RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Sasa tutakuwa na viongozi full wa Tanganyika huru.. Hatuhitaji tena mseto kwenye Tanganyika yetu..
Slaa Rais zitto makamu, mbowe waziri mkuu, tundu lisu mwanasheria mkuu, lema Mambo ya ndani, Abdalla safari sheria na katiba, Ally banaga kazi vijana, silinde tamiseni, lema mambo ya ndani, Nasarri sayansi na Teknolojia... Suzan elimu ...
Umelogwa wewe, ondoa uchafu huo hapa, hii ni katiba ya nchi sio ya chadema
 
Nampongeza warioba, nampongeza kikwete naipongeza ccm, naeapongeza watanzania, tz tunayoitaka ileeee
 
Bado nina wasiwasi na katiba rasimu hii! Bado inampa mamlaka makubwa sana rais hadi anweza ingilia muhimili wa Mahakama. Rais anateua jaji Mkuu na Makamu wake! Sijaona maana yake. Pili kama tumekubaliana serikali tatu ya muungano basi kuwe na Serikali ya zanzibar, Tanganyika na ya Muungano. Tunapenda jina letu.

Bado naendelea kusoma ila naomba soft copy iwekwe kwenye mtandao yusome na tujue ili tuichambue vizuri. Katiba ni muhimu kwa maisha yetu ya sasa na baadae.
 
Hongera sana mzee kikwete, watanzania tutakukumbuka kwa hili
 
Hii ndio katiba mpya tuliyokuwa tunaitaka, mgombea binafsi sasa poa, serikali ya tanganyika, mahakama ya juu, hakuna cha viti maalum hapa, ukomo wa ubunge sio ubunge unakuwa wa mtu mmoja tangu anazaliwa hadi kifo ye mbunge tuuuuuuu
 
Narudia tena Kabla ya tarehe 26 Aprili 1964 kulikuwa kuna nchi iliyokuwa ikiitwaTanganyika na si Tanzania bara. Msikubali kupotoshwa.
 
Ningependa zaidi tuwe na katiba za zanzibar na tanganyika kwanza ndipo hii ya muungano ije baadaye.

Hivi madaraka ya rais wa muungano dhidi ya wale wa nchi shiriki yakoje/yatakuwaje?

Na wanaposema mawaziri/wizara 15 wanamaanisha nini wakati muungano utakuwa na wizara saba ? Hizi zingine zinatoka wapi? Just confused.

Wenyewe kina Warioba, Baregu ete la, kwisha weka pesa mfukoni. Kazi kwetu wadanganyika.
 
Mkuu Tuko hii ni rasimu ambayo itajadiliwa na makundi ambayo yameanishwa kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba.

Kumbuka kuna mabadiliko tena yatafanyika kulingana na jinsi vikundi/makundi yatakavyo pendekeza ambapo bunge la katiba ndilo litakalo pitisha hii sheria mama.

Mpaka sasa hatujajua na wajumbe wa tume hawajajua kwa uhakika ni serikali ngapi zitakuwepo, kwa maana hiyo, huwezi kuanza kutafuta katiba kwa serikali ambazo hazipo na hazijulikani kama zitakuwepo. Kufanya hivyo, ni kujichukulia madaraka ya kidikteta na kuonyesha haya siyo mapendekezo bali ndiyo sheria yenyewe.

Kinachojulikana ni kwamba, kutakuwa na serikali ya Muungano na hii ni rasimu ya sheria mama kwa serikali zozote zitakazo kuja.

Kuna watu wanafikiri ngoma ndiyo imeisha wakati ngoma ndiyo inaanza kabisa. Kazi ngumu ndiyo inaanza ambapo kwa sasa makundi katika jamii atleast, yameona mwelekeo wa katiba mama utakuwaje.

Mvulugano na mvutano wa kimaslahi ndiyo unaanza. Tegemea maandamano kwa wingi na kipigo cha polisi!!.
Kwa mantiki hii mkuu endapo rasimu hii ikiwa katiba, ina maana katiba ya sasa inafutika. Hapo itakuwa 2014. Ni ipi hatma ya uchaguzi mkuu ujao?
 
pamoja na baadhi ya mambo mazuri ya rasimu ya katiba lakini naona kama ilikuwa inafanya kazi chini ya mapendekezo ya serikali kwani kuna kauli za ccm kjuwataka wanachama wake wajiandae kwa serikali tatu wqananchi walitakiwa kuachiwa maamuzi kama wanataka serikali moja,mbili au tatu na sio wao kuwaamulia wananchi,suala la uraia wa nchi zaidi ya moja pia wananchi walitakiwa watoe maamuzi na sio watu wachache,kinga ya rais ya nini wamepoteza pesa za kodi yetu bure hatuhitaji kumpa rais kinga
 
Unaposema tanzania bara na tanzania visiwani ni kiini macho kwani huku tanganyika pia kuna visiwa sasa sielewi kwa nini hili jina limezikwa na wanatumia tanzania bara ambalo sio sahihi waseme tu TANGANYIKA NA zanzibar sio tanzania bara kwani iliyoungana na zanzibar sio tanzania bara bali TANGANYIKA
 
Naapia kwa Mungu wa Mbinguni!;CCM HAWATAIPITISHA rasimu hii!

cha serikali 3,kipengele cha Tume huru,kipengele bunge lithibitishe Majaji na kipengele cha haki ya vyombo vya habari ni kabuli la CCM!
CCM wakipitisha rasimu hii 2015 watashindwa vibaya kwenye sanduku la kura

Kudos to Jugde Warioba and his CO
 
Mkuu wa Jeshi la Wananchi na la Polisi nao waidhinishwe na bunge.
 
RASIMU YA KATIBA


DHANA YA RASIMU SIFURI YA MAPENDEKEZO YA WADAU KUHUSU KATIBA MPYA YA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA TANZANIA

SURA Rasimu ina Sura 15, ibara 130 na nyongeza tatu.
Sura ya kwanza inahusu Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania na watu wake. uk. 1-4
Sura ya pili inahusu maadili na misingi mikuu ya taifa. uk. 5-7
Sura ya tatu inahusu haki kuu za binadamu na wajibu muhimu uk.7-21
Sura ya nne inahusu serikali ya shirikisho uk. 22-42
Sura ya tano inahusu Bunge la shirikisho uk. 43-63
Sura ya Sita inahusu mahakama kuu ya shirikisho uk. 64-67
Sura ya Saba inahusu Mahakama ya Rufani ya Shirikisho uk. 68-73
Sura ya nane inahusu vyombo vya dola vya Tanganyika na Zanzibar uk. 74-78
Sura ya Tisa inahusu sekretarieti ya Maadili uk. 79-80
Sura ya kumi inahusu masharti kuhusu fedha za Shirikisho uk. 81-88
Sura ya ya Kumi na moja inahusu madaraka ya umm auk. 88
Sura ya kumi na mbili inahusu majeshi ya ulinzi uk. 89
Sura ya kumi na tatu inahusu mamlaka ya kutunga katiba uk. 90-92
Sura ya Kumi na nne inahusu Tuma mbalimbali za taifa uk. 92-99 na
Sura ya kumi na tano inahusu mengineyo uk. 99-105
NYONGEZA:
Rasimu sifuri ina nyongeza tatu kama ifuatavyo:
(i) Nyongeza kuhusu mambo ya shirikisho (ii) Nyongeza kuhusu mambo yasiyo ya shirikisho na (iii) Nyongeza kuhusu idadi ya wizara za shirikisho
1
SURA YA KWANZA JAMHURI YA SHIRIKISHO YA TANZANIA NA WATU WAKE
TANGAZO LA JAMHURI 1. (1) Nchi yetu ni Tanzania na ni jamhuri ya shirikisho iliyoundwa kutokana na muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar na itaitwa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania;
(2) Eneo la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni eneo lote la Tanganyika na bahari yake pamoja na eneo lote la Zanzibar na bahari yake;
(3) Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni nchi moja yenye dola moja na vyombo mbalimbali vya utekelezaji wa mamlaka ya dola;
(4) Tanganyika itaitwa jimbo la Tanganyika na Zanzibar itaitwa jimbo la Zanzibar na kila jimbo litaongozwa na Gavana.
WATU WA TANZANIA 2.(1) Uraia wa Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania ni wa kuzaliwa kwa wenyeji wa nchi na kuasilishwa kwa wageni;
(2) Wananchi wa Tanzania wataitwa Watanzania na watakuwa na haki ya uraia kwa mujibu wa Katiba hii na sheria zitakazotungwa na Bunge la Shirikisho la Tanzania kwa ajili hiyo;
(3) Watu wote waliokuwa raia wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1964 ni raia wa Tanzania;
(4) Mtu yeyote ambaye amezaliwa baada ya tarehe 26 Aprili, 1964 hali wazazi wake wote wawili wakiwa raia wa Tanzania ni raia wa Tanzania;
(5) Mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania baada ya tarehe 26 Aprili, 1964 hali mmoja wa wazazi wake ni raia wa Tanzania ni raia wa Tanzania isipokuwa kama ataamua vinginevyo;
2
(6) Bunge laweza kutunga sheria itakayoweka masharti ya kuwawezesha watu wasiokuwa raia wa Tanzania kuwa raia kwa kuasilishwa.
DOLA YA KIDEMOKRASIA 3.(1) Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na haki za binadamu zilizotamkwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na katika Mkataba wa Haki za Binadamu na za Watu wa Umoja wa Afrika zitakuwa na nguvu za kisheria na zitachukuliwa kama ni sehemu ya Katiba hii.
(2) Bunge la Jamhuri ya Shirikisho ya Tanzania halitatunga sheria inayofuta au kupunguza nguvu haki za binadamu zilizoainishwa katika katiba hii, na mahakama zitafafanua na kufasiri haki hizo kwa kuzipatia nguvu kadri inavyowezekana badala ya kinyume chake;
(3) Sheria yoyote inayobadili masharti yanayogusa haki za binadamu zilizoainishwa katika katiba hii itapitishwa kwa azimio la Bunge lililoungwa mkono na kura zisizopungua theluthi mbili ya wabunge wote na kwa hali yoyote ile Bunge halitatunga sheria inayofuta mfumo wa vyama vingi vya siasa.
MFUMO WA SHIRIKISHO 4.(1) Utawala wa dola utafuata mfumo wa shirikisho utakaozingatia mgawanyo wa mamlaka ya dola kati ya mihimili mitatu yenye mamlaka ya utendaji, utoaji haki, na kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma;
(2) Muhimili wenye mamlaka ya utendaji utakuwa na Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
(3) Muhimili wenye mamlaka ya utoaji haki utakuwa na Mahakama Kuu ya Shirikisho, Mahakama Kuu ya Tanganyika, Mahakama Kuu ya Zanzibar na Mahakama ya
3
Rufani ya Shirikisho na vyombo vingine vya utoaji haki vitakavyoundwa kwa mujibu wa Katiba hii na sheria za nchi;
(4) Muhimili wenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma utakuwa na Bunge la Shirikisho, Baraza la Wawakilishi la Tanganyika na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar;
MGAWANYO WA MADARAKA 5.(1) Pamoja na mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili ya dola, kutakuwa pia na mgawanyo wa madaraka na shughuli za dola kati ya mambo ya Shirikisho kwa upande mmoja, na mambo ya Tanganyika na mambo ya Zanzibar kwa upande wa pili kama ilivyoorodheshwa katika Nyongeza ya Kwanza iliyoko mwishoni mwa Katiba hii;
(2) Kila chombo kilichotajwa katika ibara hii kitaundwa na kutekeleza majukumu yake kwa kufuata masharti yaliyomo katika Katiba hii, Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar;
(3) Mihimili mitatu ya dola, yaani vyombo vya kutunga sheria, Mahakama na serikali vitafanya shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliana kila mmoja ukichunga na kudhibiti utendaji kazi wa mwingine;
(4) Katika kutekeleza majukumu yake kama ilivyoagizwa kwenye ibara ndogo ya kwanza ya ibara hii, vyombo vya dola vyenye mamlaka ya Shirikisho vitakuwa na kipaumbele cha kwanza kuliko vyombo vya dola vinavyotekeleza mamlaka ya Tanganyika na Zanzibar; ilmradi kwamba majukumu yaliyokabidhiwa kwa Tanganyika na Zanzibar hayatakabidhiwa na kutekelezwa na vyombo vya dola vya Shirikisho. Majukumu yaliyokabidhiwa kwa Shirikisho yanaweza kukabidhiwa kwa vyombo vya dola vyenye mamlaka vya Tanganyika na vya Zanzibar ili yatekelezwe na vyombo hivyo kwa niaba ya Shirikisho.
4
VYAMA VYA SIASA 6.(1) Wananchi wanao uhuru wa kuunda vyama vya siasa kwa mujibu wa Katiba hii na vitawajibika kuuwezesha umma kujenga hoja, kauli na ushiriki katika uendeshaji wa dola kwa njia za kidemokrasia;
(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa Tanzania yatafanywa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria zilizotungwa na Bunge la Shirikisho la Tanzania kwa ajili ya hiyo;
(3) Bunge halitaweka masharti yanayokera au kukwamisha uanzishaji wa vyama vya siasa ama masharti ya uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa yanayokinzana, kuvunja masharti au haki nyingine zilizowekwa na Katiba hii

>>>>>>INAENDELEA HADI UKURASA WA 110


UNAWEZA KUDOWNLOAD FULL DOCUMENT HAPA CHINI (KURASA 110)
 
Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania kwa kiingereza ni Federal Republic of Tanzania. Taifa la United Republic of Tanzania halitakuwepo tenaI
 
Nimeona hawa wazee wanapendekeza wizara ya "Posta, Simu na mawasiliano". Sidhani miaka 40 ijayo bado kutakuwa na posta na simu
 
Hii rasimu ya Katiba ni usanii wa Warioba na Bosi wake Kikwete.
Ukiisoma utapata utata mtupu na kuchanganyikiwa, kwa mfano:
KUHUSU MUUNGANO
1/Tunaona neno shirikisho kila mahali, Je ni akinani walitaka shirikisho? Nini tofauti kati ya Muungano na shirikisho? Je hatuutaki tena muungano? Je shirikisho ndio mbadala wa muungano?

2/Katiba hii ni ya Tanzania, maajabu inazungumzia namna mamlaka ya Zanzibar yanapaswa kuwa nje ya muungano, wakati zanzibar wana katiba yao inayowaongoza. Lakini pia inazungumzia mamlaka ya Tanganyika nje ya muungano wakati Tanganyika haipo kisheria na wala haina katiba wala mamlaka yake ya kipee yake.
 
Back
Top Bottom