZBC, kuanzia sasa.Kila anaeweza na afuatilie.Hata hivyo ni vizuri kila mtu angetoa maoni yake ikiwa ni kitu gani ambacho akiona kimewekwa humo angefurahi sana na ni kitu gani ambacho kikiachwa atasikitika sana.

Nawasilisha!

ahaa

Kweli JF chiBOooooKO!!, yaani watu wanaandalia TV na kutoa maoni kwenye JF?

There are currently 2045 users browsing this thread. (267 members and 1778 guests)
 
Hii rasimu imeandaliwa kwa jicho la uchaguzi wa 2015. Bado haijaangalia kwa undani matatizo ya msingi ya muda mrefu ya wananchi.Taasisi muhimu za kutoa haki hazijaguswa(kiutendaji na kiwajibikaji).'Conduct' za 'members' wa hizi Taasisi bado utata.Masuala ya rasilimali,ardhi,maliasili,uraia nayo utata. Hii rasimu imetengenezwa kukipa Chama cha mapinduzi (CCM )
'fake Political Bonhomie' machoni kwa wananchi..
 
This is another useless paper...
Huwezi kupendekeza serikali tatu, alafu ukajiamulia kutengeneza katiba ya serikali moja tu kati ya hizo!!! Ni upuuzi...
Mkuu Tuko hii ni rasimu ambayo itajadiliwa na makundi ambayo yameanishwa kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba.

Kumbuka kuna mabadiliko tena yatafanyika kulingana na jinsi vikundi/makundi yatakavyo pendekeza ambapo bunge la katiba ndilo litakalo pitisha hii sheria mama.

Mpaka sasa hatujajua na wajumbe wa tume hawajajua kwa uhakika ni serikali ngapi zitakuwepo, kwa maana hiyo, huwezi kuanza kutafuta katiba kwa serikali ambazo hazipo na hazijulikani kama zitakuwepo. Kufanya hivyo, ni kujichukulia madaraka ya kidikteta na kuonyesha haya siyo mapendekezo bali ndiyo sheria yenyewe.

Kinachojulikana ni kwamba, kutakuwa na serikali ya Muungano na hii ni rasimu ya sheria mama kwa serikali zozote zitakazo kuja.

Kuna watu wanafikiri ngoma ndiyo imeisha wakati ngoma ndiyo inaanza kabisa. Kazi ngumu ndiyo inaanza ambapo kwa sasa makundi katika jamii atleast, yameona mwelekeo wa katiba mama utakuwaje.

Mvulugano na mvutano wa kimaslahi ndiyo unaanza. Tegemea maandamano kwa wingi na kipigo cha polisi!!.
 
Yaani baba lizy atawale vipindi vitatu?! Hadi 2020 hii Katiba italeta machafuko tanganyika!! Lazima tupinge kipengere hicho

JK anakusudia kuomba urais wa Tanganyika.

Warioba ametengeneza ulaji kwa CCM.


"Watanzania ni kichwa cha mwendawazimu." - Ali Mwinyi.
 
Hilo suala la kumwachia kuteua then ashauriwe na baraza la usalama la Taifa hapo kuna shida tayari................ kwa nini wateuliwa wasiwe interviewed na bunge ama kamati huru ndani ya bunge na kuthibitishwa na bubge? kwani baraza la usalama la Taifa ndo kina nani lipo Rais si miongoni mwao?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Sera za chama
zinaweza kuwa mashairi matamu sana yenye watakelezaji wabovu. Ni heri
tukachagua mtu kulingana na utendaji wake. Gharama za kurudia uchaguzi
si tatizo kama zitangapangwa na kutumika vizuri.

ndio maana kuna mgombea binafsi, wa chama ataongozwa na sera za chama, na unayempenda wewe jitahidi umsaidie asimame mwenyewe kama mgombea binafsi..akili ndogo tu inatosha kuelewa hilo
 
1. Serikali tatu ktk Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Viti Maalum (Ubunge) hakuna
3. Kuongezwa ngazi moja ya juu ya mahakama (Supreme Court)
4. Mgombea huru ruksa (Urais na Ubunge)
5. Kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais mahakani ruksa
6. Hakuna uchaguzi mpya (Ubunge na Urais) kama aliyekuwepo amekufa/amejitoa isipokua kama alieacha kiti alikua mgombea huru.
7. Kuundwa tume huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom